Mkutano wa biashara na maendeleo wa Umoja wa Mataifa tarehe 13 mjini Geneva ulitoa taarifa ya uchumi na maendeleo ya Afrika mwaka 2005 ukiainisha kuwa, uwekezaji wa kimataifa umeongezeka kwa kiasi barani Afrika miaka ya karibuni, lakini hautumiwi vizuri.
Taarifa hiyo imeainisha kuwa thamani ya uwekezaji wa kimataifa barani Afrika ilikuwa dola za kimarekani bilioni 2.2 katika miaka ya 80 karne iliyopita, na thamani hiyo iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 6.2 katika miaka ya 90. Thamani hiyo ilikuwa dola za kimarekani bilioni 13.8 mwaka 2003 na ilifikia dola za kimarekani bilioni 18 mwaka 2004.
Lakini taarifa hiyo inaona kuwa nyuma ya thamani hiyo iliongezeka kwa mfululizo, ukweli wa mambo usiofuatiliwa na watu ni kuwa asilimia ya ongezeko la thamani ya uwekezaji wa kimataifa barani Afrika ilipungua kuliko lile la jumla ya thamani ya uwekezaji wa kimataifa duniani.
Taarifa inaona kuwa uwekezaji wa kimataifa umetumiwa katika nchi chache barani Afrika. Kwa mujibu wa takwimu, nchi kumi za Afrika ambazo ni Morocco, Guinea ya Ikweta, Angola, Sudan, Nigeria, Chad, Afrika Kusini, Libya, Algeria na Tunisia zimevutia asilimia 75 ya jumla ya uwekezaji wa kimataifa barani Afrika, tena uwekezaji huo umetumiwa hasa katika sekta ya madini na kuzalisha mafuta. Kwa hiyo taarifa hiyo inaona kuwa mfumo wa uwekezaji wa kimataifa barani Afrika umepunguza kiasi cha ongezeko la juu zaidi la uchumi la bara la Afrika.
Taarifa imeainisha kuwa ongezeko la chini la uwekezaji wa kimataifa barani Afrika ni kuwa uwekezaji huo ulitoka katika nchi chache zilizotawala kikoloni nchi za Afrika. Katika miaka 20 toka mwaka 1080 hadi mwaka 2000, uwekezaji wa Ufaransa, Uingereza pamoja na Marekani ulichukua asilimia 70 ya uwekezaji wa kimataifa barani Afrika. Zaidi ya hayo, kutokana na kuathiriwa na mzigo mkubwa wa deni la nje, na faida kubwa zinazopatikana na uwekezaji wa kimataifa, kiasi cha fedha zilizotoka nje ya bara la Afrika kilizidi mara dufu kile cha mitaji ya kigeni iliyowekezwa barani Afrika.
Taarifa inaona kuwa ingawa nchi za Afrika zimefanya jitihada kubwa, lakini katika miaka 20 iliyopita maendeleo ya uchumi na jamii na mafanikio ya kupunguza umaskini hayakuwa makubwa. Kutotumiwa vizuri kwa uwekezaji wa kimataifa ni chanzo muhimu cha kusababisha hali hiyo. Taarifa hiyo inatetea kuwa jumuiya nzima ya kimataifa ingefikiri kwa makini katika masuala ya namna kuvutia kiasi kikubwa cha uwekezaji wa kimataifa na kutumia vizuri uwekezaji huo. Taarifa inaona kuwa wawekezaji wageni wanapaswa kuzingatia masuala maalum katika maendeleo ya Afrika na kuzingatia udhaifu wa mfumo wa uchumi wa Afrika na hali ya kutegemea uuzaji wa mazao asili katika nchi za nje kwa muda mrefu. Viongozi wa kutoa mkakati wa nchi za Afrika wangejifunza uzoefu mwafaka wa maendeleo ya nchi za Asia na kuchukua kuvuta na kutumia vizuri uwekezaji wa kimataifa kama sehemu moja ya mkakati wa maendeleo nzima ya taifa na kuleta mazingira mwafaka kwa uwekezaji huo kuingia kwenye nchi zao ili kupata maendeleo endelevu ya uchumi kwa ukamilifu na uratibu.
Idhaa ya Kiswahili 2005-09-14
|