Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-15 16:29:20    
Mkutano wa viongozi wakuu wa mataifa wa kuadhimisha miaka 60 ya Umoja wa Mataifa wafunguliwa

cri

Mkutano wa viongozi wakuu wa mataifa wa kuadhimisha mwaka wa 60 tokea Umoja wa Mataifa uanzishwe ulifunguliwa tarehe 14. Viongozi wakuu na wajumbe kutoka nchi 170 walihudhuria ufunguzi huo. Rais Hu Jintao wa China alitoa hotuba kwenye ufunguzi na mikutano mingine.

Ufunguzi uliendeshwa na mwenyekiti wa awamu ya 59 ya Umoja wa Mataifa, rais Omar Bongo wa Gabon na waziri mkuu wa Sweden Bw. Goran Persson.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan alitoa hotuba, akitaka nchi zote zitumie fursa hiyo kusukuma mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Alisema,

"Kutokana na uongozi wa mwenyekiti wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jean Ping, hatimaye mswada wa taarifa ya mageuzi ulipitishwa, waraka huo unahusika na bahati ya watu wa dunia."

Rais Hu Jintao kwenye hotuba yake alieleza hatua zitakazochukuliwa na China ili kuzisaidia nchi zinazoendelea. Alisema,

"China itatoa msamaha wa kodi kwa baadhi ya bidhaa kutoka kwa nchi maskini sana 39 zenye uhusiano wa kibalozi na China; itaongeza misaada kwa nchi maskini zenye madeni makubwa, na katika muda wa miaka miwili ijayo China itafuta madeni yote yenye riba ndogo na isiyo na riba iliyopangwa kulipa kabla mwishoni mwa mwaka 2004; na katika muda wa miaka mitatu ijayo China itatoa mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 10 kwa nchi zinazoendelea ili kuzisaidia nchi hizo katika ujenzi wa miundo mbinu na kusukuma ushirikiano wa ubia wa mashirika ya pande mbili; na katika muda wa miaka mitatu ijayo itaongeza misaada kwa nchi zinazoendelea, hasa nchi za Afrika katika mambo ya tiba na kuandaa wahudumu wa afya; katika muda wa miaka mitatu ijayo itawaandaa wataalamu elfu 30 wa kazi mbalimbali."

Hatua hizo za China zimesifiwa na viongozi waliohudhuria mkutano huo na hasa viongozi wa nchi zinazoendelea.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilifanya mkutano katika siku hiyo. Mada ya mkutano huo ilikuwa ni kujadili tishio linaloikabili jumuiya ya kimataifa na mageuzi ya baraza hilo.

Kwenye mkutano huo, rais Hu Jintao alisema, ili kulinda amani, baraza la usalama lazima liheshimiwe, na mfumo wa pamoja wa usalama lazima uimarishwe, ili baraza hilo litekeleze vilivyo katiba ya Umoja wa Mataifa. Kuhusu mageuzi ya Baraza la Usalama rais Hu Jintao alisema,

"Baraza la Usalama lazima lishikilie sera ya pande nyingi na liheshimiwe. Katika masuala makubwa kuhusu amani na usalama wa dunia baraza hilo lazima lifanye uamuzi kwa mujibu wa hali ilivyo na kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa Mataifa."

Aidha, rais Hu Jintao alisema, ni lazima kufanya mapambano dhidi ya tishio kwa mafanikio. Jumuyia ya kimataifa inapaswa iimarishe ushirikiano na kupambana na ugaidi wa aina zote, kusukuma na kutatua masuala ya umaskini na ubaguzi wa kijamii ili kung'oa mzizi wa ugaidi. Alisema,

"Ahadi zilizotolewa lazima zitimizwe, na baraza hilo lisikilize matumaini na maoni ya nchi za Afrika na kuzingatia matumaini yao ya kutaka amani, maendeleo na ushirikiano, na kuwafanya watu wa Afrika waone kweli kuwa familia ya kimataifa inajali.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-15