Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-15 18:43:18    
Maoni ya Afrika kuhusu suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa

cri
    Mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu kuanzishwa Umoja wa mataifa unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa na washiriki wa mkutano ni mageuzi ya Umoja wa Mataifa, maoni ya Umoja wa Afrika wenye nchi wanachama 53 yanazingatiwa zaidi. Umoja wa Afrika unatarajia amani na maendeleo ya Afrika vipatikane katika mageuzi ya Umoja wa Mataifa na kutarajia baraza la usalama lipanuliwe, ili kuimarisha maslahi ya nchi za Afrika.

    Hivi sasa bara la Afrika lina watu milioni 860 ikiwa ni 13.6% ya jumla ya idadi ya watu wa duniani, lakini nafasi ya uchumi wake ni 1% tu ya uchumi wa dunia na thamani ya biashara yake ni 2% tu ya ile ya dunia. Kati ya nchi 49 ambazo ziko nyuma kabisa kimaendeleo duniani, nchi 34 ziko katika bara la Afrika. Kati ya nchi 38 zenye madeni makubwa duniani, nchi 32 ni za Afrika. Tokea muda mrefu uliopita bara la Afrika liko katika hali ya umaskini.

    Umaskini na njaa si kama vinatishia maisha ya waafrika, bali pia ni chanzo muhimu cha kusababisha migogoro ya kijamii na kibinadamu na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi katika baadhi ya nchi za Afrika. Hivyo nchi nyingi za Afrika zinaona kuwa suala la maendeleo lingekuwa suala linalopewa kipaumbele katika majadiliano kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa.

    Mkutano wa milenia wa wakuu wa nchi wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwaka 2000 ulipitisha "Azimio la Milenia". Sasa miaka mitano imeshapita, lakini hatua za nchi nyingi za Afrika za kutekeleza lengo la maendeleo la milenia bado ziko nyuma sana na kiwango kinachotakiwa kutokana na upungufu wa fedha, mazingira mabaya ya kimaumbile na sera zisizo za haki katika biashara ya kimataifa. Endapo hatua thabiti hazitachukuliwa, nchi hizo zitashindwa kabisa kutimiza lengo hilo.

    Msingi wa viwanda wa nchi nyingi za Afrika ni dhaifu sana ambazo zinapata fedha za kigeni kwa kutegemea kusafirisha nje maliasili na mazao-ghafi. Mazingira ya usafirishaji bidhaa kwa nchi za nje ya nchi za Afrika yameharibika vibaya katika miaka ya karibuni kutokana na vizuizi vilivyowekwa na nchi za viwanda za magharibi.

    Hivyo, nchi za Afrika zinaona kuwa jambo la haraka la kutimiza lengo la maendeleo la milenia ni nchi za viwanda ziondoe vizuizi vya biashara na kuongeza misaada kwa nchi za Afrika. Mbali na hayo, nchi za Afrika zinaona kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya jitihada zaidi, kuanzisha utaratibu mwafaka na wa haki wa kimataifa katika biashara na mambo ya fedha duniani, kuongeza haki za kujiamulia mambo na kushiriki za nchi zinazoendelea, ambazo zinapokea misaada ya kimataifa na kuanzisha mazingira ya uchumi wa kimataifa yanayonufaisha nchi zinazoendelea.

    Jambo linalofurahisha ni kuwa ingawa ulipingwa sana na Marekani, "mswada wa nyaraka za matokeo" uliopitishwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa kabla ya kufanyika kwa mkutano wa wakuu wa nchi, bado umebakiza maneno ya kutaka nchi za viwanda kutekeleza ahadi zilizotoa za kuongeza misaada ya maendeleo hadi 0.7% ya jumla ya thamani ya uzalishaji mali nchini.

    Habari zinasema kuwa katika kipindi cha mkutano huo wa wakuu wa nchi, Umoja wa Afrika huenda utafanya shughuli nyingine za kueleza msimamo wake kuhusu suala la mageuzi ya baraza la usalama. Kuhusu suala la mageuzi ya baraza la usalama rais Obasanjo wa Nigeria anataka uwakilishi wa bara la Afrika ungeonekana zaidi katika baraza hilo.

    Kuhusu suala la mageuzi ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika katika azimio la mkutano wa wakuu wa nchi wa Silte ulisema kuwa, Afrika inagombea nafasi mbili za ujumbe wa kudumu wenye haki ya kupiga kura ya turufu katika baraza la usalama.

Idhaa ya Kiswahili