Ofisa wa shirika la nishati ya atomiki duniani alidokeza tarehe 15 mjini Vienna kuwa, juhudi zilizofanywa na Marekani na Umoja wa Ulaya kwa kufikisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa zimepingwa vikali na shirika hilo, na nchi nyingi pia zimeeleza kupinga kitendo hicho. Wachambuzi wanaona kuwa mkutano wa bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo utakaofanyika Jumatatu ijayo huenda hautatoa uamuzi wa kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Tangu tarehe 8 mwezi Agosti, Iran iliporejesha shughuli za kubadilisha uranium, nchi tatu za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza zinazouwakilisha Umoja wa Ulaya kufanya mazungumzo na Iran zilitishia kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama. Upande wa Washington hata ulisistiza tena kuwa, kama Iran haitasimamisha shughuli hizo, Marekani haitaondoa uwezekano wa kuchukua hatua yoyote. Iran imeonesha msimamo wake imara. katika kukabiliana na tishio hilo. Ingawa inataka kuendelea na mazungumzo na Umoja wa Ulaya, lakini ilieleza kuwa kamwe haitarudi nyuma kwenye suala hilo. Iran ilisisitiza kuwa lengo la Marekani na Umoja wa Ulaya kufikisha suala la nyuklia kwenye baraza la usalama halina msingi wa kisheria.
Baraza la wakurugenzi la shirika la nishati ya atomiki duniani ni idara pakee inayoweza kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama. Nchi nyingi wanachama za shirika hilo zinatetea kutatua migongano kwa njia ya kidiplomasia na mazungumzo, na kupinga kutishia nchi husika kwa kufikisha kutokuelewana kwenye baraza la usalama, na tena zinapinga nchi hizo kutishia kwa nguvu za kisilaha. Hata kutatua suala la nyuklia la Iran pia kunapaswa kufanywa hivi.
Nchi hizo zinaona kuwa Iran kuanzisha upya shughuli za uranium kwa kusimamiwa na shirika la nishati ya atomiki duniani hakuvunji mkataba wa kutoeneza silaha za nyuklia. Zaidi ya hayo, Russia, China na India zenye athari kubwa kwenye baraza la wakurugenzi wa shirika hilo, hivi karibuni zimeeleza kuendelea kuunga mkono kutatua suala la nyuklia la Iran kwa mazungumzo ndani ya shirika hilo na kutokubali kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Hivi karibuni, Marekani na Umoja wa Ulaya siku zote zimezishawishi nchi wanachama za baraza la wakurugenzi la shirika hilo zikubali msimamo wa Marekani na Umoja wa Ulaya, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda. Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw. Mohamed El Baradi na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan wote hawakubali kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Vyombo vya habari vya Ulaya vimeainisha kuwa hata sasa, Umoja wa Ulaya bado unaitaka Iran irudi kwenye meza ya mazungumzo. Kutokana na sababu fulani, Umoja wa Ulaya hautaki kushindwa kwa Marekani kwenye suala la nyuklia la Iran na Umoja wa Ulaya pia unajua kuwa ni vigumu kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa hivi sasa.
Idhaa ya Kiswahili 2005-09-16
|