Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-19 21:28:08    
Ziara ya rais Hu Jintao yapata mafanikio

cri

Kati ya tarehe 8 na 17 mwezi Septemba, rais Hu Jintao wa China alifanya ziara ya kiserikali nchini Canada na Mexico, na kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wa mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Katika kipindi hicho Bw. Hu Jintao alifanya shughuli za kidiplomasia zaidi ya 50 na kupata mafanikio makubwa. Kabla ya kumaliza ziara hiyo, waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Li Zhaoxing aliwaeleza waandishi wa habari wa China walioufuatana na ujumbe kuwa, moja ya mafanikio ya ziara hiyo ni kuimarisha uhusiano wa kirafiki na kishirikiano kati ya China na nchi hizo mbili.

Mwaka 1997, China ilianzisha uhusiano wa kiwenzi na Canada. Katika ziara hiyo Bw. Hu Jintao na waziri mkuu wa Canada Bw. Paul Martin waliamua kukuza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuwa wa kiwenzi na kimkakati, kuhimiza ushirikiano wa pande zote na kuweka lengo halisi. Pande mbili zilisaini mikataba 7 ya ushirikiano ikiwemo ya maeneo ya safari za ndege, njia ya reli na nishati ya nyuklia.

China na Mexico ni nchi kubwa zinazoendelea na zinakabiliwa na jukumu la namna moja la maendeleo, hivyo kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili, lilikuwa ni jambo muhimu katika mazungumzo ya wakuu wa nchi hizo mbili. Pande zote mbili zimekubaliana kuchukua hatua halisi kuimarisha uhusiano wa kiwenzi na kimkakati na kuharakisha kubuni mpango wa pamoja wa utekelezaji.

Bw. Li Zhaoxing alisema kuwa, katika ziara yake Rais Hu Jintao alieleza msimamo wa serikali ya China kuhusu masuala makubwa ya kimataifa, kuhimiza kuanzishwa kwa utaratibu mpya wa kisiasa na kiuchumi wa kimataifa wa haki na mwafaka, na kulinda maslahi halali ya nchi zinazoendelea.

Mkutano wa wakuu wa nchi wa mwaka wa 60 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa ni mkutano mkubwa kabisa katika historia ya Umoja wa Mataifa ambao ulihudhuruiwa na wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa nchi wanachama karibu 170. Bw. Hu Jintao alishiriki kwenye mikutano mingi na kutoa hotuba. Kwenye mkutano wa wajumbe wote Bw. Hu Jintao alisisitiza kujenga amani ya kudumu, ustawi wa pamoja na dunia mwafaka na kutoa mapendekezo ya kushikilia utendaji wa pande nyingi, ushirikiano wa kunufaishana, moyo wa kuvumiliana, kuleta usalama na ustawi wa pamoja na kujenga dunia yenye masikilizano. Kwenye mkutano ngazi ya juu wa uchangiaji wa fedha za maendeleo, Bw. Hu Jintao alisema kuwa China inashikilia msimamo wa kuunga mkono madai ya haki ya nchi zinazoendelea, kutaka Umoja wa Mataifa uoneshe umuhimu mkubwa zaidi katika eneo la maendeleo na kutangaza kuwa, China itachukua hatua muhimu katika pande za ushuru wa forodha, madeni, mikopo yenye riba nafuu, mambo ya afya ya umma na uendelezaji wa nguvukazi, na kuunga mkono nchi nyingine zinazoendelea kuharakisha maendeleo yake.

Kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa Baraza la Usalama, Bw. Hu Jintao alisisitiza umuhimu wa Baraza la Usalama usioweza kubadilishwa katika utatuzi wa masuala ya amani na usalama duniani, kutaka kuhakikisha heshima ya Baraza la Usalama katika kutekeleza majukumu yanayoagizwa na katiba ya Umoja wa Mataifa na kuongeza ufanisi wa Baraza la Usalama; amelitaka Baraza la Usalama lifuatilie mambo ya Afrika na kuongeza uwekezaji. Kwenye mkutano wa majadiliano, Bw. Hu Jintao alisisitiza uungaji mkono wa China kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, kutaka mageuzi yazingatie mambo makubwa, kukuza demokrasia, kujadiliana na pande nyingi na kuyaendeleza kwa hatua madhubuti na pande zote.

Maoni hayo yanaonekana katika nyaraka za matokeo ya mkutano wa wakuu wa nchi na kupongezwa na viongozi wa nchi nyingi, hasa wa nchi zinazoendelea. Vyombo vya habari vinaona kuwa hatua zilizotangazwa na Bw. Hu Jintao za kuunga mkono nchi zinazoendelea kuharakisha maendeleo yake ni halisi, China ni rafiki wa kweli wa nchi zinazoendelea.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-19