Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-20 19:29:18    
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lafuatilia suala la umaskini duniani

cri

Mara tu baada ya kufungwa kwa mkutano wa wakuu wa nchi wa maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa, mkutano wa Baraza Kuu la 60 la Umoja wa Mataifa ulianzisha majadiliano ambapo wajumbe wa nchi zinazoendelea ambazo zinachukua theluthi 2 za idadi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, walitoa hotuba wakieleza ufuatiliaji wao kuhusu suala la mageuzi na maendeleo, kurekebisha kasoro zilizotokea huko nyuma za kufuatilia usalama na kupuuza maendeleo, walifanya suala la maendeleo, hasa suala la umaskini kuzingatiwa kwenye mkutano huo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa milenia wa Umoja wa Mataifa viongozi wa nchi mbalimbali waliwahi kuahidi kuwa watapunguza nusu ya idadi ya watu maskini kabla ya mwisho wa mwaka 2015. Katika majadiliano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wawakilishi wa nchi mbalimbali walipotathmini utekelezaji wa lengo la maendeleo la milenia waliona kuwa, sasa miaka mitano imeshapita, ingawa jumuiya ya kimataifa ilichukua baadhi ya hatua mwafaka, lakini ukitupia macho dunia nzima, jitihada za kupunguza idadi ya watu maskini bado zinakabiliwa na changamoto kali.

"Taarifa ya maendeleo ya binadamu mwaka 2005" ambayo ilitolewa na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa kabla ya kufunguliwa mkutano huo inasema kuwa, suala la umaskini duniani halipungui bali ni linakuwa na matatizo mengi zaidi. Endapo maendeleo yataendelea kuwa na kasi ya hivi sasa, kabla ya mwisho wa mwaka 2010 duniani bado kutakuwa na idadi ya watu milioni 800 ambao wanatumia chini ya dola moja ya kimarekani kwa siku, idadi hiyo ya watu ni kubwa karibu milioni 400 kuliko lengo lililowekwa. Licha ya hayo kutakuwa na watu kiasi cha milioni 170 ambao watakuwa wanatumia chini ya dola 2 kwa siku. Hali ya namna hiyo ikiendelea kuwa hivyo, lengo la maendeleo la milenia halitaweza kutimizwa. Taarifa hiyo pia ilitoa mfano kuwa nchi zilizoendelea zinazitoza nchi zinazoendelea nyongeza kubwa ya ushuru, huku zinatoa ruzuku kubwa kwa mazao ya kilimo ya nchi zao yanayosafirishwa nje, walisema kuwa vitendo hivyo vinaathiri sana maslahi ya nchi zinazoendelea.

Kwenye mkutano wa majadiliano, wajumbe wa nchi nyingi walipotoa hotuba walisisitiza kuwa, kukomesha umaskini siyo jukumu la nchi moja fulani, bali ni kuwa jumuiya ya kimataifa inatakiwa kufanya jitihada kwa pamoja, kuanzisha utaratibu na kanuni za kimataifa za haki, ili kufanya nchi zote kunufaika na maendeleo ya utandawazi wa uchumi. Wajumbe wengi walisema kuwa, kwa mtazamo wa kihistoria au kufuatana na hali halisi ya hivi sasa kusaidia nchi zinazoendelea ni jukumu la uwajibikaji kwa nchi zilizoendela.

Hali halisi ni kuwa Umoja wa Mataifa ulipitisha azimio mwaka 1970 likitaka nchi zilizoendelea kuongeza misaada ya kiserikali ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kwa kiasi cha 0.7% ya pato lake. Lakini hadi hivi sasa lengo hilo bado liko mbali sana kufikiwa. Wajumbe wa nchi nyingi walisema kuwa, umaskini ni chanzo muhimu cha mapambano ya kisilaha, ugaidi, migogoro ya kijamii na ubinadamu pamoja na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi, ambavyo vinatishia vibaya amani na maendeleo ya dunia. Hivyo kutokomeza umaskini ni jukumu la haraka zaidi kwa dunia ya leo. Hivyo walitoa wito wa kutaka nchi zilizoendelea kutekeleza kwa makini ahadi zilizotoa wakati zinapotoa misaada ya fedha, usafirishaji wa teknolojia, upunguzaji madeni na biashara ya haki.

Baadhi ya wajumbe walisisitiza kuwa hivi sasa utandawazi unapanuka kwa mfululizo, duniani bado kuna mamilioni kwa mamia ya watu ambao wanatishiwa na njaa, haifai kwa nchi tajiri kufuatilia manufaa yake tu, na zinaweza kushindwa kufanya hivyo. Ni kama baadhi ya wajumbe walivyosema kuwa, endapo lengo la maendeleo la milenia litashindwa kutimizwa, siyo tu nchi maskini zitapatwa na athari mbaya, hata nchi zilizoendelea zitashindwa kujiepusha na matokeo mabaya yanayosababishwa na suala hilo. Kwani nchi zote zinaishi kwa kutegemeana, usalama na maendeleo ya pamoja ya binadamu havitaweza kuhakikishwa endapo hazitaweza kutokomeza umaskini na njaa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-20