Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-20 19:37:18    
Idara nne za China zatoa mpango kwa ajili ya kazi ya uenezi wa habari kuhusu kujenga jamii inayobana matumizi ya maji

cri

Idara ya uenezi ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, wizara ya maji ya China, kamati ya maendeleo na mageuzi ya taifa na wizara ya ujenzi ya China hivi karibuni zilitoa uarifu kwa pamoja, zikipanga kazi ya uenezi wa habari kuhusu kujenga jamii inayobana matumizi ya maji.

Uarifu huo unasema kuwa, kauli mbiu ya kazi ya uenezi kuhusu kujenga jamii inayobana matumizi ya maji ya mwaka 2005 hadi mwaka 2006 ni "kufanya juhudi kubana matumizi ya maji, na kujenga jamii inayobana matumizi ya maji katika sekta mbalimbali". Tangazo hilo linasema kuwa, kujenga jamii inayobana matumizi ya maji ni hatua ya kimkakati na ya kimsingi katika kutatua tatizo la ukosefu wa maji nchini China. Hatua hiyo inasaidia kuimarisha usimamizi wa maliasili ya maji, kuinua uwezo wa kutumia maliasili ya maji na kupata faida kutoka maliasili hayo, kuzidi kuongeza uwezo wa kupata maendeleo endelevu; kuhifadhi mazingira ya mito, kuhakikisha utoaji wa maji salama, na kuinua ubora wa maisha ya umma; pia inasaidia kuanzisha utaratibu mzuri wa ugawaji wa maji wenye usawa kwa utatuzi wa suala la ukosefu wa maji, kusukuma mbele usimamizi na matumizi ya maliasili ya maji kwa mujibu wa sheria na kwa utaratibu, na kutoa mchango katika kujenga jamii ya kijamaa yenye masikilizano.

Uarifu huo umetoa matakwa kuwa, idara husika lazima zifanye juhudi kueneza habari kuhusu hali ya ukosefu wa maji katika mchakato wa kuendeleza uchumi na jamii nchini China, hasa kuonesha kuwa ujenzi wa jamii inayobana matumizi ya maji ni jambo la dharura linalopaswa kutimizwa, na ni muhimu sasa kwa kuinua uwezo wa uchumi wa China kupata maendeleo endelevu, kuhakikisha usalama wa maisha ya watu, uzalishaji na mazingira. Idara husika lazima ziwajulishe watu wengi kuhusu kanuni na matakwa husika ya sheria kadhaa ikiwemo sheria ya maji ya Jamhuri ya Watu wa China, kutoa kipaumbele katika kueneza habari kuhusu mageuzi na uvumbuzi wa utaratibu wa ujenzi wa jamii inayobana matumizi ya maji, utaratibu wa usimamizi wa kijamii unaoongozwa na serikali, kuongozwa na masoko na kushirikisha wananchi, na utaratibu wa kusukuma mbele jamii yote kubana matumizi ya maji kwa hatua mbalimbali. Tena idara husika lazima ziimarishe uenezi wa habari kuhusu hatua mpya za kusimamia maliasili ya maji, zikiwemo ugawaji wa matumizi ya maji, udhibiti na usimamizi wa kiasi cha matumizi ya maji, ujenzi wa masoko ya maji, maingiliano ya mamlaka za maji na mashirikisho ya watumiaji wa maji.

Uarifu huo linasisitiza kuwa, sehemu na idara mbalimbali na vyombo vya habari lazima vishirikiane katika kazi hiyo ili kupata maendeleo halisi, na kutumia njia ya kueneza habari kuhusu kubana matumizi ya maji zikisimamia matumizi ya maji kwa maoni ya raia; kueneza habari kupitia vyombo vya habari vya kisasa na vyombo vya habari vya jadi; kueneza habari katika sekta muhimu na sekta maalum; na kueneza habari kupitia vyombo vya habari na kupitia njia nyingine. Lazima zifanye kazi hiyo kwa njia mbalimbali kwa mujibu wa hali ya sehemu na sekta tofauti.

Idara za uenezi wa habari na kamati za Chama cha Kikomunisti cha China za sehemu mbalimbali lazima zitoe kipaumbele kwa kazi ya uenezi wa habari, na kuongoza na kuratibukazi hiyo. Na kamati za maendeleo na mageuzi, idara za maji, na idara za ujenzi za sehemu mbalimbali lazima zifanye shughuli husika kwa mujibu wa kauli mbiu ya "kufanya juhudi kubana matumizi ya maji na kujenga jamii inayobana matumizi ya maji" na kwa mujibu wa hali ya sehemu na idara hizo. Vijiji, mashirika, ofisi, shule na mitaa mbalimbali lazima ziandae vizuri shughuli za uenezi wa habari kwa mujibu wa mipango husika.

Tangazo hilo pia linataka vyombo vya bahari vifanye vizuri kazi ya uenezi wa habari kutokana na hali zao na za wasikilizaji, kuchukua uenezi wa habari hizo kuwa kazi muhimu, kutunga mpango wa kazi hiyo wa hivi karibuni na wa muda mrefu, kutoa mapendekezo kuhusu kazi hiyo, kupanga kwa makini, kushikilia kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu, kufanya juhudi ili kupata maendeleo halisi, na kufanya kazi hiyo kwa moyo wa kushugulikia mambo kihalisi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-20