Mkutano wa baraza la wakurugenzi la shirika la nishati ya atomiki duniani ulifanyika tarehe 19 mjini Vienna. Kwa kuwa muda wa mwezi mmoja na zaidi uliopita, Iran na Umoja wa Ulaya zote hazitaki kulegeza masharti kwenye suala la nyuklia la Iran, kweli mazungumzo yaliyoendelea kati yao katika miaka miwili iliyopita yamesimama, na suala hilo hatimaye limewasilishwa kwenye baraza la wakurugenzi la shirika hilo. Hivyo basi suala hilo limekuwa lenye utatanishi.
Mkutano huo utafanyika kwa siku tano. Kutokana na ratiba ya mkutano huo, ingawa suala hilo litaanza kujadiliwa tarehe 21, lakini Umoja wa Ulaya umetunga mswada wa azimio na kuusambaza kwa bodi ya wakurugenzi wa baraza hilo. Waraka huo umefichua habari mbalimbali kuhusu Iran kukiuka mkataba wa kutosambaza silaha za nyuklia na kutetea kulifikisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kuhusu jambo hilo, mjumbe wa Iran katika shirika la nishati ya atomiki duniani Bw. Mohammed Achondsadeh alieleza kuwa, kitendo hicho cha mpango wa Umoja wa Ulaya kitabadili suala la kiufundi linaloweza kutatuliwa kiurahisi, liwe suala kubwa la kisiasa. Alieleza pia, serikali ya Iran haitaki kupambana na Umoja wa Ulaya.
Vyombo vya habari vya Ulaya vimeainisha kuwa msimamo wa Umoja wa Ulaya unaonesha umoja huo umeacha uvumilivu na suala hilo mbele ya msimamo mkali wa Iran, huenda litatatuliwa kwa mapambano badala ya mazungumzo. Vinaona kuwa Umoja wa Ulaya kuamua kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama na kuiwekea vikwazo Iran sio chaguo zuri, labda kutasababisha hali ya kutodhibitiwa ambayo kila mmoja hataki kuiona.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani Bw. Mohammed El Baradei alieleza kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo kuwa, anapinga kutumia hatua ya kuweka vikwazo. Alieleza kuwa matunda yaliyopatikana mapema ya siku hiyo katika mazungumzo ya pande sita kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea yanaonesha kuwa mazungumzo ni njia nzuri kabisa ya kutatua tofauti kati ya pande hizo mbili. Bw Baradei anaona kuwa pendekezo alilotoa rais Mahmoud Ahmadi Nejad wa Iran kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa lina maoni mapya ambayo yanatakiwa kutathminiwa kiufundi.
Bodi ya wakurugenzi wa shirika la nishati ya atomiki duniani ni idara pekee yenye mamlaka ya kufikisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama. Bodi hiyo inaona kuwa Iran ikiwa nchi yenye mamlaka, haki yake ya kutumia nishati ya nyuklia kwa amani inalindwa na mkataba wa kutosambaza silaha za nyuklia. Marekani na Umoja wa Ulaya zinatetea vigezo viwili visivyokubaliwa na watu kwenye suala hilo. Bodi hiyo inaona kuwa kuanzishwa tena kwa shughuli za kusafisha uranium kwa Iran tarehe 8 mwezi Agosti hakuvunji mkataba huo, katika hali hiyo, baraza hilo halina msingi wa sheria kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Zaidi ya hayo, Russia, China na India zenye athari kubwa kwenye bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, zote zimeeleza kuunga mkono kutatua suala hilo kwa mazungumzo ndani ya mpango wa shirika hilo na kutokubali kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Ingawa Marekani na Umoja wa Ulaya zinashikilia kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama, lakini katika hali ya kutoungwa mkono na nchi nyingi wanachama wa bodi ya wakurugenzi, hazina budi kuchelewesha kutekeleza mpango wa kufikisha suala hilo kwenye baraza la usalama.
Idhaa ya Kiswahili 2005-09-20
|