Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-21 17:56:00    
Naibu katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ataka umuhimu wa Umoja wa Mataifa uimarishwe zaidi

cri

Mkutano wa wakuu wa nchi wa maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa ulifanyika hivi karibuni huko New York, ambapo wakuu wa nchi na viongozi wa serikali kutoka nchi kiasi cha 150 walikuwa na majadiliano kuhusu mageuzi ya Umoja wa Mataifa, maendeleo ya dunia na usalama wa pamoja, tena walipitisha "Waraka wa Matokeo" uliojumlisha mageuzi ya maeneo mengi. Naibu katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa ambaye ni kiongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Mataifa ya China Bw. Cui Yongjian alipohojiwa na mwandishi wa habari hivi karibuni alisema kuwa, anatarajia umuhimu wa Umoja wa Mataifa uthibitishwe wazi zaidi kwenye mkutano wa wakuu wa nchi.

Umoja wa Mataifa ni jumuiya moja kati ya serikali na serikali yenye uwakilishi na heshima kubwa, na inafanya kazi muhimu isiyoweza kubadilishwa katika mambo ya kimataifa. Katika miaka ya karibuni heshima ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikikabiliwa na changamoto, hali ambayo inafanya baadhi ya watu kuwa na mashaka kuhusu hadhi na umuhimu wake. Bw. Jin Yongjian anaona kuwa, kuna haja ya kuimarisha hadhi na umuhimu wa Umoja wa Mataifa kutokana na shughuli za maadhimisho ya mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa. Alisema:

"Moja ya kazi muhimu za Umoja wa Mataifa ni kubuni kanuni na sheria pamoja na makubaliano mbalimbali ya kimataifa. Ninatarajia harakati hizo zitathibitisha wazi hadhi na umuhimu wa Umoja wa Mataifa."

Katika mahojiano na mwandishi wa habari, Bw. Jin Yongjian alizungumzia suala nyeti la mageuzi ya Umoja wa Mataifa. Alisema kuwa ikilinganishwa na wakati wa mwanzoni baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mabadiliko makubwa sana yametokea katika pande za hali ya kimataifa, nchi wanachama wake pamoja na majukumu yake ya kihistoria. Ili kuendana na majukumu mapya katika hali mpya ya hivi sasa, Umoja wa Mataifa wa Mataifa unatakiwa kufanya mageuzi, hayo yamekuwa maoni ya pamoja ya nchi wanachama wote. Lakini kuna tofauti kubwa ya maoni kuhusu mambo halisi ya mageuzi pamoja na mambo yanayopewa kipaumbele. Nchi nyingi zinazoendelea zinafuatilia utatuzi wa masuala kuhusu utekelezaji wa "lengo la maendeleo la milenia", maendeleo na kutokomeza umaskini, wakati baadhi ya nchi chache zinasisitiza mageuzi ya baraza la usalama zikichukulia mageuzi kuwa ni nafasi nzuri ya kujipatia hadhi ya nchi za wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama. Kuhusu mambo hayo, Bw. Jin Yongjian alisisitiza kuwa, mageuzi ya Umoja wa Mataifa yanatakiwa yawe ni mageuzi ya pande zote. Alisema,

"Mageuzi ya mageuzi ya Umoja wa Mataifa ni mageuzi ya pande zote, mambo yanayofuatiliwa na nchi nyingi zinazoendelea siyo mageuzi ya baraza la usalama, bali ni kutaka Umoja wa Mataifa kuhimiza jumuiya ya kimataifa kutenda vitendo halisi kuhusu masuala ya maendeleo, kutokomeza umaskini na ukimwi wala siyo tu kukariri ahadi zilizotoa siku za nyuma."

Bw. Jin Yongjian alisema kuwa anatarajia Umoja wa Mataifa utafanya kazi muhimu zaidi katika kufuatilia na kulinda maslahi nchi zinazoendelea, kuhimiza amani na usalama, maendeleo ya uchumi na jamii, kulinda na kuhimiza haki za binadamu na utungaji wa kanuni za kimataifa juu ya msingi wa kuzingatia maslahi ya pande mbalimbali, na kuwa muundo wenye ufanisi na heshima kubwa zaidi.

Kuhusu uthibitishaji wa sifa za nchi zinazotaka kuwa nchi wajumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, rais Roh mo Hyun wa Korea ya Kusini alisema kuwa, kigezo cha kuwa nchi wa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama ni "uhalali wa maadili" wa mchango wake kwa amani ya dunia. Anaona kuwa kanuni hiyo ni yenye uwakilishi pamoja na lengo linalofuatiliwa. Aliongeza kuwa Umoja wa Mataifa ni jumuiya kati ya serikali na serikali wala siyo klabu ya matajiri au wakurugenzi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-21