Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-21 19:16:35    
China yazingatia elimu vijijini

cri

Tarehe 10 mwezi Septemba mwaka huu ilikuwa ni siku ya 21 ya walimu, tarehe 9 asubuhi, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao na mjumbe wa taifa wa China Bi. Chen Zhili wakifuatana na katibu wa kamati ya chama ya Beijing Bw. Liu Qi na meya wa Beijing Bw. Wang Qishan walitembelea shule za msingi na za sekondari zilizoko kwenye vitongoji vya Beijing na kuonana na walimu na wanafunzi wa huko.

Siku hiyo asubuhi, Bw. Wen na msafara wake walifika kwenye shule ya msingi ya Tanzhesi. Mara baada ya kushuka kutoka kwenye gari, Bw. Wen alisalimiana na walimu, na kutembea pamoja nao huku akiuliza hali ya shule hiyo na hali ya elimu ya watoto wa sehemu hiyo.

Akifuata sauti nyororo ya wanafunzi wakisoma vitabu, Bw. Wen alipanda ngazi na kuingia darasa la kwanza la kidato cha tano kwenye ghorofa ya pili?alimwona msichana mmoja akisoma makala moja inayoitwa MKONGOJO. Watoto hao walipomwona Bw. Wen wakamsalimia: "Shikamoo! Babu Wen!"

Bw. Wen aliwajibu "Marahaba! Kesho ni sikukuu ya walimu, tunapaswa kuwakumbuka walimu wetu, na kuwashukuru kivitendo upendo wa walimu

"Elimu inategemea moyo wa upendo." Bw. Wen aliendelea kusema, "Kwa walimu, kuwapenda wanafunzi ni jambo la muhimu kabisa, hali kadhalika, kwa wanafunzi, kuwaheshimu walimu pia ni jambo la muhimu kabisa. Leo mko hapa mnajifunza, baada ya kukua na kuwa watu wazima mtawakumbuka walimu wenu, si ndiyo?"

"Ndiyo!"watoto hao walijibu kwa kauli moja.

Bw. Wen alisema kuwa elimu ya shule za msingi ni mwazo wa elimu, niye watoto mnapaswa kuwa na nia, nayo ni kulihudumia taifa kwa kutumia utaalamu wenu na jasho lenu."

Baada ya kuondoka kutoka kwenye shule ya msingi ya Tanzhesi, Bw. Wen na msafara wake walitembelea shule ya sekondari ya Tanzhesi, waliingia kwenye darasala kwanza la kidato cha pili, na kuwaona wanafunzi wakikaa kwa kutazama uso kwa uso. Mwalimu alimwambia Bw. Wen kuwa kukaa namna hiyo kuna warahisishia wanafunzi kujadiliana.

Bw. Wen alisifu njia hiyo akisema, ni vizuri wanafunzi walijiulize na kujibu maswali hayo wenyewe, kwani wakitaka kupata elimu, wanatakiwa kuchemsha ubongo wenyewe na kuongeza uwezo wa uvumbuzi.

Alimwambia mwalimu kuwa kuchemsha ubongo hakutoshi, vilevile wanafunzi wanatakiwa kujua jinsi ya kutumia ujuzi waliopata katika kutatua masuala maishani, na hiyo ndiyo ilikuwa dosari ya elimu ya zamani ya China. Pia alisema, walimu hawatakiwi kuwaambia wanafunzi vitu vyote, badala yake wanapaswa kuwaelekeza ili wagundue maswali wenyewe, kudadisi maswali hayo na kujipatia majibu.

Kuanzia mwaka huu, Beijing itapeleka walimu wapatao 1000 kila vijijini ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza kiwango cha elimu vijijini. Bw. Wen alitoa mapendekezo mawili, la kwanza, hatua hiyo ya Beijing inapaswa kuenezwa kote nchini China; la pili, kuwahamasisha wanafunzi wanaohitimu kutoka vyuo vikuu wafanye kazi ya ualimu katika shule za msingi, ili kuongeza kiwango cha elimu ya msingi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-21