Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-23 21:15:33    
Mapishi ya kupiga vipande vya nyama ya nguruwe na matango machungu

cri

Mahitaji

Vipande vya nyama ya nguruwe gramu 250, matango machungu gramu 500, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi na pilipili manga, M.S.G, sosi ya pilipili, wanga kijiko kimoja, chumvi kijiko kidogo, mchuzi wa soya kijiko kimoja, sukari kijiko kimoja, mafuta vijiko saba

Njia

1. Weka vipande vya nyama ya nguruwe kwenye bakuli moja na tia wanga kisha korogakoroga. Kata matango machungu yawe vipande, tia chumvi korogakoroga, baada ya dakika 15 uviweke kwenye maji na osha chumvi iliyowekwa kwenye vipande vya matango machungu.

2. tia mafuta kwenye sufuria pasha moto mpaka yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu na tangawizi, korogakoroga, halafu tia nyama ya nguruwe na matango machungu, korogakoroga kwa dakika 5, tia maji, chumvi, M.S.G, mchuzi wa soya, sosi ya pilipili, sukari na pilipili manga, na punguza moto kidogo vichemke kwa dakika 20, halafu mimina maji ya wanga, tia vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.