Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-26 20:46:02    
Shirika la Fedha Duniani landaa mpango wa kufuta na kupunguza madeni ya nchi maskini

cri

Mkutano wa Kamati ya Fedha katika Shirika la Fedha Duniani uliofanyika katika tarehe 24 huko Washington umepitisha mpango wa kuzifutia nchi maskini kabisa madeni yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40, na bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Fedha Duniani itafanya mkutano kupitisha mpango huo.

Kati ya nchi 18 zitakazofaidika na msamaha huo, nyingi zaidi ni nchi za Afrika. Nchi hizo zitasamehewa madeni yanayodaiwa na Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40. Isipokuwa nchi hizo nchi nyingine 20 zitapunguziwa madeni kwa masharti. Kutokana na hayo, jumla ya thamani ya madeni yatakayosamehewa yatafikia dola za Kimarekani bilioni 55. Mwenyekiti wa Baraza la Fedha Duniani ambaye pia ni waziri wa fedha wa Uingereza Bw. Gordon Brown kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, kutokana na juhudi ngumu wawakilishi wa mazungumzo mwishowe wameafikiana kuhusu mpango huo.

Mpango huo umetokana na ahadi zilizotolewa na nchi za Marekani, Ujerumani, Japan, Uingereza, Canada, Ufaransa, Italia na Russia katika mkutano uliofanyika mwezi Julai mwaka huu huko Scotland. Kwenye mkutano huo kundi la nchi hizo nane lilipendekeza kufuta madeni ya nchi zilizo maskini kabisa duniani zinazodaiwa na Shirika la Fedha Duniani, Benki ya Maendeleo ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika. Ingawa Shirika la Fedha Duniani limekubali kufuta madeni ya nchi maskini kabisa duniani, lakini lazima lijadiliane na Benki ya Dunia, kwani mpango huo unapingwa na baadhi ya maofisa wa Benki hiyo na nchi kadhaa. Wapinzani wanaona kuwa msamaha huo wa madini mengi utaharibu uwezo wa kuchangisha fadha na uwezo wake wa kutoa mikopo. Kama wapinzani wakikataa, bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia haitaweza kuupitisha mpango huo wa kuondoa na kupunguza madini kwa kura nyingi za kutosha.

Ili kuwafanya wapinzani wauunge mkono mpango huo, mawaziri wa fedha wa kundi la nchi nane walimwandikia barua rais wa Benki ya Dunia Bw. Wolfowitz, wakisema kuwa kundi hilo la nchi nane litabeba hasara yote ya Benki ya Dunia itakayosababishwa na mpango huo, na kwenye barua walieleza kirefu namna ya kuchagisha fedha nyingi zaidi ili kuhakikisha shughuli za Benki ya Dunia zinakwenda kama kawaida.

Habari zinasema, bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia itafanya mkutano wa kupitisha na kutekeleza mpango huo. Wachambuzi wanaona kuwa ingawa mpango huo utazipunguzia mizigo baadhi ya nchi maskini, na mpango huo utasaidia lengo la maendeleo ya milenia lililotolewa na Umoja wa Mataifa, lakini huwezi kuondoa kabisa umaskini wa nchi hizo. Nchi tajiri zinapaswa ziendelee kutekeleza wajibu wa kusaidia nchi hizo katika elimu, maradhi na uchumi. Kadhalika, wanasema kuwa hivi sasa kuna nchi maskini zaidi ya 60 duniani ambazo kwa wastani pato la kila mwananchi halifikii dola za Kimarekani 500 kwa mwaka, nchi hizo pia zinastahili kufaidika na msamaha wa madeni.

Wakati nchi za Afrika zinapokaribisha mpango huo zinasema kuwa msamaha huo wa madeni lazima uhakikishwe unatekelezwa bila masharti yoyote ya kisiasa, vinginevyo utakuwa ni karatasi tupu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-26