Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-27 21:32:47    
Msimamizi wa tovuti kubwa kabisa ya kutafuta habari (search engine) kwa lugha ya Kichina duniani

cri

Siku moja ya mwezi Agosti mwaka huu, kijana mmoja mwenye umri wa miaka 37 wa China aligonga kengele ya kumaliza shughuli za soko la hisa la NASDAQ ya siku ile, ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza baada ya hisa za kampuni anayoingoza, inayojulikana kwa kampuni ya tekinolojia ya tovuti ya Baidu, China kuuzwa kwenye soko hilo. Katika siku hiyo bei ya hisa ya kampuni ya Baidu ilipanda kwa zaidi ya 350%, kampuni hiyo ilikusanya mitaji ya dola za kimarekani milioni 109, kiasi hicho ni kikubwa zaidi kuliko mitaji iliyokusanya sekta ya tovuti ya China kabla ya hapo. Katika kipindi hiki cha nchi yetu mbioni nitawafahamisha kuhusu ofisa mtendaji wa kwanza wa kampuni hiyo Bw. Li Yanhong.

Mwaka 1987 kijana Li yanhong alipokuwa na umri wa miaka 19 alijiunga na chuo kikuu cha Beijing, ambacho ni maarufu sana nchini China, akisomea elimu ya sekta ya mawasiliano ya habari. Mwaka 1991, Li Yanhong alikwenda kusoma nchini Marekani. Jambo lililowatatanisha watu ni kuwa baada ya kufaulu mtihani wa kusomea udakatari na karibu kumaliza tasnifu ya kumaliza masomo yake, Bw. Li Yanhong aliamua kuacha kuendelea na masomo ya shahada ya udakatari. Alipoeleza kwanini aliamua hivyo Bw. Li Yanhong alisema kuwa baada ya kupita miaka mingi ya masomo, aligundua kuwa kitu anachopenda siyo kufanya utafiti wa taaluma ya elimu bali ni kushughulikia mambo halisi. Alisema,

"Nilipomaliza masomo kwa miaka miwili na nusu, niliamua kujishughulisha mapema iwezekanavyo na mambo halisi, niliona kuwa kitu kilichonivutia zaidi siyo kusoma kwa undani kuhusu elimu kubwa ya utafiti bali ni kueneza shughuli za tekinolojia ambazo zinaathiri zaidi maisha ya watu wengi."

Watu wengi wanaona kuwa kama Bw. Li Yanhong asingechukua uamuzi huo leo kusingekuwa na tovuti ya Baidu. Kwani tokea wakati ule Bw. Li Yanhong alianza kushughulikia sekta ya tovuti ya kutafuta habari kwa nguvu zake zote. Katika muda wa miaka zaidi ya mitatu baada ya kuondoka chuo kikuu, Bw. Li Yanhong alijishughulisha na kazi za uendelezaji wa mfumo wa ukusanyaji wa habari kuhusu mambo ya fedha katika kampuni ya Dow Jones, ambapo Bw. Li Yanhong alisanifu mfumo wa kukusanya habari za mambo ya fedha kwa ajili ya ukurasa wa tovuti ya jarida maarufu la "Wall street Journal" ambao unatumika sana hadi hivi sasa na tovuti za kampuni kubwa za Wall street. Aidha, mafanikio aliyopata katika utafiti wake kuhusu uhusiano kati ya ubora wa tovuti na kiwango cha utafutaji yaliorodheshwa kuwa hataza yake nchini Marekani. Kwa kutumia tekinolojia hiyo ya kiwango cha juu, Bw. Li Yanhong alijiunga na kampuni maalumu ya tovuti za kutafuta habari inayojulikana sana duniani kwa INFOSEEK.

Toka kampuni ya Dow Jones hadi kampuni ya INFOSEEK, uzoefu wa kazi wa Bw. Li Yanhong ulimfanya apata ajira tulivu na yenye mshahara mkubwa. Lakini tabia ya Bw. Li yanhong ilifanya asikubali maisha yasiyo na mabadiliko. Mwezi Januari mwaka 2000 yeye na rafiki yake mkubwa walirejea nchini China na kuanzisha kampuni ya Baidu ya leo kwa mitaji ya dola za kimarekani milioni 1.2 waliyopata kwa mkopo wa benki. Bw. Li Yanhong alisema kuwa, uzoefu wa kazi zake nchini Marekani ulimfahamisha kuwa kufanya kazi za teknolojia peke yake ni vigumu kutimiza lengo lake la "kubadilisha maisha ya watu wa kawaida kwa tekinolojia" kwani kueneza tekinolojia kunategemea utendaji wa kibiashara wa kampuni, hivyo Bw. Li Yanhong alifikiria kuanzisha kampuni yake mwenyewe.

"Kutokana na uzoefu wa kazi nilizofanya kwa miaka 6 nchini Marekani, nilifahamu hatua kwa hatua kuwa ni vigumu kutimiza lengo la kubadilisha dunia kwa kutumia tekinolojia peke yake, wakati mwingi matumizi ya tekinolojia yanadhibitiwa na masoko na sera za biashara, kazi nilizofanya katika kampuni zile za Marekani zilifanya nipoteze nafasi za biashara, hivyo niliamua kuanzisha shughuli zangu mwenyewe."

Sababu nyingine iliyomshawishi Bw. Li Yanhong kurejea nchini na kuanzisha shughuli zake ni kuona soko kubwa la mtandao nchini China. Wakati zaidi ya 70% ya watu kutumia mtandao nchini Marekani, kiwango cha matumizi ya mtandao nchini China kilikuwa 8% tu, hivyo soko la China lina uwezo mkubwa ambao bado haujatumika. Mbali na hayo, akiwa mchina Bw. Li Yanhong anafahamu zaidi kanuni za uandishi wa sentensi za lugha ya Kichina kuliko wahandisi wa Marekani, jambo ambalo ni muhimu sana kwa usahihi wa utafutaji kwa lugha ya Kichina. Bw. Li Yanhong alisema kuwa mambo hayo yaliimarisha nia yake ya kuanzisha kampuni ya Baidu.

Machoni pa wafanyakazi wa Baidu, Bw. Li Yanhong ni mtu mpole na makini. Meneja wa tekinolojia wa kampuni hiyo bibi Wang Mengqiu alisema,

"Anapojaribu kukushawishi, mara kwa mara anakueleza sababu zake, na wala sio kukuamuru kwa haraka ufanye mambo unayopaswa kuyafanya. Wakati wanapojadiliana, kama wanayosema ni sahihi, yeye anakubali kubadilisha uamuzi wake bila shida."

Bosi huyo "mpole" machoni pa wafanayakazi wa kampuni ya Baidu, wakati mwingine alishikilia maoni yake bila kujali chochote, hususan katika wakati muhimu kuhusu mageuzi makubwa ya kampuni.

Mwanzoni baada ya kuanzishwa kampuni ya Baidu Bw. Li Yanhong alichagua njia ya kufanya ushirikiano na tovuti nyingine za sekta hiyo. Uchunguzi unaonesha kuwa hivi sasa tekinolojia ya utafutaji ya zaidi ya 80% ya tovuti zenye uwezo wa utafutaji kwa lugha ya Kichina inatokana na uungaji mkono wa tekinolojia ya kampuni ya Baidu. Watu wengi wanaona kuwa hiyo ni njia ya maendeleo yenye pato zuri. Lakini mwaka 2001 Bw. Li Yanhong alifanya uamuzi wa kufanya shughuli za utafutaji kampuni Baidu peke yake. Uamuzi huo ulileta maoni tofauti. Bw. Guo Dan ambaye alijiunga na kampuni ya Baidu muda si mrefu baada ya kuanzishwa kwa kampuni ya Baidu na hivi sasa yeye ni msimamizi wa tekinolojia ya kampuni, alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa wakati ule karibu hakukuwa na mfanyakazi hata mmoja aliyeunga mkono maoni ya Bw. Li Yanhong. Bw. Guo alisema, "Kampuni ya Baidu ilifanya kazi za kutafuta habari na kutoa huduma kwa tovuti nyingine, lakini kampuni hiyo haionekani mbele ya watu. Kampuni ya Baidu ilifuata mtindo huo wa mazoea. Hivyo shinikizo kubwa lililomkabili Bw. Li Yanhong ni kuwa watu wote wakiwemo wakurugenzi hawakufahamu kuwa mtindo wa namna hiyo haufai tena kutokana na maendeleo ya Internet.

Mwandishi wetu wa habari alifahamishwa kuwa Bw. Li Yanhong hakukuwa na upole tena, alishikilia kwa uthabiti maoni yake. Anaona kuwa kuendelea kutoa uungaji mkono wa tekinolojia ya utafutaji kwa tovuti nyingine hakutaweza kuleta maendeleo zaidi kwa shughuli za kampuni ya Baidu.

Sasa tunaona kuwa uamuzi wake umeimarisha uhai wa Baidu, baada ya jitihada za miaka minne, hivi sasa Baidu imekuwa bohari ya kwanza kwa ukubwa duniani kuhusu data za kichina na inashughulikia maombi zaidi ya watu milioni 100 kutoka nchi zaidi ya 100 kila siku.

Idhaa ya Kiswahili 2005-09-27