Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-28 16:33:29    
Ujerumani Waelekea Kuunda Serikali ya Mseto

cri

Chansela wa Ujerumani Bwana Gerhard Schoroder wa Ujerumani tarehe 27 katika mji wa Ufaransa, Strassburg, alisema kuwa Ujerumani utaunda serikali ya mseto. Dalili zote zimeonesha kuwa serikali hiyo ya mseto imekuwa ikikaribia Ujerumani.

Chansela Schoroder alipokuwa kwenye shughuli za "Baraza la Ulaya" alisema kuwa serikali ya mseto ya Ujerumani inapaswa iwe serikali ya mageuzi yenye utulivu, heshima na inayoweza kuridhisha matarajio ya wachaguzi walio wengi. Bw. Schoroder pia alisema, kazi ya kuunda serikali ya mseto pengine haiwezi kukamilika haraka. Alisema, "ingawa kazi hiyo haitatumia miezi kadhaa lakini inahitaji muda."

Wachambuzi wanaona kuwa maneno aliyosema Bw. Schoroder yanatokana na masharti aliyotoa mwenyekiti wa Chama cha Muungano Mama Angela Merkel tarehe 26 kuhusu kufanya mazungumzo na Chama cha Demokrasia ya Jamii kuunda serikali ya mseto. Mama Merkel alisema uaminifu wa pande mbili na mawazo ya namna moja kuhusu mageuzi ni masharti ya kuunda serikali ya vyama viwili. Alisisitiza kuwa Chama cha Demokrasia ya Jamii lazima kiwe tayari kimawazo kuwa serikali ya awamu ifuatayo lazima iwe ya mageuzi. Tarehe 27 Bw. Schoroder kwenye hotuba yake, licha ya kuonesha nia yake ya kukubali kuunda serikali ya mseto pia alionekana kuwa na mawazo sawa na Mama Merkel kuhusu serikali ya mageuzi.

Katika siku hiyo licha ya Schoroder, baadhi ya maofisa waandamizi wa vyama hivyo viwili pia walionesha kuunga mkono kuunda serikali ya mseto. Walisema, kuunda serikali ya mseto ni chaguo pekee linalofaa. Katika upande wa Chama cha Demokrasia ya Jamii, meya wa mji wa Bremen Bw. Henning Scherf alipohojiwa na waandishi wa habari alisema, Chama cha Demokrasia ya Jamii na Chama cha Muungano, vyama hivi viwili vinapaswa kufanya mazungumzo wazi. Alisema, kuunda serikali ya mseto ni njia pekee ya kutatua suala la kuunda serikali mpya baada ya uchaguzi mkuu. Katika upande wa Chama cha Muungano, mwenyekiti wa chama cha CSU Bw. Edmund Stoiber alipohojiwa na waandishi wa habari alisema anatumai vyama hivyo viwili vitafanya uamuzi haraka wa kuunda serikali ya mseto, "kwa sababu tokea Schoroder atangaze kufanyika uchaguzi kabla ya wakati uliowekwa, Ujerumani imekosa uongozi wa serikali kwa miezi minne."

Vyama vya demokrasia ya jamii na muungano vimeamua kufanya mazungumzo kwa mara ya pili tarehe 28 kuhusu uwezekano wa kuunda serikali ya mseto. Vyombo vya habari vimegundua kuwa katika siku za kaaribuni hakukuwa na hali ya vyama hivyo viwili kutupiana lawama na shutuma kama ilivyokuwa kabla ya tarehe 22 mazungumzo yalipofanyika kwa mara ya kwanza, bali vimeonesha nia ya namna moja ya kutaka kushirikiana katika kuunda serikali, mazingira ya mazungumzo yatakayofanyika tarehe 28 yamekuwa mazuri. Hii inaonesha kuwa ili kukwamua hali ya kisiasa ilivyo sasa, vyama hivyo viwili vimetambua kuwa kuunda serikali ya muungano wa vyama hivi viwili vikubwa ni chaguo pekee.

Ni kama Bw. Schoroder alivyosema kuwa kazi ya kuunda serikali ya mseto haiwezi kukamilishwa haraka. Kutokana na tofauti kuhusu Chama cha Muungano kitakuwa chama kikubwa cha kwanza katika bunge la Ujerumani na kuwa na haki ya kuunda serikali, na masuala kuhusu mfumo wa huduma za jamii na nakisi ya bajeti. Kwa hiyo ingawa kuunda serikali ya mseto ni mwelekeo uliokubalika kwa pande mbili, lakini mazungumzo kuhusu kuunda serikali ya mseto hayatakuwa shwari.

Idhaa ya kiswahili 2005-09-28