Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-28 18:07:45    
Mapishi ya samaki kwa njia ya mtindo wa ki-sichuan

cri

Mahitaji

Samaki wa Li mmoja, nusu ya kitunguu, kiasi kidogo cha vipande vya figili, tangawizi, vitunguu saumu, vitunguu maji, pilipili hoho na wanga, sosi ya pilipili hoho kijiko 3/4, maji bakuli moja, mchuzi wa soya kijiko 1/2, sukari vijiko 2, siki vijiko 3, mvinyo vijiko 2, mafuta ya ufuta kijiko 1/2, unga wa pilipili manga kijiko 1/2, chumvi vijiko 2.

Njia

1. ondoa matumbo ya samaki na umwosha, mkaushe na kasha tia chumvi na unga wa pilipili manga, iweke kwenye sahani kwa dakika 10, halafu tia wanga kwenye samaki. Pasha moto tia mafuta ndani ya sufuria mpaka yawe nyuzi ya 60, tia samaki ndani ya sufuria, kaanga mpaka yawe wa rangi ya hudhurungi, kasha mpakue.

2. pasha moto tena, mimina mafuta kidogo, tia vipande vya kitunguu, vitunguu saumu, tangawizi, figili, korogakoroga, halafu tia saumu ya pilipili hoho, tia samaki, mimina mvinyo, mimina maji, tia mchuzi wa soya, sukari, siki, mafuta ya ufuta, pilipili manga, baada ya kuchemka punguza moto kidogo, endelea kuchemsha kwa dakika 5, halafu uipakue, tia vipande vya pilipili hoho na vitunguu maji. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.