Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-29 20:02:46    
Nguvu za ushindani za nchi mbalimbali machoni pa Baraza la Uchumi duniani

cri
    Baraza la uchumi duniani tarehe 28 lilitoa "taarifa kuhusu nguvu ya ushindani duniani kwa mwaka 2005---2006". Kwa mujibu wa taarifa hiyo Finland imedumisha hadhi ya kuwa na nguvu kubwa zaidi ya ushindani duniani kwa miaka mitatu mfululizo. Nchi zilizochukua nafasi za kutoka mbili hadi kumi ni Marekani, Sweden, Denmark, Taiwan ya China, Singapore, Iceland, Uswisi, Norway na Australia. China ilichukua nafasi ya 49 ikifuatiwa na India, Brazil na Russia.

    Taarifa inasema kuwa Finland imefikia kiwango cha juu katika usimamizi wa ngazi ya taifa wa uchumi na ubora wa miundo ya umma. Aidha sekta ya biashara ya binafsi inaonekana kuwa na mwelekeo wa kutumia teknolojia ya kisasa na kuunga mkono uvumbuzi wa utamaduni mpya. Hali ya jumla ya kiwango cha teknolojia ya Marekani imetia fora kabisa duniani, tena ina nguvu kubwa sana katika uvumbuzi wa utamaduni mpya, lakini kasoro yake ni kukosa uimara katika mazingira ya uchumi wa taifa, na inachukua nafasi ya 47 katika upande huo, hali ya namna hiyo inaonesha kuwa Jumuiya ya kimataifa ina wasiwasi mkubwa kuhusu uchumi wa taifa wa Marekani, hususan pengo linaloonekana katika mambo ya fedha ya umma.

    Mwaka huu nchi za Ulaya ya kaskazini zinaendelea kuonekana vizuri kuhusu nguvu za ushindani, ambazo Ireland imepanda kwa hatua nne na kufikia nafasi ya 26, Estonia ilichukua nafasi ya 20 kwa miaka miwili mfululizo na kuwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi ya ushindani miongoni mwa nchi 10 zilizojiunga na Umoja wa Ulaya mwaka jana. Lakini Ugiriki ilishuka hadi nafasi ya 46 kutoka nafasi ya 37 ya mwaka jana, hivyo nchi hiyo na Italia ambayo inachukua nafasi ya 47, zimekuwa nchi mbili zilizochukua nafasi ya nyuma kabisa miongoni mwa nchi 25 za Umoja wa Ulaya isipokuwa Poland. Poland bado inachukua nafasi ya 51 ingawa imejisogeza mbele kwa nafasi 9.

    Chile inachukua nafasi ya 23 mwaka huu ni kama ilivyokuwa hapo nyuma kuwa inazitangulia sana nchi nyingine za Latin Amerika kwa nafasi 31 mwaka huu kutoka nafasi 26 mwaka jana. Hali ya namna hii haionekani kwenye sehemu nyingine duniani. Katika sehemu ya mashariki ya kati na Afrika ya kaskazini, nchi ya umoja wa falme za kiarabu na Qatar zinachukua nafasi za 18 na 19. Ingawa nguvu za ushindani za nchi za Afrika za kusini mwa jangwa la Sahara siyo kubwa, lakini miongoni mwake kuna baadhi ya nchi zilizopata mafanikio zikiwemo Afrika ya Kusini ambayo ilichukua nafasi ya 42, Botswana nafasi ya 48, Mauritius 5 na Ghana 59, ambayo inatupiwa macho kutokana na kusogea mbele kwa nafasi 9.

    Nguvu za ushindani za Taiwan ya China na Singapore zinachukua nafasi za mbele barani Asia na kuizidi Japan inayochukua nafasi ya 12. China na India ambazo zinachukua nafasi ya 49 na ya 50. Mwaka huu zinakaribiana zaidi kuliko miaka ya nyuma. Mwaka huu China imeshuka kwa nafasi 3, wakati India imepanda kwa nafasi 5. Tathimini kuhusu mazingira ya uchumi wa China ilishuka kidogo kutokana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la uwekezaji wa vitega-uchumi baada ya uwekezaji kupunguzwa katika baadhi ya sekta nchini China, ambapo India imejisogeza mbele kutokana na kiwango cha juu cha teknolojia zake. Taarifa inaona kuwa katika miaka ya karibuni China na India zilikuwa na ongezeko la kasi, lakini zinakwamishwa na matatizo mengi ya kiutaratibu, endapo hayatatatuliwa vizuri kasi ya ongezeko la nguvu ya ushindani ya uchumi duniani itapungua zaidi.

    Mwanauchumi wa kwanza wa baraza la uchumi duniani ambaye ni mkurugenzi wa "mradi wa nguvu ya ushindani duniani" Bw. Augusto Lopez Carlos amesema kuwa, katika miaka ya karibuni baada ya kuondolewa kwa ugawaji wa raslimali usio mwafaka, ufanisi wa uchumi umeongezeka kwa kasi, lakini kuboreshwa kwa udhahiri kwa uwezo wa uzalishaji mali kunategemea kufungua mlango zaidi na kutegemea mwelekeo wa sera zake.

    Baraza uchumi duniani limetoa "taarifa kuhusu nguvu ya ushindani duniani" kwa miaka 26 mfululizo, na taarifa ya mwaka huu inahusu nchi na sehemu 117. Upangaji wa nafasi za nguvu za ushindani unatokana na takwimu zilizotangazwa na nchi na sehemu hizo, tathmini za baraza uchumi duniani kuhusu hali ya uchumi na maoni ya viongozi wa nchi na kampuni za nchi na sehemu mbalimbali.

Idhaa ya Kiswahili