Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-09-30 20:17:28    
Uzalishaji na uuzaji wa magari ya China uliendelea kuongezeka katika miezi 8 iliyopita ya mwaka huu

cri

Kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na shirikisho la viwanda vya magari la China, uzalishaji na uuzaji wa magari ya China uliendelea kuongezeka kwa utulivu katika miezi 8 iliyopita ya mwaka huu. Kati ya uzalishaji huo, uzalishaji na uuzaji wa magari ya usafiri umeongezeka kwa asilimia 10, ukiwa umezidi kwa kiasi kikubwa ongezeko la uzalishaji wa magari ya kazi.

Takwimu zinaonesha kuwa, toka mwezi Januari hadi mwezi Agosti, China imezalisha magari milioni 3.7 na kuuza magari milioni 3.64, ikiwa ni ongezeko la asilimia 8.23 na asilimia 10.61. Kati ya hayo, magari ya usafiri milioni 2.5 yamezalishwa na milioni 2.45 yameuzwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 10.24 na asilimia 15.09 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Magari ya kazi milioni 1.2 yamezalishwa na milioni 1.19 yameuzwa, likiwa ni ongezeko la asilimia 4.3 na asilimia 2.41 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Kwa magari ya usafiri, katika miezi 8 ya mwanzo ya mwaka huu, uzalishaji wa magari madogo (saloon car) umeongezeka kwa kiasi kikubwa zaidi kuliko aina nyingine za magari, na uzalishaji na uuzaji wa magari hayo umefikia milioni 1.74 na 1.68, zikiongezeka kwa asilimia 11.49 na asilimia 15.78 kuliko mwaka jana wakati kama huo. magari laki 1.06 ya matumizi mbalimbali MPV (Multi-Purpose Vehicle) yalizalishwa na kuuzwa kwa elfu 980, yakiongezeka kwa asilimia 32.27 na asilimia 34.66 kuliko mwaka jana wakati kama huo; magari laki 1.18 ya michezo SUV (Sports Utility Vehicle) kwa jumla yalizalishwa na kuuzwa kwa 119.8, yakiongezeka kwa asilimia 0.11 na asilimia 8.23 kuliko mwaka jana wakati kama huo, jumla ya magari laki 5.3 ya matumizi yote CUV yalizalishwa na kuuzwa laki 5.52, likiwa ni ongezeko la asilimia 5.24 na asilimia 11.72 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Katika mwezi Agosti, uzalishaji na uuzaji wa magari kwa jumla ulifikia magari laki 4.4 na laki 4.2, ikiwa ni ongezeko la asilimia 17.08 na asilimia 9.02 kuliko mwaka jana wakati kama huo. Kati ya magari hayo, magari ya usafiri laki 3.15 yalizalishwa na laki 2.92 yaliuzwa, yakiongezeka kwa asilimia 35.39 na asilimia 24.15 kuliko mwaka jana wakati kama huo; magari ya kazi laki 1.261 yalizalishwa na laki 1.263 yaliuzwa, yakipungua kwa asilimia 12.52 na asilimia 14.96 kuliko mwaka jana wakati kama huo.