Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-03 20:39:07    
Muziki wa Jadi wa Kichina na Rock'n'Roll Waungana nchini China

cri

Muziki wa Rock'n'Roll ulianza kutokea katika miaka ya 50 ya karne ya 20 vijijini nchini Marekani, wakati huo waimbaji wa vijijini magharibi mwa China walipokea sifa za muziki wa Afrika na kuupata muziki huo. Bendi ya Tangchao ya China iliingiza muziki wa jadi wa Kichina ndani ya muziki huo na kupata muziki wa Rock'n'Roll wa Kichina.

wasikilizaji wapendwa, mliosikia ni muziki uliopigwa na bendi hiyo "Kurejea tena katika Enzi ya Tang". Huu ni wimbo wa kwanza katika albamu ya bendi hiyo. Mwimbaji mkuu alitumia mahadhi ya opera ya Kibeijing akisaidiwa na gitaa, wimbo huo unavutia sana kwa mtindo na maneno.

Bendi ya Tangchao iliasisiwa mwaka 1988. Baada ya albamu ya kwanza kutolewa mwaka 1992 bendi hiyo inafuatiliwa zaidi na wapenda muziki na kuwa "dalili ya utamaduni mpya barani Asia".

wasikilizaji wapendwa, mliosikia ni wimbo mwingine uliopo katika albamu ya bendi hiyo "Njozi njema chini ya balamwezi". Sauti kama ya kunong'onezwa na maneno yanawagusa wasikilizaji. Maneno ya wimbo huo ni kama yafuatayo:

Siwezi kusahau ulipokuwa kwangu kwa raha na uchungu,

Siwezi kusahau tulipoagana kwa moyo wa upendo katika

mbalamwezi wa usiku,

Lakini hayo yote yamechukuliwa mbali na upepo,

Yaliyobaki sasa ni kumbukumbu tamu.

Bendi hiyo ilichanganya muziki wa Kichina na muziki wa Rock'n'Roll, wasikilizaji wanarudishwa kwenye zama za kale kwa muziki huo wa mchanganyiko huo.

katika albamu ya kwanza, nyimbo zote zinavutia kwa mitindo tofauti na maneno yenye maana ya kina, inaonesha kuwa bendi hiyo ina ufahamu mkubwa kuhusu maisha ya kila siku na utamaduni wa China.

Ikilinganishwa na albamu ya kwanza, albamu ya pili ina nyimbo nyingi ndefu ndefu. Wimbo katika albamu ya pili, "Hadithi za Madola Matatu ya Kifalme" umetungwa kwa maneno ya utangulizi wa riwaya ya "Madola Matatu ya Kifalem": "Maji ya Mto Changjiang yamimikia baharini, mawimbi yawachukua mashujaa wengi. Haki na uovu, ushindi na kushindwa yote yamekuwa bure. Milima ni ile ile, na jua hili hili."

wasikilizaji wapendwa, mliosikia ni sehemu ya wimbo wa "hadithi za Madola Matatu ya Kifalme".

Bendi ya Tangchao imeunganisha muziki wa jadi wa Kichina na muziki wa kisasa na kuufanya muziki wake uwe wa aina mpya kabisa.

Wasikilizaji wapendwa, mliosikia ni wimbo mwingine katika albamu ya pili, "Njozi". Wakati bendi hiyo ilipoanza kujulikana, watu wengi walisema muziki wao ni mwanzo mwingine wa utamaduni wa Asia. Lakini wanamuziki wa bendi hiyo walisema, kitu wanachotaka ni kuwafahamisha watu kuwa, tupo vijana tunaopenda muziki na kutaka kueleza hisia na matumaini yao kupitia nyimbo zao.

Wapenda muziki wa bendi hiyo wanasema, "kama ukipata msisimko na ukakamavu kutoka muziki wa bendi hiyo, na kama ukipata moyo wa kujiamini kutoka nyimbo za bendi hiyo, basi wanamuziki wamefanikisha lengo lao ambalo hapo kabla watu waliona kuwa ni wazungu walioweza kulifanikisha."

Pamoja na muziki huu wa "Sindikizo" kipindi chetu cha leo kimefikia tamati yake, tunawatakieni afya njema na kwaherini.