Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-04 19:23:35    
Hali ya usalama ndani ya Palestina yaleta wasiwasi kwa watu

cri

Kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina tarehe 3 iliitisha mkutano maalum huko Gaza na Ramallah kwa wakati mmoja, ikipitisha pendekezo la kutokuwa na imani na serikali inayoongozwa na Bw Ahmed Qureia, na kumtaka mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Abbas aunde serikali mpya ndani ya wiki mbili. Sababu ya kamati ya utungaji wa sheria kupitisha pendekezo la kutokuwa na imani na serikali ni kuwa, serikali ya Qureia haikufanya juhudi za kudhibiti hali ya mambo na kusababisha hali ya vurugu kwenye ukanda wa Gaza.

Sababu iliyosababisha moja kwa moja hali ya usalama ya Gaza izidi kuwa mbaya kwa ya dharura, ni mgogoro uliotokea tarehe 2 kati ya polisi wa Palestina na watu wenye silaha wa Hamas. Siku hiyo polisi wa Palestina walipokuwa kwenye doria mjini Gaza, walikabiliana na watu wenye silaha wa kikosi cha Qassam Brigade kilicho chini ya kundi la Hamas, ambapo pande hizo mbili zilikwaruzana na kupambana. Baadaye watu wa kikosi cha Qassam Brigade waliwatupia polisi wa Palestina mabomu ya mikono, ambapo polisi wawili walijeruhiwa. Pande hizo mbili zikawakusanya mara moja watu wa kila upande wao kuzisaidia na kusababisha mapambano ya kufyatuliana risasi. Baadaye watu wenye silaha wa Qassam Brigade walishambulia kituo cha polisi ndani ya kambi moja ya wakimbizi iliyoko kaskazini ya Gaza, ambapo naibu mkuu wa idara ya polisi ya kambi hiyo aliuawa, polisi wengi kadha wa kadha walijeruhiwa. Habari zilisema kuwa, mgogoro huo ulifanyika kwa saa 6, na kusababisha vifo vya watu watatu na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa, na wengi wao ni raia wa kawaida.

Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, uhusiano kati ya kikosi cha polisi cha Palestina na makundi mbalimbali ya kijeshi umekuwa na hali wasiwasi katika siku hizi, hii inahusiana moja kwa moja na hatua zilizotolewa hivi karibuni na mamlaka ya utawala wa Palestina kuhusu udhibiti wa usalama na kuimarisha udhibiti juu ya makundi yenye msimamo mkali. Utawala wa Palestina hivi karibuni umeamua kuwa, ili kufufua utaratibu wa kisheria kwenye ukanda wa Gaza, na kulinda utaratibu wa jamii wa kawaida, watu wenye silaha hawaruhusiwi kushika silaha hadharani. Ingawa makundi mbalimbali ya kijeshi yameahidi kuwa yatafuata agizo hilo la utawala, lakini kwa kweli yanakataa kufuata agizo, na kulaani mamlaka ya utawala wa Palestina kushika fursa kupiga pigo makundi mbalimbali ya kijeshi. Kutokana na migororo ya kijeshi na vurugu za kivita zilizodumu kwa miaka mingi pamoja na mashambulizi ya kijeshi ya Israel na hali ya vurugu ya usimamizi wa ndani, kikosi cha polisi cha Palestina kinakabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile zana na silaha duni, watu wasio na sifa bora, na nguvu dhaifu ya kufanya mapambano na kadhalika, kila kikikabiliana na uchokozi wa makundi mbalimbali ya kijeshi ya Palestina, kikosi cha polisi huwa kinashindwa kutekeleza kwa ufanisi jukumu lake la kulinda usalama na kuheshimu heshima ya mamlaka ya utawala wa Palestina.

Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Bw Mahmoud Abbas tarehe 3 alisema kuwa, kikosi cha usalama hakiwezi kukaa kimya juu ya uchokozi wa makundi ya kijeshi, na kitachukua hatua zote kadiri iwezekanavyo ili kutokomeza vitendo hivyo vya kimabavu. Msemaji wa wizara ya ndani ya Palestina siku hiyo alisema kuwa, kikosi cha usalama la Palestina kimedhamiria kufufua mfumo wa sheria na utaratibu wa jamii, hakiruhusu mtu yeyote kuwa juu ya sheria bila kujali mustakbali wa taifa.