Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-05 17:40:42    
Mapishi ya kichwa cha samaki na doufu kwenye maziga

cri

Mahitaji

Kichwa cha samaki, doufu gramu 200, uyoga mweusi gramu 25, mvinyo wa kupikia gramu 25, mchuzi wa soya gramu 75, sosi ya pilipili gramu 25, sukari gramu 10, vipande vya vitunguu saumu gramu 25, tangawizi gramu 20.

Njia

1. osha kichwa cha samaki na ukikate vipande viwili, tia sosi ya pilipili na mchuzi wa soya. Kata doufu iwe vipande vipande, na uvitie kwenye maji ya moto kwa dakika 2 kisha uvipakue.

2. pasha moto tia mafuta kwenye sufuria mpaka yawe nyuzi ya 80, tia kichwa cha samaki kwenye sufuria, ikaange mpaka iwe rangi ya hudhurungi, tia mchuzi wa soya, sukari na mvinyo, na uipindue na endelea kukaanga upande mwingine, mimina maji gramu 750, tia vipande vya doufu, uyoga mweusi, tangawizi. Baada ya kuchemka uviweke vitu hivyo kwenye maziga, na pungua moto kidogo endelea kuchemsha kwa dakika 15, tia vipande vya vitunguu saumu na mimina mafuta ya ufuta. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.