Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-06 19:24:48    
Bunge la Iraq lafuta vifungu vya marekebisho vya katiba kuhusu upigaji kura wa maoni ya raia wote

cri

Bunge la mpito la Iraq tarehe 5 lilipiga kura na kufuta vifungu vya marekebisho ya katiba kuhusu upigaji kura wa maoni ya raia wote, na kudumisha ufafanuzi uliopo juu ya "wapiga kura" kwenye upigaji kura wa maoni ya raia. Wachambuzi wamedhihirisha kuwa, hii imeonesha kuwa migongano kati ya madhehebu ya Shia, ya Suni na kundi la wakurd nchini Iraq inazidi kuwa mikali siku hadi siku.

Bunge la Iraq siku hiyo limefufua ufafanuzi uliopo kuhusu "wapiga kura" katika upigaji kura wa raia wote. Kutokana na hayo, kwenye mchakato wa upigaji kura wa maoni ya raia wote, "wapiga kura" ndio wapiga kura wanaoshiriki kwenye upigaji kura, siyo wapiga kura walioandikishwa tu. Naibu spika wa bunge la mpito ambaye pia ni kiongozi wa madhehebu ya Shia Bwana Husaain al Shahristani alisema kuwa, upigaji kura wa maoni ya raia wote utakaofanyika tarehe 15 utafanyika kutokana na ufafanuzi huo, serikali ya mpito ya Iraq itauarifu Umoja wa Mataifa kuhusu hali hiyo.

Mwanzoni katiba ya muda ya Iraq ilieleza kuwa, katika upigaji kura kama theluthi mbili ya wapiga kura wa mikoa mitatu yoyote kati ya mikoa 18 watapiga kura za hapana, basi katiba haitaweza kupitishwa. Bunge la mpito la Iraq tarehe 2 kwa ghafla lilitoa ufafanuzi mpya juu ya kanuni iliyotajwa hapo kabla, likithibitisha "wapiga kura" ni "wapiga kura walioandikishwa", yaani kama theluthi mbili ya "wapiga kura walioandikishwa" wa mikoa mitatu watapiga kura za hapana ndipo katiba haitaweza kupitishwa, hii itaongeza taabu kubwa ya kupatikana kwa theluthi mbili ya kura za hapana. Madhehebu ya Suni yamepinga vikali ufafanuzi huo yakidai kuwa yatasusia upigaji kura wa maoni ya raia utakaofanyika tarehe 15.

Baada ya bunge la mpito kufuta vifungu vya marekebisho ya katiba kuhusu upigaji kura wa maoni ya raia, makundi ya kisiasa ya madhehebu ya Suni yameeleza kukaribisha hatua hiyo. Msemaji wa kamati ya mazungumzo ya taifa ya madhehebu ya Suni Bwana Saleh al Mutlaq alisema kuwa, madhehebu hayo hayatawataka waarabu wa madhehebu ya Suni wasusie upigaji kura wa maoni ya raia wote.

Wachambuzi wanaona kuwa, kutokana na marekebisho yaliyotolewa tarehe 2 kwenye bunge la mpito, kama mswada wa katiba wa Iraq utaweza kupitishwa katika upigaji kura wa maoni ya raia wote utakaofanyika tarehe 15, uaminifu wa katiba mpya pia utapungua kwa kiasi kikubwa. Na madhehebu ya Suni huenda yataweza kususia uchaguzi mkuu wa bunge utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu, na kuleta taabu kubwa kwa ukarabati wa demokrasia na usalama wa Iraq. Kabla ya kufanyika upigaji kura wa maoni ya raia wote, bunge la mpito la Iraq limefuta vifungu vya marekebisho ya katiba kuhusu upigaji kura huo, hii imeyawezesha madhehebu ya Suni yaendelee kujiunga na mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq, na itasaidia mchakato wa ukarabati wa kisiasa na usalama wa Iraq.

Lakini mabadiliko ya misimamo ya bunge la mpito la Iraq kuhusu kanuni ya katiba juu ya upigaji kura wa maoni ya raia wote yameonesha pia kuwa, migongano kati ya madhehebu ya Shia , ya Suni na kundi la wakurd inazidi kuwa mikali siku hadi siku, ambayo imeletea hali isiyojulikana kama mswada wa katiba utapitishwa tarehe 15 Oktoba au la. Wachambuzi wanaona kuwa, upigaji kura wa maoni ya raia wote utakaofanyika tarehe 15 Oktoba utaonesha wazi zaidi mustakabali wa mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa Iraq, watu watafuatilia zaidi kama Iraq itapiga hatua ya kuelekea kwenye nchi yenye demokrasia au kuelekea kwenye janga la vurugu na ufarakanishaji.