Katibu mkuu wa Jumuiya ya NATO Bwana Jaap de Hoop Scheffer na ujumbe unaoundwa na wajumbe wa nchi wanachama 26 za NATO walifanya ziara nchini Afghanistan kuanzia tarehe 4 hadi 6. Bwana Jaap de Hoop tarehe 6 alitangaza huko Kabul kuwa, jeshi la utoaji misaada ya usalama la kimataifa linaloongozwa na NATO litapanua eneo lake la kulinda amani na kuongeza askari wake nchini Afghanistan.
Bwana Jaap de Hoop aliyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa naye pamoja na rais Hamid Karzai wa Afghanistan baada ya kumaliza mazungumzo kati yao. Bwana Jaap alisema kuwa, Jumuiya ya NATO itapanua shughuli zake za kulinda amani nchini Afghanistan hadi sehemu za mashariki na kusini za nchi hiyo, na kuongeza askari wake kuwa elfu 13 au 14 nchini humo. Rais Karzai alisema kuwa Afghanistan inatumai kujenga ushirikiano wa kimkakati wa muda mrefu na NATO, kuongezeka na kupungua kwa idadi ya askari wa jeshi la NATO kunatokana na maendeleo ya hali ya usalama ya nchini Afghanistan.
Habari zinasema kuwa, lengo kuu la ziara hiyo ya Bwana Jaap de Hoop na ujumbe wa NATO, ni kufanya maandalizi ya kupanua shughuli za NATO kulinda amani nchini Afghanistan.
Kwa Jumuiya ya NATO, vitendo vya kulinda amani nchini Afghanistan vya jeshi la utoaji misaada ya usalama la kimataifa linaloongozwa na NATO vimechukuliwa kuwa alama muhimu ya NATO katika kutimiza mageuzi ya mikakati. Baada ya kukomeshwa kwa vita baridi, NATO iliwahi kupoteza wapinzani. Baada ya kutokea kwa tukio la tarehe 11 Septemba nchini Marekani, NATO imeuchukulia ugaidi kuwa ni tishio kubwa, ikaanza kutekeleza mikakati yake ya dunia nzima, na kushiriki kwenye vitendo vya kulinda amani nje ya Ulaya. Hivyo NATO siku zote inatilia maanani vitendo vyake vya kulinda amani nchini Afghanistan, na kusisitiza mara kwa mara kuwa vitendo hivyo ni muhimu zaidi katika vitendo vyake vikubwa.
Kwa serikali ya Afghanistan, ingawa ukarabati wa kisiasa wa Afghanistan umeingia njia ya kawaida hatua kwa hatua, na uchaguzi wa rais na bunge umefanyika kwa nyakati tofauti, lakini hali ya usalama ya Afghanistan bado si tulivu, serikali ya Afghanistan bado inaihitaji jumuiya ya kimataifa itoe misaada mikubwa kwake kuhusu hali ya usalama wake.
Wachambuzi wanaona kuwa, Jumuiya ya NATO imeamua kuongeza askari wake nchini Afghanistan na kupanua vitendo vyake vya kulinda amani nchini humo, hii inalingana na mahitaji ya pamoja ya NATO na Afghanistan, hayo ni matumaini ya pamoja ya pande hizo mbili. Lakini wachambuzi wameainisha pia kuwa, NATO ikitaka kutimiza kikweli upanuzi wake wa vitendo vya kulinda amani hadi sehemu ya kusini ya Afghanistan bado inakabiliwa na matatizo makubwa mawili.
Kwanza inahitaji kupata watu wengi na zana nyingi, hili ni tatizo la kwanza linalohitaji kutatuliwa na Bwana Jaap de Hoop.
Aidha, namna ya kushughulikia ipasavyo uhusiano na jeshi la shirikisho linaloongozwa na Marekani nchini Afghanistan pia inastahili kuzingatiwa. Jeshi hilo linaloongozwa na Marekani lina watu karibu elfu 20, kama jeshi la NATO litapanua shughuli zake hadi kwenye sehemu za kusini na mashariki ya Afghanistan, namna ya kusawazisha vitendo vya majeshi hayo mawili ni tatizo linalohitaji kutatuliwa kwa dharura.
|