Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-10 20:07:51    
Akufaaye wakati wa dhiki ndio rafiki wa kweli

cri

Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika Asia ya kusini limesababisha Pakistan na India hasara kubwa za mali na vifo vya watu wengi nchini India na Pakistan, tetemeko hilo linafuatiliwa sana na jumuyia ya kimataifa. Hadi tarehe 10 watu karibu elfu 20 wamekufa katika tetemeko hilo wamekuwa karibu elfu 20, na idadi hiyo sio ya mwisho. Mbele ya maafa hayo yaliyotokea ghafla, nchi zilizoathirika za Pakistan na India zimeonesha moyo mtukufu wa ubinadamu, mshikamano katika dhiki na ushirikiano katika uokoaji. Tetemeko hilo limesababisha maafa makubwa kwa nchi zote hizo mbili, lakini maafa hayo yamezisogeza nchi hizo karibu.

Pakistan imeathirika vibaya zaidi katika tetemeko hilo. Muda mfupi baada ya kutokea kwa tetemeko, jioni ya tarehe 8 waziri mkuu Singh wa India alimpigia simu rais Musharraf wa Pakistan na kutoa mkono wa pole kutokana na watu wengi wa Pakistan kufa na kujeruhiwa Pakistan na kusema kwamba India iko tayari kuisaidia Pakistan wakati wote. Huu ni wema mkubwa wa India kwa Pakistan. Kutokana na kuwa tetemeko hilo lilitokea katika sehemu ya Kashmir inayogombaniwa na pande mbili mara nyingi kwa vita, urafiki huo uliooneshwa na Singh hakika utasaidia utulivu wa sehemu hiyo. Bw. Musharraf alitoa shukrani na kumwambia kwamba atamwambia anapohitaji msaada. Katika sehemu ya Kashmir ambapo yalitokea maafa makubwa zaidi, vikosi vya pande mbili vilivyosimamia sehemu ya kutenganisha pande mbili vilifanya "mkutano wa bendera" na kuamua pande mbili zisaidiane.

Sababu ya nchi mbili kuweza kushirikiana baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi ni uhusiano uliokuwa ukiboreshwa katika miaka ya karibuni. India na Pakistan ni nchi mbili muhimu katika Asia ya kusini, lakini kihistoria nchi hizo hizo zina uhasama na kusababisha msukosuko wa kikanda. Migogoro ya kijeshi haikutulia katika miongo kadhaa katika sehemu ya Kashmir. Baada ya karne ya 21 kuanza, viongozi wa pande mbili walifanya mazungumzo mara nyingi, uhusiano wa pande mbili umeanza kuwa mzuri. Kuanzia mwezi Februari mwaka 2004, nchi mbili zilifanya madhru mengi ya mazungumzo ya amani. Mwezi Septemba mwaka huu kwa kutumia fursa ya kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa, viongozi wa nchi hizo mbili walikutana huko New York. Mwanzoni mwa mwezi huu mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili walikutana na kuonesha kuwa watasukuma mazungumzo ya pande mbili na kujitahidi kutatua tatizo la Kashmir.

Jambo linalostahili kutajwa ni kwamba mshikamano wa India na Pakistan katika uokoaji wa maafa umezidisha imani ya pande mbili, na utasukuma mbele mchakato wa amani. Vyombo vya habari vinaona kuwa mbele ya maafa makubwa ya kimaumbile, sehemu iliyotenganisha pande mbili katika Kashmir imekuwa daraja la kuunganisha nchi mbili, ingawa tetemeko hilo la ardhi ambalo halikuwahi kutokea kwa karibu karne moja iliyopita limewaletea hasara kubwa, lakini tetemeko hilo pia limewaunganisha zaidi watu wa Asia ya kusini na hasa watu wa nchi hizo mbili katika kukabiliana kwa pamoja na chamgamoto ya maafa ya kimaumbile.

"Rafiki akufaaye wakati wa dhiki ndio rafiki wa kweli", mshikamano wa pande mbili katika mapambano dhidi ya maafa ya kimaumbile unamaanisha pande hizo zinaelekea kwenye amani na ushirikiano. Kutokana na kuwa uhusiano wa India na Pakistan ni muhimu kwa utulivu wa sehemu ya Asia ya kusini, mshikamano huo wa pande mbili ni habari njema kwa sehemu hiyo na hata kwa dunia.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-10