Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-11 17:51:45    
Wafanyabiashara wa China watafuta nafasi ya biashara Korea ya Kusini

cri

Mkutano wa nane wa wafanyabiashara wa China na wenye asili ya China duniani ulifunguliwa tarehe 10 huko Seoul, mji mkuu wa Korea ya Kusini. Mkutano huo ambao utafanyika kwa siku 3, unahudhuriwa na wawakilishi zaidi ya 3,000 kutoka nchi na sehemu 28 duniani. Kauli-mbiu ya mkutano huo ni "Kukua pamoja na wafanyabiashara wa China na kustawi pamoja na dunia" utakuwa uwanja mpya wa maingiliano kwa wafanyabiashara wa China na wenye asili ya China duniani na pia ni kutoa nafasi ya kufanya ushirikiano kati yao na wafanyabiashara wa Korea ya Kusini.

Katika kipindi cha mkutano huo, washiriki watakuwa na majadiliano kuhusu hali na maendeleo ya teknolojia za mawasiliano ya habari, viumbe na mawasiliano ya habari kuhusu utamaduni. Mbali na hayo, utafayika mkutano wa maelezo kuhusu uwekezaji wa wafanyabiashara wa China, mkutano wa maelezo kuhusu mazingira ya uwekezaji ya Korea ya Kusini pamoja na mkutano wa wakuu watendaji wa wafanyabiashara wa Korea ya Kusini na wa China.

Asubuhi ya tarehe 10, mwandishi wetu wa habari aliona washiriki wa mkutano walifika mapema walikuwa wakipanga mstari kusubiri kufungua mlango wa ukumbi wa mkutano, huku wakibadilishana kadi za majina na kuelezana hali zao. Wakati walipoulizwa na mwandishi wa habari kuhusu lengo la safari zao, wengi walisema kuwa ni kwa ajili kupata marafiki wapya na kutafuta nafasi za biashara. Mshiriki mmoja kutoka China alisema,

  

"Jina langu ni Wen Xueli, nimekuja kwa kuwakilisha jumuiya ya sekta ya vipuri vya elektroniki ya China. Lengo letu muhimu ni kuimarisha ushirikiano wa sekta ya mawasiliano ya habari (IT) wa nchi mbili za China na Korea ya Kusini. Nchi hizo mbili zikiimarisha ushirikiano zinaweza kupata maendeleo ya kunufaishana."

Mshiriki mmoja kutoka mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong alisema,

"Ninatoka Hong Kong. Ninataka kufahamiana na baadhi ya watu na kuwa marafiki."

Mratibu wa jumuiya ya wafanyabiashara wa China nchini Australia Bw. Shi Guohua alisema,

"Ninatoka Australia. Nia yangu ni kuonana na wafanyabiashara wa hapa na kuangalia nafasi ya kufanya ushirikiano."

Mkutano huo uliandaliwa na jumuiya ya wafanyabiashara wa

China nchini Korea ya Kusini, wizara ya fedha na uchumi, wizara ya mambo ya nje na biashara, wizara ya sheria na utawala, wizara ya utamaduni na utalii, wizara ya uzalishaji mali na mali asili, wizara ya ujenzi na mawasiliano pamoja na baadhi ya serikali za mitaa za huko.

  

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo, ambaye ni kiongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara wenye asili ya China nchini Korea ya Kusini Bw. Yuan Guodong alipotoa hotuba kwenye ufunguzi wa mkutano huo alisema kuwa, tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Korea ya Kusini, China imekuwa nchi ya kwanza kwa ukubwa katika shughuli za uwekezaji nchini Korea ya Kusini na usafirishaji bidhaa. Lakini, wafanyabiashara wa China hawafahamu mazingira ya uwekezaji nchini Korea ya Kusini, hivyo kuna nafasi kubwa sana ya kujiendeleza katika nchi hiyo.

Mwenyekiti wa umoja wa wanaviwanda na wafanyabiashara wa China ambaye alifika huko kwa ajili ya kushiriki mkutano huo Bw. Huang Mengfu alipotoa hotuba kwenye sherehe ya ufunguzi alisema kuwa, China ni moja ya nchi za ukoo wa uchumi duniani, maendeleo ya uchumi ya China yamepata uungaji mkono wa nchi mbalimbali duniani, China nayo imetoa soko kubwa na nafasi ya uwekezaji kwa nchi mbalimbali duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-11