Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-11 21:03:57    
Vyakula vya China

cri

Vitoweo vya China vimegawanyika katika aina nane kutokana na umaalumu wa mapishi yake, zikiwa ni pamoja na Shandong, Sichuan, Guangdong, Fujian, Jiangsu, Zhejiang, Hunan na Anhui.

Kukamilika kwa aina moja ya vitoweo kunahitaji miaka mingi na umaalumu wa mapishi yake, vilevile kunaathiriwa na hali za kijiografia, hewa, rasilimali na mazoea ya chakula. Kulikuwa na mtu aliyefananisha mapishi ya vitoweo ya Jiangsu na Zhejiang kama warembo wembamba wa sehemu ya kusini ya China; Vitoweo vya mikoa ya Shandong na Anhui kama watu makamo wenye nguvu wa sehemu ya kaskazini; vitoweo vya mikoa ya Guangdong na Fujian kama vijana watanashati; Na vitoweo vya mikoa ya Sichuan na Hunan kama wasomi wenye ujuzi na elimu nyingi.

VITOWEO VYA AINA NANE VYA CHINA

Vitoweo vya Shandong

Vitoweo vya mkoa wa Shandong ni pamoja na vya sehemu mbili za kusini mwa mji wa Jinan na mashariki ya Shandong. Umaalumu wake ni kuwa na chumvi na mafuta mengi, vikichanganywa na vitunguu na vitunguu saumu. Vitoweo vizuri vya aina hiyo ni pamoja na vyakula vya baharini, supu na maini na utumbo wa wanyama.

Vitoweo vya Sichuan

Vitoweo vya Sichuan ni pamoja na vya miji miwili ya Chenngdu na Chongqing. Umaalumu wake ni vyenye ladha, chumvi na pili nyingi. Vitoweo vinavyopendwa sana na watu ni pamoja na vipande vidogo vya nyama ya kuku vinavyokaangwa pamoja na karanga na pilipili, viganja vya dubu, vipande vya nyama ya nguruwe pamoja na pilipili, mapezi ya papa na kaa wa baharini;

Vitoweo vya Jiangsu

Vitoweo vya Jiangsu ni vya miji ya Yangzhou, Suzhou na Nanjing.

Umaalumu wa vitoweo hivyo ni kuzingatia kutumia viungo na kuhifadhi mchuzi wake wa asili. Mbinu zinazotumika katika mapishi ni kuchemsha.

Vitoweo vyake maarufu ni vipande vidogo vidogo vya nyama na mboga vilivyopikwa kwa kutumia supu ya kuku, na makongoro ya nguruwe yaliyochanganywa na unga wa nyama ya kaa wa baharini.

Vitoweo vya Zhejiang

Vitoweo vya Zhejiang ni pamoja na miji ya Huangzhou, Ningbo na Shaoxing, ambavyo vya Hangzhou vinajulikana zaidi.

Umaalumu wa vyakula hivyo ni laini, vyenye ladha nzuri na kutokuwa na mafuta mengi.

Vitoweo maarufu ni kamba wadogo wa baharini wenye harufu ya chai, kuku pamoja na samaki wenye ladha ya siki.

Vitoweo vya Guangdong

Vitoweo vya Guangdong ni pamoja na vya miji Guangzhou, Chaozhou, na Dongjiang, ambavyo vya Guangzhou ni vyenye sifa kubwa zaidi.

Umaalumu wa vitoweo hivyo ni vyenye ladha nzuri na kutumia chumvi kidogo sana.

Vitoweo maarufu ni pamoja na nyama za aina tatu za nyoka, paka na kuku, nguruwe mchanga mzima, aina ya tikiti maji nyeupe, na nyama ya Gulao.

Vitoweo vya Hunan

Vitoweo vya Hunan vinazingatia ladha nzito za pilipili na siki. Na vitoweo maarufu ni pamoja na mbegu za yungiyungi tamu na mapezi ya papa

Vitoweo vya Fujian

Vitoweo vya Fujian ni vya miji ya Fuzhou, Quanzhou na Xiamen, ambavyo vya mji wa Fuzhou ni maarufu zaidi.

Umaalumu wa wake ni kutumia vyakula vya bahairni, na kuzingatia ladha tamu, siki na chumvi.

Vitoweo maarufu ni pamoja na kuku, samaki mwenye maji ya machenza, kamba wa Taiji na samaki waliokaangwa.

Vitoweo vya Anhui

Vitoweo vya Anhui ni pamoja na vya sehemu ya kusini ya Anhui na sehemu za kando mbili za mto Changjiang na Huai. Vitoweo vya sehemu ya kusini ya Anhui ni maarufu zaidi.

Umaalumu wa vitoweo hivyo ni kuongeza ladha ya vitoweo kwa ham, sukari na kwa mbinu ya kuchemsha kwa moto mkubwa na mdogo.

Vitoweo maarufu ni pamoja na nyama ya mabata yaliyochanganywa na mbuyu na kuku.

Vitoweo vya Sichuan vyenye sifa za vitoweo vya sehemu mbalimbali

Kati ya vitoweo vya maeneo maalumu manane, vitoweo vya mkoa wa Sichuan vimeenea katika sehemu nyingi zaidi.

Vitoweo vya Sichuan vinajulikana kwa miaka mingi, na vimewavutia watu wa nchini na wa nchi za nje kwa sifa yake ya kipekee. Vitoweo vya Sichuan vinazingatia rangi, harufu, namna vinavyoonekana na hususan ladha yake, na kutumia ipasavyo viungo vya aina mbalimbali.

Pamoja na maendeleo ya uzalishaji mali na ustawi wa uchumi, juu ya msingi wake wa asili, vitoweo vya Sichuan vina sifa za vitoweo vya sehemu za kusini na kaskazini pamoja na ubora wa vitoweo vya karamu ya kuribisha wageni. Hivi sasa vitoweo vya Sichuan vimekuwa na sifa kubwa, ambayo watu wanasema, "Chakula kizuri kiko China, Vitoweo vitamu viko Sichuan".

Vitoweo vya Sichuan vinatia maanani mabadiliko ya ladha, ambavyo hakuna kitoweo kinachokosa viungo vya aina tatu muhimu, yaani pilipili, mbegu za Bunge prickly ash na pilipili manga.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-11