Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-13 21:22:48    
Mtaalamu wa China atazamia matokeo ya upigaji kura wa maoni ya raia kuhusu katiba mpya ya Iraq

cri

Upigaji kura wa maoni ya raia kuhusu katiba mpya utafanyika tarehe 15 mwezi huu, ambapo wapiga kura waliojiandikisha wapatao milioni 15 watashiriki upigaji kura huo. Hili ni jambo kubwa katika mchakato wa ukarabati wa kisiasa nchini Iraq. Katiba mpya ya Iraq itapitishwa au la? Mwandishi wetu wa habari amemhoji mtafiti wa idara ya utafiti wa Asia ya magharibi na Afrika katika Taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bwana Yin Gang.

Bwana Yin Gang alisema kuwa, dalili zenye juhudi zimeonekana katika maendeleo ya hali ya mambo nchini Iraq hivi karibuni. Madhehebu ya Suni yaliyowahi kususia kithabiti katiba mpya hapo kabla, tarehe 11 yalikuwa na mazungumzo na madhehebu ya Shia na kundi la wakurd, maendeleo yamepatikana katika mazungumzo hayo, chama zaidi ya kimoja cha madhehebu ya Suni kimeahidi kuwa kitawaita wanachama wao kupiga kura ya ndio juu ya katiba mpya, hii imeongeza uwezekano wa kupitishwa kwa katiba mpya. Wakati huo huo, viongozi wa makundi makuu ya kisiasa ya Iraq pia wamekubali kurekebisha vifungu kadhaa vya katiba mpya ili kupata uungaji mkono wa wapiga kura wengi zaidi juu ya katiba hiyo mpya. Bwana Yin Gang alisema:

Hii imeonesha matumaini mazuri waliyo nayo wananchi wa Iraq hata wakiwemo wale wa madhehebu ya Suni wenye wasiwasi juu ya mchakato wa siasa wa Iraq, kwamba wanatumai mafanikio yatapatikana katika mchakato wa ukarabati wa kisiasa wa nchi hiyo, pia kuonesha akili zao za kisiasa.

Bwana Yin Gang alifafanua kuwa, kwa kweli kutokana na kanuni za katiba ya muda ya Iraq, hakuna uwezekano mkubwa kwa kufutwa kwa katiba mpya. Katiba ya muda ya Iraq iliwekwa kuwa, kama kuna theluthi mbili ya wapiga kura wa mikoa mitatu yoyote kati ya mikoa 18 ya Iraq watapiga kura za hapana, katiba mpya haitapitishwa. Bwana Yin Gang alisema:

Kama theluthi mbili ya wapiga kura watapiga kura ya hapana, hii itaomaanisha kuwa watu hao si kama tu wanapinga kifungu Fulani au vifungu kadhaa Fulani vya mswada wa katiba, bali wanataka kutokomeza mswada huo, tena wanataka kufanya tena uchaguzi mkuu, kuchagua upya bunge la taifa, na kuunda upya kamati ya utungaji wa katiba, hayo yote yatakuwa kazi ngumu, hivyo hali hii haitaweza kutokea.

Bwana Yin Gang anaona kuwa, asilimia 80 ya wapiga kura watashiriki katika upigaji kura wa maoni ya raia kuhusu katiba mpya.

Upigaji kura huo ni upigaji kura wa kudumu ambao unahusiana na katiba ya taifa, idadi ya wapiga kura wa safari hii ingezidi ile ya wapiga kura walioshiriki uchaguzi wa bunge la mpito uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu.

Bwana Yin Gang alisisitiza kuwa, kama katiba ya Iraq itaptishwa kwenye upigaji kura wa maoni ya raia, itakuwa na umuhimu mkubwa. Hii itaonesha kuwa mchakato wa kisiasa wa Iraq utaingia kipindi kipya, hayo vilevile yatakuwa mafanikio makubwa zaidi yaliyopatikana katika mchakato wa kisiasa wa Iraq chini ya juhudi za pamoja za jumuia ya kimataifa. Alisema, kama hali ni hiyo, maisha ya kisiasa nchini Iraq yataingia katika hali ya kawaida, wananchi wote wa Iraq watafuata katiba katika shughuli zao, katiba hiyo itawasaidia wananchi wa Iraq wajiendeshe nchi yao na kulinda usalama wa jamii yao.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-13