Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-17 17:49:48    
Kitendo kikaidi cha makosa cha Waziri mkuu wa Japan hakika kitasababisha matokeo mabaya

cri

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi tarehe 17 asubuhi kwa mara nyingine tena amekwenda kwenye Hekalu la Yasukuni kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita. Hii ni mara ya tano kwa waziri mkuu huyo kwenda kwenye hekalu hilo tangu ashike wadhifa mwezi Aprili mwaka 2001, pia ni kitendo chake cha kudhuru tena hisia za wananchi wa nchi husika za Asia bila kujali upinzani mkali na maonyo ya watu nchini Japan na nchi jirani za Asia. Kitendo hiki cha kikaidi cha makosa hakika kitaudhuru vibaya uhusiano kati ya China na Japan, waziri mkuu huyo anapaswa kubeba lawama kutokana na matokeo ya kitendo chake.

Undani wa kwenda kwenye hekalu la Yasukuni ni kuwa, Japan inatambua sahihi au la historia ya vita vya uvamizi vilivyoanzishwa na wanajeshi wa Japan. Kwenye hekalu la Yasukuni kuna vibao vya wahalifu wa kivita wa ngazi ya A kama vile Hideki Tojo na wengineo ambao walikuwa waanzilishi na viongozi wa vita vya kuzivamia nchi za nje vilivyoanzishwa na Japan. Wahalifu hao waliwaua wananchi wengi wa nchi mbalimbali wa Asia zilizodhuriwa vibaya na vita vya uvamizi vilivyoanzishwa na wanajeshi wa Japan, hekalu la Yasukuni ni alama ya Japan ya kufanya uvamizi na upanuzi nje ya nchi hiyo na ni hekalu ambapo mizimu ya wahalaifu wa kivita inaabudiwa. Mwaka huu wakati wa kuadhimisha miaka 60 tangu ushindi upatikane katika vita vya kupambana na ufashisti duniani na katika mapambano ya wananchi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan, serikali ya Japan ingejikosoa kwa kina juu ya vita hivyo, na kukumbuka mafunzo ya historia ili kuzuia balaa kama hilo lisitokee tena. Lakini katika wakati huo, waziri mkuu huyo wa Japan amekwenda tena kwenye hekalu la Yasukuni, kitendo hiki kimeonesha kuwa hana udhati wa kutambua historia ya vita vya uvamizi vya zamani, hana udhati wa kuomba radhi kwa wananchi wa nchi za Asia walioteswa na wanajeshi wa Japan, na hana udhati wa kutambua historia ya uvamizi. Je, serikali ya namna hii na kiongozi wake wana uaminifu gani? Japan itawezaje kupata uaminifu kutoka kwa nchi za Asia na jumuiya nzima ya kimataifa?

Watu wameona kuwa, tokea mwishoni mwa mwaka jana, waziri mkuu huyo wa Japan aliahidi mara kwa mara kuwa atachambua mwafaka suala la hekalu la Yasukuni. Jumuiya ya kimataifa inatumai kuwa uchambuzi wake mwafaka ni kuwa atatambua wazi hali nyeti na hali mbaya ya kwenda kwenye hekalu hilo, ili kuchukua uamuzi sahihi wenye busara. Lakini watu wanasikitika kuwa, waziri mkuu huyo amekwenda tena kwenye hekalu hilo kutoa heshima kwa mizimu ya wahalifu wa kivita badala ya kufuata nia ya jumuiya ya kimataifa. Hili ni kosa kubwa kabisa.

Jambo linalostahili kutajwa ni kuwa, safari hii Bw Koizumi amekwenda kwenye hekalu la Yasukuni katika hali ambayo vyama visivyo vya utawala vya Japan na watu wa ndani ya chama tawala wanapinga vikali, hata mahakama kuu ya Osaka ilitoa hukumu kuwa kitendo chake kinakiuka katiba. Hii imeonesha ukaidi wake mkubwa wa kutambua kwa makosa suala la kwenda kwenye hekalu hilo kutoa heshima kwa wahalifu wa kivita.

Serikali ya China siku zote inatilia maanani uhusiano kati ya China na Japan na kufanya juhudi kuwawezesha wananchi wa nchi hizo mbili kuwa na urafiki kizazi baada ya kizazi. Kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 60 tangu ushindi upatikane katika mapambano ya wananchi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan na katika vita vya kupambana na ufashsti duniani, rais Hu Jintao wa China alipotoa hotuba pia alisisitiza kuwa, sera ya serikali ya China ya kuendeleza uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na Japan haibadiliki. Lakini kitendo cha Bw Koizumi kimekiuka ahadi ya serikali ya Japan kuhusu masuala ya kishitoria na kukiuka msingi wa kisiasa wa uhusiano wa China na Japan, pia kimedhuru hisia za wananchi wa China. Katika hali hiyo, ni vigumu kuendeleza vizuri uhusiano kati ya China na Japan. Bw Koizumi ni lazima abebe lawama juu ya matokeo ya kitendo chake.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-17