Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-18 16:31:04    
WTO yaanza kushughulika na mgogoro wa biashara ya ndege kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya

cri

Habari kutoka WTO tarehe 17 zinasema kuwa WTO imeunda vikundi viwili vya wataalamu na kufanya uchunguzi kuhusu kesi iliyotolewa na pande mbili, Marekani na Umoja wa Ulaya, kuhusu ruzuku isiyostahiki ya matengenezo ya ndege na kuutolea hukumu mgogoro wa biashara ya ndege kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya. Kutokana na kuwa Marekani na Umoja wa Ulaya zinaongoza duniani katika utengenezaji wa ndege kubwa za kiraia, na mgogoro huo unahusika na fedha nyingi, mgogoro huo ni mkubwa ndani ya WTO na unafuatiliwa sana.

Mwaka 1992 pande mbili ziliwahi kukubaliana kuwa ruzuku ya Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kutengeneza ndege za Airbus haitaruhusiwa kuzidi 33% ya gharama zote na Marekani haitaruhusiwa kuzidi 3% ya gharama zote za mauzo ya ndege za Boeing kwa mwaka. Lakini wakati huo kampuni ya Boeing haikutia maanani kampuni ya Airbus ambayo ilikuwa mwanzoni tu.

Kwa muda mrefu kampuni ya Boeing ilikuwa inajivunia hali yake nzuri bila kutaka kujiendeleza, hatua na hatua kampuni hiyo imeachwa nyuma na kupoteza uwezo wa ushindani. Kinyume na hali hiyo kampuni ya Airbus ilijitahidi kujiendeleza na imepata mafanikio makubwa. Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2001 na 2002 ndege za airbus zilizouzwa sokoni zilichukua 38% na 44% ya ndege zote duniani, mwaka 2003 ndege zilizotengenezwa zilifikia 305, kwa mara ya kwanza zilizidi ndege za Boeing zilizotengenezwa 281 mwaka huo. Kwa makadirio, ndege za Airbus zitaendelea kuongoza duniani kuliko Boeing katika miaka kadhaa ijayo, na zitachukua theluthi mbili ya soko la ndege duniani.

Maendeleo ya Airbus yamekuwa tishio kwa Boeing, basi tarehe 6 Oktoba mwaka jana Marekani iliwasilisha mashitaka yake kwenye WTO ikisema kuwa muda wa kutoa ruzuku kwa Umoja wa Ulaya umekuwa na miaka mingi hata 35, na mauzo ya ndege za Airbus yamezidi ndege za Boeing, kwa hiyo Umoja wa Ulaya haufai kuendelea kutoa ruzuku ambayo hapo awali ilitolewa kwa ajili ya kusaidia "kampuni changa" ya Airbus, na kusema kuwa ruzuku kwa ajili ya kutengeneza ndege aina ya airbus A308 hata imefikia bilioni 6.5, tena inafikiria kutoa ruzuku kwa ajili ya kuendeleza aina ya A350. Ruzuku hizo zote zinakwenda kinyume na kanuni za WTO.

Baada ya Marekani kuushitaki Umoja wa Ulaya kwa muda wa saa chachache tu mara Umoja wa Ulaya ukaing'ata Marekani kwa kupeleka shitaka lake kwenye WTO likisema kuwa oda ya ndege za kijeshi iliyoagizwa na ikulu ya Marekani na gharama za utafiti kwa ajili ya kampuni ya Boeing zote ni "ruzuku kwa sura nyingine", na serikali ya Marekani hata imetunga sheria ya fursa maalumu kwa mapato ya ndege zinazouzwa katika nchi za nje na kutoa ruzuku na msaada wa dola za Kimarekani milioni 200 kwa ajili ya kampuni ya Boeing. hivi karibuni Marekani imetoa msamaha wa ushuru na msaada wa ujenzi wa miundombinu. Ruzuku hizo kwa jumla zimefikia dola za Kimarekani bilioni 23 na kusababisha hasara ya Airbus. Huu ni ushahidi mwingine wa Marekani kwenda kinyume na kanuni za WTO kuhusu ruzuku.

Tarehe 11 Januari mwaka huu pande mbili zilitangaza kusimamisha mashitaka na kurudi tena kwenye mazungumzo, na kutangaza kuwa zitajitahidi kufuta ruzuku ndani ya miezi mitatu kwa pande zote ili kuanzisha "soko la haki". Lakini baada ya muda wa miezi mitatu kupita, pande mbili bado hazikukubaliana. Kutokana na hali hiyo mwezi Mei Marekani ilitaka WTO iunde vikundi viwili vya wataalamu kufanya uamuzi. Lakini uchaguzi wa wataalamu wa vikundi hivyo uligonganisha pande mbili, basi jukumu hilo la kuamua wataalamu limemwangukia mkurugenzi mkuu mpya wa WTO Pascal Lamy. Kwa sababu Bw. Lamy alitoka kutoka kamati ya Biashara ya Umoja wa Ulaya, alimwagiza naibu wake kuwajibika ili kujiepusha na lawama.

Inasemekana kwamba vikundi hivyo vilivyoundwa tarehe 17 vina wataalamu watatu kutoka biashara huru ya kimataifa, watafanya uamuzi katika muda wa miezi 6 hadi 9 baada ya kufanya uchunguzi. Upande wowote ukiwa na pingamizi kuhusu uamuzi unaweza kukata rufani mahakama ya WTO. Vyombo vya habari vinaona kuwa kutokana na kesi hiyo kuwa na utatanishi na inahusika maslahi makubwa ya pande mbili, kesi hiyo inaweza ikachukua muda mrefu.

Idhaa ya kiswahili 2005-10-18