Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-18 17:53:09    
Nchi zilizoendelea zinapaswa kuwajibika na kazi ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini

cri

Mkutano wa kuadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ulifanyika tarehe 17 huko Rome, Italia. Wakuu na wajumbe wa nchi mbalimbali waliohudhuria mkutano huo wametoa mwito kuwa nchi zilizoendelea zinapaswa kuwajibika na kazi ya jumuiya ya kimataifa ya kutatua matatizo ya njaa, umaskini na utapiamlo.

Tangu kuanzishwa kwa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa mwaka 1945, shirika hilo linafanya juhudi kubwa bila kulega hata kidogo na limetoa mchango mkubwa katika kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea katika usalama wa nafaka, maendeleo endelevu ya vijiji na ufundi vijijini. Lakini hali ya jumla ya usalama wa nafaka duniani bado si ya kufurahisha, tatizo la njaa bado ni adui mkubwa anayekabili maendeleo ya jamii ya binadamu. Kwenye mkutano huo, rais Festus Mogae wa Botswana alizungumzia matatizo yanayoikabili sehemu ya Afrika kusini ya Sahara. Akisema:

Njaa na maradhi ni vyanzo vya balaa kwa wananchi wa Afrika. Njaa na utapiamlo hakika ni matatizo makubwa kabisa yanayowakabili wananchi wa nchi za dunia ya tatu. Matatizo hayo yanaufanya utimizaji wa malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa kuwa jambo gumu sana.

Kwenye mkutano huo, rais Robert Mugabe aliainisha kuwa, jumuiya ya kimataifa hasa nchi zilizoendelea zinapaswa kufuatilia zaidi nchi zinazoendelea, kuacha ulinzi wa kibiashara, na kufungua soko. Rais Mugabe alisema:

Katika siku ya hivi leo ya karne ya 21, kutokana na kukabiliwa na matatizo ya njaa na umaskini, mtu yeyote na nchi yoyote zote zitaweza kukabiliwa na tishio. Kama nchi zilizoendelea hazitafuta sera ya utoaji ruzuku za kilimo na misaada mingine kwa mazao ya kilimo kwa nchi zao, maendeleo ya kilimo ya nchi zinazoendelea siku zote yatakabiliwa na vizuizi vikubwa, na maslahi ya kiuchumi ya nchi zinazoendelea yatapata hasara.

Nchi 32 kati ya nchi 38 maskini zinazodaiwa madeni makubwa duniani, 32 ni za Afrika. Na nyingi kati ya hizo ni nchi ndogo ambazo hazina uwezo wa kulipa madeni. Jumuiya ya kimataifa hasa nchi zilizoendelea zinapaswa kuwajibika na kazi ya kuisaidia Afrika kuondokana na umaskini.

Rais Carlo Azeglio Ciampi wa Italia akiwa mjumbe wa nchi zilizoendelea alipotoa hotuba alisisitiza kuwa, kuondoa mzigo mkubwa wa madeni ni msingi wa kuzisaidia nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini, kwa kupitia tu njia hiyo ndipo itakapowezekana kuondoa tishio kubwa linalomkabili binadamu tangu kuingia karne ya 21.

Kwenye mkutano huo, katibu mkuu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa Bwana Jacques Diouf pia amesisitiza umuhimu wa China katika mapambano ya dunia nzima dhidi ya njaa na umaskini uliokithiri. Akisema:

Katika mchango wa kuimarisha usalama wa nafaka na kuondoa umaskini, ushirikiano kati ya China na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa hauwezi kukosekana. China ikiwa nchi kubwa inayoendelea, inatoa mchango mkubwa katika ongezeko la kilimo na kuimarisha usalama wa nafaka na kuondoa umaskini. Wakati huo huo kwa kupitia utaratibu wa ushirikiano kati ya kusini na kusini, China inatoa misaada ya nafaka na ufundi wa kilimo kwa Afrika na nchi nyingine zinazoendelea.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-18