Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-18 17:55:22    
Kitendo cha Bw Koizumi kutoa heshima kwenye hekalu la Yasukuni ni cha kijinga

cri

  

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi tarehe 17 alikwenda tena kutoa heshima kwenye hekalu la Yasukuni, ambapo vimewekwa vibao vya mizimu vya wahalifu wa kivita wa ngazi ya kwanza bila kujali upinzani mkali wa vyombo vya habari vya nchini Japan na vya nchi za nje. Hii ni mara ya 5 kwa Bw Koizumi kutembelea hekalu la Yasukuni tangu alipochukua wadhifa wa uwaziri mkuu. Lakini ni kwa nini Bw Koizumi ni mkaidi kiasi hicho kuhusu suala la kutembelea hekalu la Yasukuni? Kwa nini amechagua tarehe 17 kutembelea hekalu hilo? Mwandishi wetu wa habari aliwahoji mtafiti wa idara ya masuala ya Japan ya taasisi ya sayansi ya jamii ya China Bw. Gao Hong na mkurugenzi wa kitivo cha historia cha chuo kikuu cha ualimu cha Shanghai Bw. Su Zhiliang kuhusu masuala hayo.

Bw. Gao Hong alisema kuwa kutembelea tena hekalu la Yasukuni kwa Bw Koizumi kunaonesha kuwa yeye bado anajidanganya na kuwadanganya watu wengine kuhusu masuala ya historia, bila shaka atapingwa na watu wa nchi nyingine za Asia, hiki ni kitendo cha kijinga. Alisema,

"Kutembelea hekalu la Yasukuni au la kunaonesha mtazamo wa serikali ya Japan na wanasiasa wa nchi hiyo kuhusu masuala ya historia. Kutembelea hekalu la Yasukuni ambako vimewekwa vibao vya mizimu ya wahalifu wakuu wa kivita, siyo tu kuwa kunadhuru hisia za watu wa nchi jirani zake bali pia kunaipeleka Japan kwenye njia ya makosa. Hivyo kwa kuangalia kutoka maslahi ya muda mrefu ya watu wa Japan, maslahi ya watu wa nchi mbalimbali za Asia au utulivu na ustawi wa sehemu hiyo nzima, kitendo cha Bw Koizumi ni cha makosa na kinastahili kulaaniwa na kukosolewa."

Alipozungumzia sababu za kushikilia kutembelea hekalu la Yasukuni kwa Koizumi Bw. Gao Hong alisema kuwa, Koizumi anachukulia dhamira ya wananchi kuwa dau linalowekwa katika mchezo wa kamari, akijaribu kuathiri dhamira ya watu wa Japan kwa imani dhamira yake mwenyewe. Alisema,

"Kwa Koizumi, ili kutekeleza siasa na dhamira yake, kufuata njia ya nchi kubwa ya kisiasa na kijeshi, anajitahidi kutoa wito au kuonesha mfano akitaka kuamsha 'heshima ya taifa na uhamasa wa uzalendo' wa watu wa Japan. Kutokana na wazo hilo, kitendo chake cha kutembelea hekalu la Yasukuni ni cha makosa kabisa."

Bw. Gao Hong alisema kuwa Bw Koizumi kuchagua tarehe 17 kutembelea hekalu la Yasukuni kunatokana na mawazo yake yafuatayo,

"Kwanza, majukumu muhimu ya bunge la taifa yametimizwa kwa jumla, anaona kuwa anaweza kudhibiti hali ya kisiasa ya Japan kwa urahisi, hivyo akafanya ujasiri kutembelea kwa mara nyingine tena kwenye hekalu la Yasukuni ili kupata uungaji mkono wa watu wa kundi la mrengo wa kulia; Pili, Bw Koizumi anatakiwa kuunda upya baraza la mawaziri mwanzoni mwa mwezi Novemba, hii ni ishara anayotoa kwa baraza jipya la mawaziri, na pia ni kuonesha msimamo wake kuhusu mambo ya kidiplomasia, usalama na kijeshi, na kuonesha kuwa ataendelea kutekeleza sera zake za kidiplomasia."

Bw. Gao Hong alisema kuwa kuna baadhi ya sababu nyingine, ambazo huenda ni pamoja na kuwa tarehe 17 ilikuwa ni siku ya kurejea kwa chombo cha anga cha China "Shenzhou No.6", ambapo wachina wengi walikuwa wakifuatilia sana habari kuhusu kurejea kwa chombo hicho.

Kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano wa China na Japan Profesa Su Zhiliang anaona kuwa, China na Japan ni nchi majirani na zina maslahi ya pamoja, hivyo nchi mbili zinatakiwa kudumisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali. Ametoa wito wa kutaka serikali ya Japan kuzingatia mambo makubwa na kuyatendea kwa hatua mwafaka masuala ya historia. Alisema kuwa katika karne ya 21, Asia imepata nyakati za maendeleo ya amani, hivyo unatakiwa msimamo wa kuangalia mbele, serikali ya Japan inatarajiwa kuacha kabisa kitendo chake cha makosa cha kutembelea hekalu la Yasukuni.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-18