Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-19 17:34:27    
Mapishi ya vipande vya nyama ya nguruwe

cri

Mahitaji:

Nyama ya nguruwe gramu 300, pilipili mboga gramu 100, vipande vya vitunguu maji gramu 5, mvinyo wa kupikia gramu 15, M.S.G gramu 2, ute wa yai moja, maji ya wanga gramu 25, mafuta ya ufuta gramu 5.

Njia:

1. kata nyama ya nguruwe iwe vipande vipande, baada ya kuosha ikaushe na uiweke kwenye bakuli moja, tia chumvi, ute wa yai, na maji ya wanga korogakoroga. Kata pilipili mboga iwe vipande vipande.

2. pasha moto tia mafuta kwenye sufuria, mpaka yawe na joto la nyuzi 50, tia vipande vya nyama ya nguruwe na koroga kwa haraka na tia pilipili mboga korogakoroga halafu ipakue.

3. pasha moto tena mimina mafuta kidogo, tia vipande vya vitunguu maji, nyama ya nguruwe na pilipili mboga korogakoroga, mimina maji kidogo na tia M.S.G, chumvi na mvinyo wa kupikia, korogakoroga, mimina maji ya wanga, na mafuta ya ufuta korogakoroga halafu vipakue. Mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-12