Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-19 19:28:10    
Kondoo wenye manyoya membamba

cri

Habari kutoka kwa idara ya ufugaji ya mji wa Chaoyang mkoani Liaoning siku za karibuni zinasema kuwa, kutokana na juhudi za kampuni ya maendeleo ya teknolojia ya ufugaji ya Yi Xing ya mji wa Chaoyang na wataalamu wa ufugaji wa mkoa huo katika miaka kadhaa iliyopita, aina mpya ya kondoo wenye manyoya membamba zaidi wamezalishwa kwa mafanikio, na kuifanya China iwe nchi ya pili kuwa na kondoo wa aina hiyo duniani.

Kikundi cha wataalamu cha kamati ya raslimali ya mifugo ya mkoa wa Liaoning kimethibitisha kuwa, kipenyo cha wastani cha manyoya ya aina hiyo ya kondoo ni micron 14.77, na kipenyo cha manyoya ya kondoo jike ni micron 14.64, ambazo zote zimevuka vigezo vya kimataifa yaani micron 18.

Imefahamika kuwa, kondoo wa aina hiyo wanaweza kuwa na manyoya yenye kipenyo chini ya micron 18. manyoya hayo yanaweza kutumiwa katika kufuma vitambaa vya hali ya juu sana. Hivi sasa, kondoo wa aina hiyo wanaweza kupatikana nchini Australia tu.

Kuzalisha kondoo wenye manyoya membamba zaidi ni moja ya miradi ya 863 ya taifa ya utafiti wa sanyasi na teknolojia. mwishoni mwa miaka ya 90 ya karne iliyopita, wataalamu wa ufugaji wa mji wa Chaoyang wameanza kutafiti uzalishaji wa kondoo wa aina hiyo. Wilaya ya Jianping ni moja ya vituo vya kuzalisha manyoya membamba, na pia ni sehemu ya kuzalisha na kuhifadhi kondoo bora ya Kaskazini Mashariki ya China, ambayo ina historia ndefu ya kuzalisha kondoo wenye manyoya membamba.

Kwa wastani, kila Kondoo wa manyoya membamba wa kaskazini masharika ya China anaweza kutoa kilo 13.5 za manyoya, na kwa kondoo jike ni kilo 6. manyoya hayo ni membamba sana na yamefikia kiwango cha ubora wa manyoya ya kondoo wa Austrilia.

Wataalamu wamefanikiwa kuzalisha kundi la kondoo wa aina mpya kwa kutumia teknolojia za jeni, na idadi ya kondoo kwenye kundi hilo imefikia 565. aina hiyo ya kondoo inaweza kuzalisha manyoya mengi zaidi, ambayo kondoo jike wanazalisha kilo 5 za manyoya na kwa kondoo dume kilo 7.5.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-19