Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-19 19:30:31    
Siku ya kuadhimisha miaka 110 tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Tianjin

cri

Tarehe 2 mwezi Oktoba ni siku ya kuadhimisha miaka 110 tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Tianjin ambacho ni chuo kikuu cha kwanza katika zama ya karibu ya China.

Wahitimu zaidi ya 5000 wa chuo hicho kutoka nchini na ng'ambo pamoja na wanafunzi na walimu wa chuo hicho waliiadhimisha siku hiyo kwa njia rahisi.

Chuo kikuu cha Tianjin inatokana na chuo kikuu cha Beiyang ambacho kilianzishwa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 1895. mwaka 1951, chuo kikuu hicho kilibadilishwa jina kuwa chuo kikuu cha Tianjin. Mwaka 1959, chuo hicho kiliidhinishwa na baraza la mawaziri kuwa kimoja kati ya vyuo vikuu 16 muhimu vya taifa. Mwezi Desemba mwaka 2000, chuo kikuu cha Tianjin kilikuwa kimoja cha vyuo vikuu hodari vya China vilivyojulikana nchini na duniani ambavyo vinawekwa mkazo na serikali ya China katika karne mpya. Katika karne kadhaa zilizopita, chuo kikuu cha Tianjin siku zote kinashikilia wito wa chuo kicho "kushughulikia mambo kwa kufuata hali halisi" na moyo wa uzalenda na kutoa mchango kwa ajili ya taifa, kuandaa wahitimu hodari zaidi ya laki moja na kupata mafanikio mengi mazuri ya sayansi na teknolojia.

Tarehe 2, mwandishi wetu wa habari alipoingia kwenye chuo hicho, hakuona ufujaji kwenye maadhimisho lakini aliweza kusikia hali ya furaha kila mahali. Wanafunzi na wahitimu waliorudi walikuwa na pilikapilika za kuandaa sherehe. Hakuna sherehe kubwa, ila tu mkusanyiko wa wahitimu wa chuo hicho, maonesho ya historia ya chuo, mihadahara ya baraza la maendeleo inayotupia macho siku za baadaye, mabadilishano ya kiutamaduni, shughuli za hisani kwa ajili ya maadhimisho hayo, na sherehe ya kuweka jiwa la kimsingi na kuzindua. Ndiyo kwa njia hiyo rahisi, wanafunzi na wakulima wa chuo hicho waliadhimisha siku hiyo ya miaka 110 ya kuanzishwa kwa chuo chao.

"kukumbusha historia na kurithi utamaduni mzuri; kutupia macho siku za baadaye na kujitahidi kuendelea na kuvumbua; kuungana katika kuvumbua mafanikio mapya; kuhamasisha katika kujenga chuo kikuu cha kiwango cha juu" ni agizo la maadhimisho hayo. Kwenye maadhimisho hayo, sherehe ya kuizindua sanamu ya nta ya mwazilishi wa chuo kikuu cha Beiyang na elimu ya juu katika zama ya karibu ya China Marehemu Sheng Xuanhuai ilifanyika.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-19