Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-20 17:39:37    
Mabadiliko ya uhusiano kati ya Iran na Marekani yanategemea mwelekeo wa suala la nyuklia la Iran

cri

Hivi karibuni dalili ya hali wasiwasi imetokea katika uhusiano kati ya Uingereza na Iran. Uingereza inailaani Iran kuhusika na tukio la mashambulizi dhidi ya jeshi la Uingereza lililoko kwenye sehemu ya kusini ya Iraq, na Iran inalaani Uingereza kuhusika na milipuko miwili iliyotokea katika jimbo la Khuzestan la kusini ya Iran.

Uingereza siku zote inailaani Iran na chama cha Hezbollah cha Lebanon kinachoungwa mkono na Iran kutoa vifaa na ufundi kwa watu wenye silaha wa Iraq ili watu hao waweze kuanzisha mashambulizi dhidi ya jeshi la Uingereza lililoko kwenye sehemu ya kusini mwa Iraq. Tarehe 16 mwezi huu waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bibi Condoleezza Rice alitoa lawama hizo kwa mara nyingine tena. Lakini Iran imepinga lawama dhidi yake. Hata Iran iliilaaini Uingereza ni "mchokozi wa nyuma" wa milipuko miwili iliyopita tarehe 15 katika jimbo la Khuzestan la kusini magharibi ya Iran. Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran tarehe 18 alisema kuwa Uingereza ilishiriki kwenye tukio la kuzusha milipuko hiyo. Maneno hayo yameleta hali wasiwasi zaidi katika uhusiano kati ya Iran na Uingereza. Vyombo vya habari vya Iran hata vimeitaka serikali isimamishe uhusiano wa kibalozi na Uingereza.

Wachambuzi wanaona kuwa, hali wasiwasi ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili kwa kweli imeonesha mapambano kati ya nchi za magharibi na Iran kuhusu suala la nyuklia la Iran.

Nchi tatu Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinazowakilisha Umoja wa Ulaya zilifanya mazungumzo na Iran kuhusu suala la nyuklia kuanzia mwaka 2003, Umoja wa Ulaya unajaribu kupitia mbinu za kidiplomasia na kiuchumi kuihimiza Iran iache mpango wa nyuklia. Mwezi Novemba mwaka 2004, Iran na nchi hizo tatu zilifikia makubaliano ya kuacha kwa muda shughuli za kusafisha uranium nzito. Lakini baada ya Ahmadinejad kuchaguliwa kuwa rais wa Iran, rais huyo amechukua sera imara kuhusu suala la nyuklia, na kufufua shughuli kadhaa za kinyuklia. Tarehe 24 Septemba, shirika la nishati ya atomiki la kimataifa lilipitisha azimio la kuitaka Iran iache mara moja shughuli zote zinazohusika na uranium nzito, lakini Iran ilikataa azimio hilo. Kuanzia hapo suala la nyuklia la Iran likakwama. Hivi karibuni ingawa serikali ya Iran imeeleza kuwa inapenda kufufua mazungumzo na Umoja wa Ulaya, lakini bado inashikilia kudumisha haki yake ya matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia. Msimamo huo una pengo kubwa na ule wa Umoja wa Ulaya wa kuitaka iache shughuli za uranium nzito.

Kwa upande mwingine, maoni ya Umoja wa Ulaya na Marekani kuhusu suala la nyuklia yameelekea kuwa ya pamoja siku hadi siku. Hivi sasa Marekani na nchi washiriki wake wa magharibi zinafuatilia kama Iran kama itarudi kwenye meza ya mazungumzo au la, kama haitarudi kwenye mazungumzo, nchi hizo zinataka kupitia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuiwekea Iran vikwazo vya kiuchumi na kuipa adhabu nyingine.

Wachambuzi wanaona kuwa, uhusiano kati ya Iran na Uingereza umebadilika kuwa na hali ya wasiwasi kwa dharura, hii si kama tu imeonesha mapambano kati ya Iran na Uingereza, bali pia imeonesha utatanishi mkubwa wa uhusiano na maslahi ya pande mbalimbali zinazohusika juu ya suala la nyuklia la Iran. Kama Iran ikisimamisha uhusiano wa kibalozi kati yake na Uingereza, itaziba kabisa mlango wa kufanya mazungumzo na Umoja wa Ulaya, na kusababisha mvutano kati ya Iran na magharibi kupambamoto, hii hailingani na maslahi ya Iran; hali kadhalika, kama mazungumzo kati ya nchi tatu za Uingereza, Ufaransa na Ujerumani na Iran yatavujika kabisa, hii vilevile hailingani na maslahi ya Uingereza na Umoja wa Ulaya. Hivyo mabadiliko ya uhusiano kati ya Iran na Uingereza yatategemea mwelekeo wa maendeleo ya suala la nyuklia la Iran.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-20