Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-21 16:09:16    
Iran yapiga hatua muhimu kwenye suala la nyuklia

cri

Shirika la habari la magharibi lilieleza tarehe 20 kuwa serikali ya Iran iko tayari kuliwasilisha shirika la nishati ya atomiki duniani nyaraka muhimu kuhusu mpango wake wa nyuklia na kukubali shirika hilo limhoji ofisa mwandamizi wa Iran anayeshughulikia mpango huo. Wachambuzi wameainisha kuwa, hii ni hatua muhimu iliyopigwa na Iran kwa ajili ya kutatua suala la nyuklia yake.

Umoja wa Ulaya na Marekani zote zinauchukulia mpango wa nyukilia wa Iran kama ni sehemu moja ya mpango wa silaha za nyuklia. Zinaona kuwa Iran ilifanya shughuli za nyuklia kwa muda mrefu bila kutoa taarifa kwa shirika la nishati ya atomiki duniani, jambo ambalo limekwenda kinyume na ahadi iliyotoa hapo awali kwa jumuiya ya kimataifa. Zaidi ya hayo, haijulikani kuwa katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, Iran ilipata teknolojia gani ya kufanya shughuli za uranium nzito, zana hizo zimewekwa wapi na kama zana na teknolojia hizo zimetumika kutengeneza silaha za nyuklia au la. Nchi za magharibi zinaona kuwa masuala hayo hayajafahamishwa na Iran na yamesababisha suala la nyuklia la Iran kutotatuliwa hadi leo.

Tarehe 24 mwezi uliopita, shirika la nishati ya atomiki duniani lilipitisha azimio lililotolewa na Umoja wa Ulaya kuhusu suala la nyuklia la Iran ambalo linataka Iran isimamishe shughuli zote zinazohusiana uranium nzito. Azimio hilo linaashiria kuwa kama Iran itakataa matakwa hayo, shirika hilo litatoa ripoti kuhusu suala hilo kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa katika wakati mwafaka.

Je, ni kwa nini Iran imefanya kitendo hicho cha kuimarisha ushirikiano na shirika hilo baada ya mwezi mmoja tangu azimio hilo lilipopitishwa? Watu wanaona kuwa azimio la shirika hilo limeifanya Iran ikabiliane na uchaguzi mzito, kuwa Iran inalindaje haki yake bila kupambana moja kwa moja na jumuiya ya kimataifa, jambo ambalo ni kazi muhimu inayofanywa na Iran kwenye suala hilo kwa mujibu wa maslahi yake. Kwa hiyo serikali ya Iran imechukua hatua halisi mpya katika suala hilo kutokana na maslahi ya taifa ya Iran.

Pili, wachambuzi wanaona kuwa madhumuni ya kitendo hicho cha Iran ni kurudi nyuma katika masuala kadhaa yasiyo muhimu ili kupata huruma za jumuiya ya kimataifa, na kuhakikisha Iran inapata haki ya kutoa maoni yake katika mazungumzo ya nyuklia.

Tatu, mwezi uliopita pande husika zimefanya usuluhishi kati ya Iran na Umoja wa Ulaya. Iran imejua kuwa kupambana hakutatatua suala hilo ambalo hatimaye litatauliwa kwa mazungumzo kwa chini ya shirika hilo. Iran imejua kuwa msimamo wake mkali ilioshikilia hapo awali umeulazimisha Umoja wa Ulaya kutofanya chochote, ila tu kuchukua vitendo vya pamoja na Marekani. Kama Iran itarudi nyuma katika suala hilo, basi itaufanya Umoja wa Ulaya uendelee kufanya kazi yake maalum, ili kufikia lengo lake la kuitenga Marekani.

Habari zinasema kuwa Umoja wa Ulaya mara moja umejibu kitendo hicho cha Iran. Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya walieleza tarehe 20 kuwa kitendo hicho cha Iran ni cha dhati ambacho kinaweza kudhihirisha uhusiano kati ya jeshi la Iran na mpango wake wa nyuklia. Hivyo Umoja wa Ulaya unafikiri kutowasilisha suala la nyukilia la Iran kwenye baraza la usalama katika mkutano wa bodi ya wakurugenzi ya shirika la nishati ya atomiki duniani utakaofanyika mwezi Novemba.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-21