Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-25 20:02:57    
Matumizi madogo ya maliasili yaipatia kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Taiyuan mapato mengi

cri

Kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Taiyuan ambayo ni kampuni kubwa ya chuma na chuma cha pua na kampuni kubwa kabisa ya chuma kisichopata kutu nchini China inasukuma mbele ujenzi wa kiwanda kinachobana matumizi ya maliasili. Matumizi ya nishati na maji ya kampuni hiyo kwa uzalishaji wa chuma cha pua yamepungua kwa kiasi kikubwa. Kampuni hiyo kimepata mapato mengi kwa matumzi madogo ya maliasili.

Uzalishaji wa chuma kisichopata kutu wa kampuni hiyo uliongezeka kuwa tani laki 7.2 ya mwaka 2004 kutoka tani laki 1.355 ya mwaka 1999, thamani ya uuzaji iliongezeka kuwa yuan bilioni 29 kutoka bilioni 8.7, na kodi inayotoa kwa serikali imefikia yuan milioni bilioni 42.87 kutoka yuan milioni 983.

Wakati uzalishaji wa uchuma cha pua na mapato ya kampuni hiyo inapoongezeka kwa kiasi kikubwa, matumizi ya nishati na maji yanapungua kwa kiasi kikubwa. Katika mwaka 2004, nishati iliyotumikwa kwa kuzalisha tani moja ya chuma cha pua ni kigezo cha makaa ya mawe kilo 948, ambayo ilipungua kwa asilimia 20 kutoka kilo 1198 ya mwaka 1999. Na maji yaliyotumiwa kwa kutengeneza tani moja ya chuma cha pua pia imepungua kuwa tani 7 ya hivi sasa kutoka tani 23. Maji hayo yaliyopunguzwa yanaweza kuipunguzia kampuni hiyo matumizi ya fedha yuan milioni 10 kila mwaka.

Miaka ya karibuni, kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Taiyuan ilianza kutumia teknolojia ya juu, kusukuma mbele uzalishaji usiosababisha uchafuzi, na kutimiza lengo la kubana matumizi ya nishati, maji na vitu vingine, kupunguza uchafuzi na kuongeza mapato. Kuanzia mwaka 1999, kampuni hiyo ilichuja mashine kadhaa zinazotumia nishati nyingi na kusababisha uchafuzi wengi, zikiwemo kinu cha kuyeyusha chuma ambacho kinaweza kuzalisha chuma tani laki 2 kwa mwaka, na kinu za kutengeneza majora ambacho kinaweza kuzalisha majora ya chuma tani laki 5 kwa mwaka, na ilijenga miradi 30 inayohifadhi mazingira vikiwemo miradi ya kushughulikia maji machafu, na kusafisha vumbi katika kinu cha makaa ya mawe na kinu cha kuzalisha umeme. Mwaka 2004, kampuni hiyo ilitenga yuan bilioni 1.569 na kuanzisha miradi kadhaa ya uzalishaji isiyosababisha uchafuzi, ikiwemo teknolojia ya CDQ, kusafisha gesi ya kinu cha makaa ya mawe, kuboresha teknolojia ya kinu cha umeme kwa kufanya uzalishaji usiosababisha uchafuzi, kushughulikia takataka ya chuma cha pua, kusafisha maji machafu, kuzalisha umeme kwa shinikizo la gesi ya tanuri la kuyeyusha chuma, na kwa gesi hiyo.

Baada ya miradi hayo kumalizika, gesi ya tanuri la kuyeyusha chuma na tanuri linalozunguka zinatumiwa vizuri. Nishati hizo ni sawa na kigezo cha makaa ya mawe tani milioni 1.56 kwa mwaka, na ni sawa na uzalishaji wa mwaka mmoja wa godi kubwa la makaa ya mawe. Kampuni hiyo inapopunguza matumizi ya maliasili, pia imehifadhi mazingira. Moshi na vumbi zilizotolewa katika mwaka 2004 zilipungua kwa asilimia 78 zikilinganishwa na mwaka 1999, na maji machafu yalipungua kwa asilimia 68%. Kampuni hiyo kimeanza kuwa kiwanda kinachofanana na bustani.

Kubana matumizi ya maliasili na kuongeza mapato ni kanuni ya kimsingi ya uchumi unaopata maendeleo endelevu. Kampuni ya chuma na chuma cha pua ya Taiyuan kimeweka shabaha mpya, yaani kubana tena matumizi ya nishati hadi kufikia kigezo cha makaa ya mawe kilo 680 ndani ya miaka mitatu, ili kufikia au kukaribia kiwango cha juu duniani; kubana matumizi ya maji hadi kufikia tani 3.8; kufanya kigezo cha ujumla cha matumizi ya nishati katika sehemu muhimu za uzalishaji kifikie au kukaribia kiwango cha juu duniani; kutotoa vitu vinavyoleta uchafuzi na maji machafu; kupunguza hewa chafu kwa asilimia 80 ili kufikia kigezo cha pili cha hewa, na kujenga kiwanda kisichosababisha uchafuzi cha kiwango cha juu duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-25