Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-25 21:32:06    
Bustani ya Kisayansi ya Fengtai

cri

Muda si mrefu uliopita, waandishi wa habari na wataalamu kutoka nchi mbalimbali wa Radio China Kimataifa walitembelea Bustani ya Fengtai ya Eneo la kisayansi ya teknolojia la Zhongguancun (Z-Park), kujionea wenyewe maendeleo ya kasi ya kisayansi na teknolojia yaliyopatikana nchini China. Leo tunawaletea maelezo kuhusu Bustani ya Kisayansi ya Fengtai.

Mhusika wa kamati ya usimamizi ya Eneo la Zhongguancun Bwana Gai Yuyun anasema:

"Hivi sasa Eneo la Zhonguancun limeendelezwa kuwa na sehemu moja na bustani saba, kutoka mtaa mmoja wa kuuzia bidhaa za elektroniki zamani, ambapo Bustani ya Kisayansi ya Fengtai ni sehemu yenye uhai mkubwa wa uvumbuzi katika kusini ya mji wa Beijing, itakuwa moja ya sehemu muhimu za maendeleo ya kimkakati ya Eneo la Z-Park siku zijazo."

Bustani ya Fengtai ni sehemu moja ya bustani 7 za Eneo la Z-Park , ilianzishwa mwaka 1991, eneo lake ni kilomita tano za mraba. Mwaka 1997 kituo cha uvumbuzi wa kisayansi cha Fengtai kilisifiwa kuwa "kiangulio cha kimataifa cha mashirika madogo" na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa. Mwaka 2003, bustani hiyo ilithibitishwa kuwa kituo cha majaribio cha "uchumi wa makao makuu" cha Beijing.

Waandishi wa habari wa China na wa ng'ambo walipotembelea Bustani ya Kisayansi ya Fengtai, mambo yaliyowavutia zaidi ni "uchumi wa makao makuu" na "kiangulio cha mashirika".

"Uchumi wa makao makuu" ni matokeo ya kiuchumi ya kutenganisha makao makuu ya mashirika na karakana zake za uzalishaji. Katika miaka ya karibuni, Bustani ya Fengtai imeanzisha kwa mafanikio "bustani ya kibiashara ya kisasa" (Advanced Business Park), ambayo ni ya kwanza nchini China. Hivi sasa bustani hiyo imeshajenga majengo 170 ya makao makuu, na imetia saini na kampuni kubwa zaidi ya 100.

Kampuni ya teknolojia ya nishati ya Zhonglian ya Beijing inayoshughulikia nishati zisizokuwa na vitu vya uchafuzi, ni moja ya kampuni zilizoweka makao makuu yao kwenye bustani hiyo. Mhusika wa kampuni hiyo anasema:

"Mazingira ya Bustani ya Kisayansi ya Fengtai ni mazuri sana, baada ya kuingia hapa sifa ya kampuni yetu imeinuka, na thamani ya mikataba imeongezeka kwa kiwango kikubwa. Pia tunaweza kupata huduma bora, na kupewa sera ya kipaumbele, na kupunguziwa gharama za uendeshaji."

"Kiangulio" tutakachozungumzia leo si kiangulio cha kawaida cha kuyaangua vifaranga, bali ni "kiangulio" cha kuangua mashirika madogo na ya wastani ili yaweze kujiendeleza kwa haraka. Kituo cha Kiangulio cha Mashirika cha Kimataifa cha Beijing (IBI) sasa kinaangua mashirika madogo zaidi ya 1000 yaliyotoa nafasi za ajira kwa watu zaidi ya 10,000. Kati ya mashirika hayo madogo, mashirika zaidi ya 40 yalianzishwa na wanafunzi wa China waliomaliza masomo nchi za nje na kurudi nchini China kuendesha biashara zao. Mhusika wa kituo hicho alijulisha kuwa:

"Umaalum mkubwa wa kituo chetu ni kuyachukua majengo yasiyotumika au mahoteli yenye ufanisi mdogo na kuyakodisha majengo yake kwa mashirika madogo yenye uvumbuzi na miradi ya teknolojia ya hali ya juu, yasiyo na uzoefu na mitaji ya kuendesha shughuli zao yenyewe."

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mhusika huyo, "Kiangulio" hicho kinaweza kuyavutia mashirika mengi namna hii, kutokana na huduma bora, bei rahisi za kukodisha ofisi na kuwa na miundo mbinu ya kutosha kuendesha shughuli zao. Kituo cha "Kiangulio" kinayapatia huduma mashirika hayo hasa katika maeneo yafuatayo: kuyafundisha mashirika madogo jinsi ya kuendesha shughuli zao, kuyatafutia maabara za utafiti, mitaji, upashanaji habari na kuyasaidia kufanya shughuli mbalimbali za usajili. Kwa mfano, kampuni ndogo zilipoanzisha shughuli zao hukosa mitaji, "Kiangulio" huzisaidia kukusanya mitaji kutokana na uaminifu wake na uhusiano wake mzuri na vyombo vya fedha.

Bustani ya Kisayansi ya Fengtai inatilia maanani sana uvumbuzi wa kisayansi, sasa imekuwa na mashirika mengi yenye uwakilishi katika maeneo ya upashanaji habari, dawa za viumbe, mitambo ya kisasa na malighafi mpya, na miradi mingine yenye teknolojia ya hali ya juu. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi ya bustani hiyo Bwana Fu Xurjiang anasema:

"Hadi mwishoni mwa mwaka 2004, mashirika yaliyoko kwenye Bustani ya Fengtai yalikuwa na miradi zaidi ya 2000 ya teknolojia ya hali ya juu, kati hiyo, miradi 68 ilipewa sifa ya uvumbuzi wa kisayansi. Mwaka 2004, kwa jumla miradi 178 yenye teknolojia ya hali ya juu ya mashirika ya bustani hiyo yalithibitishwa, ambapo miradi 247 iliomba hakimiliki ya kitaifa."

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2004, mashirika zaidi ya 2700 yaliingia kwenye Bustani ya Kisayansi ya Fengtai, ambayo yalitimiza uzalishaji mali yuan zaidi ya bilioni 120, na kulipa kodi ya Yuan bilioni 3.7, imekuwa nguvu kubwa ya maendeleo ya uchumi ya wilaya ya Fengtai.

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-25