Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-26 21:36:22    
China itatimiza hali ya kuwepo kwa uwiano kati ya mahitaji na utoaji wa maji kabla ya mwaka 2015 kwa njia ya kutunza maji tu

cri

Mkuu wa taasisi ya usimamizi wa kiuchumi ya chuo kikuu cha safari za ndege na za anga ya juu cha Beijing, ambaye pia ni mkuu wa kamati ya kuhimiza uchumi wa mzunguko ya Beijing Profesa Wu Jisong katika kitabu chake "uchumi wa mpya wa mzunguko", ameandika kuwa, "China itatimiza hali ya kuwepo kwa uwiano kati ya mahitaji na utoaji wa maji kabla ya mwaka 2015 kwa njia ya kutunza maji." Kauli hiyo imetoa "ufumbuzi" wa suala la upungufu wa maji nchini China.

Hivi sasa, kwa kawaida China ina upungufu wa maji kwa mita za ujazo bilioni 40 kwa mwaka. Baada ya kuchunguza mwelekeo wa matumizi ya maji katika miaka ya hivi karibuni, Profesa Wu aligundua kuwa, ingawa pato la jumla la taifa la China limeongezeka kwa asilimia 8 kila mwaka katika miaka 7 iliyopita, lakini kiasi cha matumizi ya maji kinapungua kwa asilimia 0.45 kila mwaka; idadi ya watu ya China imeongezeka kwa asilimia 0.74 na kiasi cha matumizi ya maji kwa kila mtu kinapungua kwa asilimia 1.18 kila mwaka. Profesa Wu alisema kuwa, "hali hiyo ni mafanikio ya marekebisho ya miundo ya sekta na kazi ya kutunza maji."

"njia muhimu ya kutatua upungufu wa maji ni kutekeleza uchumi wa mzunguko na kujenga jamii yenye kutunza raslimali." Profesa Wu anaona kuwa, kama kazi ya kutunza maji ikiimarishwa zaidi, lengo la pato la jumla la taifa kuongezeka maradufu bila ya kuongeza matumizi ya maji ifikapo mwaka 2010 litaweza kutimizwa. Baada ya mwaka 2010, ufanisi wa kutunza maji kutokana na marekebisho ya miundo ya uchumi huenda utapungua, lakini serikali ya China ikiwekeza zaidi katika kazi hiyo na teknolojia husika, ufanisi wa matumizi ya maji utaweza kuinuliwa, na hali hiyo itasaidia kudhibiti kiasi cha jumla cha matumizi ya maji kwa msingi wa kutosheleza maendeleo ya uchumi wa China. Profesa Wu alisema "lazima tudhamirie kabisa, na kuchukua hatua za kisera na kimfumo, ili kuhakikisha lengo la kutunza maji linatimizwa."

Profesa Wu aliainisha kuwa, kutunza maji ya matumizi ya kilimo hasa ni kuinua ufanisi wa umwagiliaji maji mashambani. Hivi sasa kiasi cha ufanisi huo ni 0.43, na kiasi hicho ni 0.7 hadi 0.8 katika nchi zilizoendelea, kama kiasi hicho cha China kikiweza kufikia 0.6, maji yenye mita za ujazo zaidi ya bilioni 49.4 yanaweza kutunzwa. Kutunza maji ya matumizi ya viwanda hasa ni kuinua ufanisi wa marudio ya matumizi ya maji na kueneza teknolojia za kutunza maji. Mwaka 2002, kiasi cha ufanisi wa marudio ya matumizi ya maji kilikuwa ni asilimia 50, ikiwa ni chini sana kuliko asilimia 80 katika nchi zilizoendelea. Kama ufanisi huo ukiweza kuinuliwa kufikia asilimia 60, uwezo wa kutunza maji utaweza kuongezeka kwa mita za ujazo bilioni 16 kwa mwaka; njia muhimu za kutunza maji ya matumizi ya maisha mijini ni kupunguza kiasi cha maji yanayovuja kutoka kwenye mabomba na kupandisha bei ya maji.

Profesa Wu alisema "kujenga jamii yenye kutunza maji, pia kunahitaji kuvumbua na kujenga mfumo wa kutunza maji, uchumi wa kutunza maji, teknolojia za kutunza maji na utamaduni wa kutunza maji. Kama hatua hizo zikichukuliwa, mahitaji na utoaji wa maji nchini China utafikia hali ya uwiano ifikapo mwaka 2015."

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-26