Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-27 20:38:52    
China yafurahishwa na mustakabali wa ushirikiano wa ACO

cri
    Mkutano wa nne wa mawaziri wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi wa Asia ya Shanghai, ACO, ulifanyika tarehe 26 mjini Moscow. Mkutano huo ulikuwa na majadiliano na kufikia makubaliano kuhusu utekelezaji wa azimio la mkutano wa viongozi wa nchi wa Astana wa ACO uliofanyika mwezi Julai mwaka huu na kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya uchumi na utamaduni. Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alitoa hotuba kwenye mkutano huo akieleza maoni ya China kuhusu kuimarishwa kwa ushirikiano wa uchumi na utamaduni wa ACO na kutoa mapendekezo na hatua kamili zinazochukuliwa. Alisema kuwa China inafurahishwa na mustakabali wa ushirikiano wa ACO.

    Viongozi walioshiriki kwenye mkutano huo ni pamoja na waziri mkuu wa Kazakhstan Bw. Danial Akhmetov, waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao, waziri mkuu wa Kyrgyzstan, waziri mkuu wa Russia Bw. Mikhail Fradkov, waziri mkuu wa Tajikistan Bw. Akil Akilov na naibu waziri mkuu wa Uzbekistan Bw. Utkur Sultanov. Viongozi wa nchi nyingine walioshiriki kwenye mkutano huo wakiwa kama wachunguzi ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje wa India Bw. Natwar Singh, makamu wa kwanza wa rais wa Iran Bw. Parviz Davoodi, waziri mkuu wa Mongolia Bw. Tsakhia Elbegdorj na waziri mkuu wa Pakistan Bw. Shaukat Aziz.

    Kutokana na majukumu yaliyothibitishwa kwenye mkutano wa viongozi wa serikali wa Astana wa ACO uliofanyika tarehe 5 mwezi Julai, viongozi wa nchi walioshiriki kwenye mkutano walijadili masuala mengi kuhusu kulinda hali ya utulivu, uchumi na biashara, teknolojia ya kisayansi, utamaduni na masuala mengine yanayofuatiliwa na watu. Waziri mkuu wa Russia Bw. Mikhail Fradkov kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mkutano huo kumalizika alisema kuwa, mkutano huo ulijadili masuala mengi. Licha ya kuweko masuala kuhusu uchumi na biashara, pia mazungumzo yalihusu namna ya kukabiliana na changamoto zinazoletwa na ugaidi, watu wenye siasa kali, mihadarati pamoja na masuala mengine kuhusu mila, utamaduni na elimu. Alisema, "Washiriki wa mkutano wanaona kuwa katika muda wa miaka karibu mitano iliyopita, ACO ilifanya kazi nyingi, lakini bado kuna kazi nyingi katika siku za baadaye. Tutatumia vilivyo raslimali kubwa za asili, uchumi na mali za watu zaidi ya bilioni 3, kuinua kiwango cha maisha ya watu wa sehemu hiyo na kufanya kazi muhimu katika shughuli za kiuchumi na kisiasa duniani."

  

    Kutokana na taarifa ya pamoja iliyotolewa na mkutano huo, mawaziri wakuu hao wameamua kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na kuboresha mazingira ya uwekezaji juu ya msingi wa kanuni za kunufaishana na usawa. Wanaona kuwa idara husika za nchi wanachama wa jumuiya hiyo zinatakiwa kutekeleza ipasavyo mipango kwa msingi wa mapendekezo yaliyotolewa na mkutano wa mawaziri wa uchumi na biashara wa Bishkek uliofanyika mwezi Februari mwaka huu, kuhusu miradi ya majaribio ya nishati, mawasiliano, upashanaji habari, sayansi, tekinolojia na kilimo.

    Waziri mkuu wa China Bw. Wen Jiabao alitoa hotuba kwenye mkutano huo akieleza maoni ya China kuhusu kuimarisha ushirikiano wa nchi wanachama wa ACO. Alisema kuwa sasa mwongozo wa ushirikiano umethibitishwa, kitu muhimu kwa hivi sasa ni utekelezaji, ushirikiano wa mambo ya uchumi na usalama ni vitu viwili muhimu. Katika ushirikiano wa uchumi, tunatakiwa kuimarisha kuoanisha sera, kuzidisha uwekezaji katika maeneo mbalimbali, kuharakisha utekelezaji wa mambo mbalimbali na kufanikisha makubaliano tuliyofikia. Alisema kuwa China inapenda kufanya juhudi kadiri i iwezavyo kuimarisha ushirikiano wa ACO. Alisema, "Mwaka huu tumeahidi kutoa mafunzo kwa watu 1,500 wenye ujuzi maalumu kwa ajili ya nchi wanachama wa APEC katika miaka 3 ijayo, mafunzo hayo yatagharimu Yuan za Renminbi milioni 75, na tutatoa mikopo nafuu ya dola za kimarekani milioni 900 ya miaka 20 kwa riba ya 2% kwa nchi zinazonunua bidhaa za China zinazosafirishwa kwa nchi za nje."

  

    Alipogusia matatizo yaliyoko hivi sasa katika ushirikiano wa uchumi wa ACO, alisema kuwa "mkataba wa ushirikiano wa benki za ACO" na "kumbukumbu ya mkutano wa kwanza wa kamati ya wanaviwanda ya ACO" za mkutano huo zinalenga matatizo hayo.

Idhaa ya Kiswahili