Mlipuko wa mabomu ya kujiua ulitokea tarehe 26 huko Hadera, nchini Israel, na kusababisha vifo vya watu watano na watu kumi kadhaa kujeruhiwa. Huu ni mlipuko wa kwanza wa mabomu ya kujiua kutokea nchini Israel baada ya Israel kuondoka kutoka Gaza mwezi Septemba.
Mji wa Hadera uko kando ya bahari ya Mediterranean, kaskazini magharibi mwa Israel. Kwa kuwa mji huo uko karibu na mstari wa kusimamisha vita vya mwaka 1967, unashambuliwa mara kwa mara toka migogoro ya kimabavu kati ya Paletina na Israel uanze mwaka 2000. Mlipuko huo ulitokea kwenye soko la wazi mjini Hadera. Tarehe 26 alasiri saa tisa na nusu, watu wengi walikuwa wananunu mahitaji kwenye soko hilo. Ghafla, Mpalestina mmoja alilipua mabomu kilogramu 10 za mabomu alyokuwa ameficha mwilini mwake, vibanda vilivyokuwa karibu naye vilibomolewa, watu watano walikufa katika mlipuko huo, na wengine kumi kadhaa walijeruhiwa. Baadaye, polisi walifunga barabara zote mjini na barabara ya kasi iliyokaribu na soko hilo. Habari kutoka kituo cha redio cha Israel zilisema kuwa, baada ya mlipuko, watuhumiwa wawili waliondoka haraka na gari moja jeupe, hivi sasa polisi inalisaka gari hilo.
Baadaye, kundi la Islamic Jihad lilitangaza kuwajibika na tukio hilo, na kusema kuwa, mashambulizi hayo ni kulipiza kisasi dhidi ya kikundi cha Israel cha kumwua kiongozi mmoja wa kundi hilo siku chache zilizopita kwenye kando ya magharibi ya Mto Jordan.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas tarehe 26 alitoa taarifa kulaani mlipuko huo. Taarifa hiyo ilisema kuwa, mashambulizi hayo yamehatarisha maslahi ya raia wa Palestina na pengine yatachochea migongano ya kimabavu kati ya Palestina na Israel. Jambo linalopaswa kutajwa ni kuwa, kabla ya mlipuko huo kutokea saa chache zilizopita, Bw. Abbas alitoa hotuba kuvitaka vikundi mbalimbali vya Palestina vitekeleze makubaliano ya Cairo ya kusitisha vita dhidi ya Israel, ili kudumisha utulivu kati ya pande hizo mbili. Alishutumu vikali vitendo vya wanamgambo wa Palestina vya kurusha roketi dhidi ya Israel, alisema kuwa, vitendo hivyo vitasababisha tu mashambulizi ya Israel, hivi sasa raia wa Palestina wanahitaji kuboresha uchumi.
Serikali ya Israel siku hiyo iliilaani Palestina kushindwa kudhibiti wanamgambo wake, na kuitaka Palestina ichukue hatua haraka, kuvivunja vikundi hivyo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Koffi Annan siku hiyo alitoa taarifa kuzitaka Palestina na Israel zijizuie, ili kuepusha kuongezeka kwa mapambano. Taarifa imesisitiza kuwa, njia pekee ya kutatua migogoro kati ya Israel na Palestia ni kufanya mazungumzo.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bw. Scott McClellan siku hiyo alisema kuwa, tukio hilo limeshusha heshima ya uongozi wa Bw. Mahmoud Abbas. Pia aliihimiza Mamlaka ya Utawala wa Palestina ichukue hatua kali zaidi, ili kuzuia mashambulizi yanayofanywa na vikundi vya Palestina.
Baada ya Israel kuondoka kutoka Gaza mwezi Septemba, hali kati ya Israel na Palestina haikuelekea kuwa ya utulivu kama watu walivyotarajia. Kinyume na matarajio, migogoro kati ya pande hizo mbili ilitokea mara kwa mara. Makubaliano ya kusimamisha vita yaliyofikiwa kati ya Palestina na Israel mwezi Februari mwaka huu karibu yamevunjika. Israel baada ya kuondoka kutoka Gaza bado haijafungua njia mpakani mwa Gaza, na kukwamisha uchumi ya sehemu hiyo.
Mlipuko wa kujiua uliotokea tarehe 26 umeongeza hali mbaya ya uhusiano ulio dhaifu kati ya Palestina na Israel. Mkutano kati ya mwenyekiti wa Mamlaka ya Utawala wa Palestina Bw. Mahmoud Abbas na waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon uliopangwa kufanyika hivi karibuni sasa haujulikani kama utafanyika.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-27
|