Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-28 20:03:10    
Ndege za Israeli zashambulia sehemu ya Gaza

cri
    Jeshi la anga la Israeli tarehe 27 usiku lilishambulia kambi ya wakimbizi iliyoko sehemu ya kaskazini ya Gaza, na kuwaua wapalestina 7 wakiwemo maofisa wa ngazi ya juu wa chama cha Islamic Jihad cha Palestina. Hiki ni kitendo cha Israel cha kulipiza kisasi dhidi ya shambulizi la bomu la kujiua lililotokea kwenye mji wa Hadera tarehe 26.

    Kutokana na hayo, mazungumzo yaliyopangwa kufanyika hivi karibuni kati ya waziri mkuu wa Israeli Bw. Ariel Sharon na mwenyekiti wa mamlaka ya taifa ya Palestina Bw. Mahomood Abbas yameahirishwa. Makubaliano ya kusimamisha mapambano yaliyoafikiwa mwezi Februari mwaka huu yanakabiliwa na changamoto.

    Watu walioshuhudia mashambulizi hayo walisema kuwa kombora lililofyatuliwa na ndege ya kivita isiyo na rubani lilipiga gari moja lililokuwa likitembea ndani ya kambi ya wakimbizi, ofisa wa ngazi ya juu wa kundi la Islamic Jihad pamoja na msaidizi wake waliokuwa ndani ya gari waliuawa. Mlipuko pia uliwaathiri wapalestina kadhaa waliokuwa wakitoka nyumbani mwao katika mwezi wa Ramadhani, watu 5 walikufa akiwemo mtoto mmoja wa kiume mwenye umri wa miaka 15. Taarifa iliyotolewa na jeshi la Israel ilitangaza kuwajibika na shambulizi hilo la kijeshi la "Zoezi la Usalama" dhidi ya maofisa wa ngazi ya juu wa kundi la Islamic Jihad. Jeshi la Israel lilimlaani ofisa huyo wa Jihad ambaye aliongoza kazi ya kurusha makombora kwa sehemu ya kusini ya Israel, kwa kupuuza makubaliano ya kusimamisha mapambano yaliyotiwa saini kati ya Palestina na Israel.

    Msemaji wa chama cha Islamic Jihad alitoa taarifa siku hiyo akisema kuwa kundi lake litalipiza kisasi haraka dhidi ya vitendo vya kijeshi vya Israel, wakati kiongozi wa Al-Aqsa Martyrs Brigade alitangaza huko Gaza kuwa kundi lake halitatekeleza tena makubaliano ya kusimamisha mapambano kati yake na Israel.

    Baada ya mji wa Hadera wa Israel kushambuliwa kwa bomu la kujiua, serikali ya Israel iliamua kuanzisha zoezi la kijeshi dhidi ya sehemu inayosimamiwa na Palestina. Mbali na kufanya mashambulizi ya ndege, jeshi la Israel lilimkamata ofisa mmoja wa cheo cha juu wa kundi la Islamic Jihad kwenye mji wa Jenin ulioko kando ya magharibi ya mto Jordan. Jeshi la Israel lilidokeza kuwa safari hii wanalichukulia kundi la Islamic Jihad kuwa shabaha ya zoezi hilo la kijeshi, hususan kwenye sehemu mbili za kaskazini ya Gaza ambapo kuna ngome ya maroketi ya Qassam ya wapalestina, na sehemu nyingine ambayo ni pamoja na miji ya Jenin na Tul Karm pamoja na baadhi ya vijiji vya karibu vilivyoko kando ya magharibi ya mto Jordan na kuwasaka wanachama wa kundi la Jihad. Aidha jeshi la Israel limetekeleza utawala wa kijeshi kwenye kando ya magharibi ya mto Jordan na kufunga njia zote zinazoelekeza kwenye eneo linalodhibitiwa na Palestina.

    Waziri mkuu wa Israel Bw. Sharon tarehe 27 alitangaza kuwa zoezi la kijeshi la Israeli litakuwa la pande zote na la kudumu mpaka wanamgambo wa Palestina waache kabisa "vitendo vya kigaidi". Alisema kuwa katika hali ya namna hiyo hawezi kuwa na mazungumzo na mwenyekiti wa mamlaka ya Palestina Bw. Mahmood Abbas isipokuwa atachukua hatua kali dhidi ya makundi ya kijeshi, la sivyo mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel hautapata maendeleo. Bw. Sharon na Bw. Abas wangekuwa na mazungumzo katikati ya mwezi huu ili kujadili namna ya kuhimiza mchakato wa amani baada ya Israel kukamilisha mpango wa upande mmoja wa kuondoka. Mwanzoni mwa mwezi huu, pande hizo mbili zilishindwa kuafikiana kuhusu baadhi ya maswala muhimu, hivyo ziliamua kuahirisha mazungumzo hadi mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi Novemba.

    Waziri mkuu wa serikali ya Palestina Bw. Ahmed Qureia tarehe 27 alisema kuwa hatua kali zilizochukuliwa na Israel dhidi ya shambulizi la bomu la kujiua lililotokea huko Hadera litazidisha mgogoro uliopo kati ya Palestina na Israel. Rais Hosni Mubarak wa Misri siku hiyo alipohojiwa na vyombo vya habari vya Israel alisema kuwa Israeli inamhitaji Abbas, hivyo inapaswa kuchukua hatua halisi kumsaidia Abbas kuimarisha hadhi yake miongoni mwa watu wa Palestina. Aliongeza kuwa Israel kuchukulia kuyanyang'anya silaha makundi ya kijeshi yenye siasa kali kuwa ni sharti la kwanza la kuhimiza mchakato wa amani, ni hatua ambayo itasababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Palestina.

Idhaa ya Kiswahili