Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-10-31 15:52:30    
Tamasha la utamaduni wa China lakaribishwa nchini Marekani

cri

Tamasha la utamaduni wa China lilianza tarehe mosi Oktoba na litafanyika kwa mwezi mmoja nchini Marekani. Katika tamasha hilo kuna michezo ya sanaa ya aina mbalimbali kama vile muziki wa symphony, bale, muziki wa Kichina, opera za Kichina, sarakasi na maonesho ya picha, mavazi na vitu vya sanaa. Tamasha hilo limewavutia sana watazamaji wa Marekani, ambao wanaona kuwa tamasha hilo limewaletea nafasi nzuri ya kuufahamu utamaduni wa China. Kwenye maonesho ya muziki ya kundi la symphony la Guangzhou, muziki huo wa "Die Lian Hua" (Kipepeo Chapenda Maua) umeonesha vilivyo hisia za wanawake za upendo, upole, haya, wivu na machachari kwa kutumia ala za muziki za Kichina na za Kimagharibi. Katika sehemu ya pili ya maonesho hayo, muziki wa piano wa "Mto Huanghe" ulioshirikiana na okistra na uliopigwa na mpigaji mashuhuri wa peano Lang Lang ulishangiliwa kwa muda mrefu. Bw. Don Wallace alistaajabu sana kwa kusikiamchanganyiko mzuri wa muziki wa jadi wa Kichina na wa Kimagharibi. Alisema, "Ni jambo la kufurahisha kuufahamu muziki wa kichina kwa kusikiliza. Muziki wa "Mto Huanghe" ni mzuri kweli, sijawahi kusikiliza muziki mzuri kama huo, nitatafuta data nifahamu mtunzi wa muziki huo."

Alisema, amewahi kusikia kuhusu mto Huanghe, lakini hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kusikiliza muziki kuhusu mto huo. Anaona kuwa muziki huo una nguvu kubwa ya kutetemesha kama mto wa Huanghe, alifahamu ushupavu wa wachina kwa kusikiliza muziki huo. Alishukuru kwa tamasha hilo ambalo limewaletea muziki mzuri kama huo.

Mmarekani mmoja mzee mwenye asili ya China ambaye ameishi nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 30, alisisimka na kutokwa na machozi baada ya kusikiliza muziki wa Mto Huanghe. Alisema, "Ni jambo la maana sana kuwajulisha watu wa Marekani muziki kama huo, kwa sababu uvumi wa "tishio la China" unaenea sana nchini humo, maingiliano ya utamaduni yanaweza kuwasaidia sana watu wa Marekani kufahamu China ilivyo, kutoifahamu China kunaweza kusababisha migogoro ambayo italeta hasara kwa watu wa nchi zote mbili. Naona furaha kwa China kufanya tamasha hilo."

Bw. Triplett alikwenda kwenye maonesho ya muziki pamoja na familia yake. Alisema, ingawa mtoto wake bado mdogo, lakini anapenda kumpatia nafasi ya kusikiliza muziki wa Kichina na kuona ala za muziki za Kichina. Alisema, "Muziki wa Kichina ni tofauti kabisa na muziki wa Marekani, muziki tuliousikia ulinifanya nijisikie niko kwenye mazingira ya dunia nyingine."

Katika tamasha hilo, pia kuna maonesho ya aina nane ya yanayoielezea China. Katika jumba la maonesho la kituo cha michezo ya sanaa cha Kennedy watazamaji wengi walisimama mbele ya maonesho ya "Mvutio wa Beijing" wakiangalia picha za zinazoonesha mji wa Beijing wa kale na wa sasa. Kwenye jumba la ghorofa zilioneshwa sanamu kadhaa za kiasili za askari na farasi zilizofukuliwa kutoka kaburi la mfalme wa Enzi ya Qin, na mavazi ya fasheni na mapambo ya vito. Wkulikuwa na watazamaji ambao walikuwa wakitoka na kuingia.

Meneja mkuu wa Kampuni ya Nishati ya GHK Bw. Robert Hefner na mkewe walivutiwa sana mapambo ya vito yaliyotengenezwa kwa mtindo wa Kichina. Alisema, "Napenda sana vitu vya Kichina, na mke wangu anapenda kuvaa mapambo ya vito ya Kichina. Maonesho haya yanatuvutia kweli."

Mke wa Bw.Hefner alisema, "Maonesho yananivutia kwa sababu mavazi yana mchanganyiko wa mtindo wa Kichina na za Kimagharibi, na kitambaa kinachotumika kimekuwa kizuri kuliko zamani."

Sanamu zilizochongwa na wasanii tisa wa China zilizowekwa mbele ya jengo la kituo cha michezo ya sanaa pia zilivutia watazamaji wengi, ambao walipiga piga mbele ya sanamu hizo. Naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Uchoraji cha China Bw. Fan Di'an alisema, "Sanamu hizo zikiwa mbele ya kituo cha michezo ya sanaa zimeleta mazingira ya mchangnyiko wa utamaduni wa Kimashariki na Kimagharibi, ingawa maonesho hayo sio makubwa lakini yanawavutia watazamaji kupiga picha kwa ajili ya kumbukumbu."

Aliongeza kuwa meneja mkuu na naibu wake kituo cha michezo ya sanaa pia walisema kuwa, wanapenda sana sanamu hizo za uchongaji, kwa sababu zinaashiria kuwa kituo hicho kinafanya tamasha la utamaduni wa China na zimeleta mazingira ya utamaduni wa China.

Rais wa bodi ya wakurugenzi ya Kamati ya Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Chen Xiangmei pia alisifu sana sanamu hizo, alisema, "Sanaa haina mpaka, ni ya dunia nzima, katika miaka 10 iliyopita, pengine China isingefanya maonesho hayo lakini sasa imepiga hatua. Tumeelewana zaidi na kushirikiana zaidi, kwa hiyo naona tamasha hilo ni muhimu, na sote tunalifurahia."

Idhaa ya Kiswahili 2005-10-31