Katibu mkuu wa kamati kuu ya chama cha kikomunsiti cha China ambaye pia ni rais wa China Hu Jintao alifanya ziara rasmi ya kirafiki nchini Korea ya kaskazini kuanzia tarehe 28 hadi 30 Oktoba kutokana na mwaliko wa katibu mkuu wa chama cha reba cha Korea ya kaskazini ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kamati ya ulinzi wa taifa Bwana Kim Jon Il.
Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 30 hapa Beijing, mkuu wa idara ya mawasiliano na nje ya kamati kuu ya chama Bwana Wang Jiarei alisema kuwa, ziara hiyo ya Hu Jintao ilipata mafanikio makubwa na kufikia lengo la kuimarisha urafiki wa jami kati ya China na Korea ya kaskazini, kuongeza uaminifu na kupanua ushirikiano wa kunufaishana, ziara hiyo ina umuhimu mkubwa kwa kuimarisha ujirani mwema na urafiki kati ya China na Korea ya kaskazini na kuhimiza amani na maendeleo ya sehemu ziliko nchi hizo mbili hata dunia nzima.
Bwana Wang alifahamisha kuwa, katika ziara yake hiyo, rais Hu Jintao na viongozi muhimu wa Korea ya kaskazini walibadilishana maoni kwa kina juu ya uhusiano kati ya vyama viwili na nchi mbili, suala la nyuklia la peninsula ya Korea pamoja na masuala ya kimataifa na kikanda yanayozihusu, wamepata maoni ya pamoja juu ya masua mengi. Bwana Wang alisema:
Katika ziara yake hiyo, viongozi wakuu wa vyama viwili na nchi mbili za China na Korea ya kaskazini wameelekeza zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya China na Korea ya kaskazini. Aidha pande hizo mbili zimesisitiza kuwa zitaendelea kusukuma mbele mazungumzo ya kutatua kiamani suala la nyuklia la peninsula ya Koreaa. Zaidi ya hayo pande hizo mbili zimesisitiza kuwa zitahimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Korea ya kaskazini, aidha kila upande wa pande hizo mbili umesifu sana mafanikio ya ujenzi uliyopata upande mwingine.
Ziara hiyo ya rais Hu Jintao ilifanyika baada ya kupata matokeo ya kipindi katika duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 kuhusu suala la nyuklia la peninsula ya Korea na kabla ya kuanzishwa kwa duru jipya la mazungumzo hayo. Bwana Wang alisema:
Suala la nyuklia la peninsula ya Korea na mazungumzo ya pande 6 yalikuwa masuala muhimu waliyozungumzia katibu mkuu Hu Jintao na katibu mkuu Kim Jon-Il. Viongozi hao wawili wameona kwa kauli moja kuwa, duru la 4 la mazungumzo ya pande 6 limepata matokeo yenye juhudi, taarifa ya pamoja ni maoni ya pamoja yaliyofikiwa kati ya pande mbalimbali, hivyo lazima kuitekeleza; na katibu mkuu Kim Jong-Il ameahidi kuwa Korea ya Kaskazini itahudhuria duru la 5 la mazungumzo ya pande 6 kwa mpango uliowekwa, na itashirikiana pamoja na pande husika mbalimbali ili kusukuma mbele mchakato wa utatuzi wa kiamani wa suala la nyuklia la peninsula ya Korea . Tunaweza kuamini kuwa chini ya juhudi za pamoja duru la 5 la mazungumzo ya pande 6 yatakayofanyika kwa mpango uliowekwa yatapata matokeo kwa kuelekea kutatua kiamani suala la nyuklia la peninsula ya Korea. Alipozungumzia mustakbali wa ushirikiano wa kiuchumi na kiteknolojia kati ya China na Korea ya kaskazini, Bwana Wang alisema:
Viongozi wa nchi mbili za China na Korea ya kaskazini wameahidi kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Hivi sasa Korea ya kaskazini imepata maendeleo makubwa katika ujenzi wa kiuchumi na maisha ya wananchi, lakini bado inakabiliwa na taabu kadha wa kadha, China itatoa msaada kwa iwezavyo.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-31
|