Milipuko mitatu iliyotokea tarehe 29 huko New Delhi, mji mkuu wa India imesababisha vifo vya watu zaidi ya 59 pamoja na majeruhi 210. Serikali ya India ilitangaza kuwa matukio hayo ni mashambulizi ya kigaidi. Waziri wa mambo ya ndani ya India Bw. Shivraj Patil tarehe 30 alisema kuwa polisi imewakamata watuhimiwa 22 wanaohusika na matukio hayo, hivi sasa uchunguzi bado unaendelea.
Polisi wa New Delhi waliyazingira masoko yote yaliyotokea milipuko mara tu baada ya milipuko kutokea na kutaka kufunga maduka yote ya mjini, polisi walifanya msako usiku kucha kwenye hoteli, migahawa, vituo vya magari moshi na vituo vya mabasi vya karibu. Polisi walisema kuwa hivi sasa bado hawawezi kuthibitisha ni nani waliozusha matukio ya milipuko na hawakutaka kudokeza habari nyingi zaidi kuhusu upelelezi uliofanyika. Waziri wa mambo ya ndani wa India Bw. Shivraj Patil tarehe 30 usiku baada ya kushiriki kwenye mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri ulioitishwa na waziri mkuu Manmohan Singh alisema kuwa, hivi sasa uchunguzi unafanyika kwenye njia sahihi, polisi wamepata habari nyingi na watatangaza haraka pindi watakapopata ushahidi wa uhakika.
Kundi la watu wenye silaha linalojulikana kwa jina la "Inquilab" yaani mapinduzi, kilivipigia simu vyombo vya habari vya sehemu ya Kashimir inayosimamiwa na India kikidai kuhusika na milipuko mitatu iliyotolea mjini New Delhi. Habari zinasema kuwa kundi hilo lilianzishwa mwaka 1996 na halikufanya shughuli nyingi, lakini lina uhusiano mkubwa na chama kimoja cha kiislamu chenye siasa kali kinachojulikana kwa "Jeshi la Wakereketwa". Chama cha "Inquilab" kilisema kuwa lengo la mashambulizi hayo ni kutaka jeshi la usalama la India liondoke kabisa kutoka sehemu ya Kashimir inayodhibitiwa na India. Lakini siku hiyo polisi wa New Delhi walisema kuwa maneno yaliyosemwa na kundi hilo yanahitaji kuthibitishwa. Polisi walitangaza tarehe 30 kuwa mtu atakayetoa habari kuhusu matukio hayo atapata zawadi ya Rupia laki moja, ambazo ni sawa na dola za kimarekani elfu 2. Polisi imetangaza namba za simu za polisi kwa kutumia vyombo vya habari na ilisema kuwa itazuia siri kabisa kuhusu habari za mtu atakayetoa habari.
Vyombo vya habari vya India vimesema kuwa habari wanazopata polisi hivi sasa bado si kamili, hivyo bado hawawezi kupata mtu aliyepanga njama hiyo. Vyombo vya habari vingi vinasema kuwa chama cha kiislamu kinachojulikana kwa "Jeshi la Wakerekatwa" kinaelekea zaidi kuhusika na milipuko hiyo. Gazeti la "Indian Times" limechapisha makala ikisema kuwa "Jeshi la Wakerekatwa" linaelekea zaidi kuhusika na milipuko hiyo, kwa kuwa kiongozi mmoja wa chama hicho wa aliyekamatwa hivi karibuni alipofunguliwa mashitaka kwenye mahakama ya New Delhi alisema kuwa watalipiza kisasi dhidi ya serikali ya India. Gazeti la "The Express" la India lilisema kuwa wataalamu wanaopambana na magaidi na wachunguzi wa New Delhi wanashuku "Jeshi la Wakerekatwa" ambalo lina uhusiano mkubwa na kundi la"Al-qaeda"linadhaniwa zaidi kuhusika na milipuko hiyo. Kwani chama hicho kinafanya shughuli nyingi kwenye sehemu ya kaskazini ya India na kilifanya mashambulizi mengi ya kigaidi kwenye sehemu ya Kashimir inayodhibitiwa na India tokea mwaka 1989, na lengo lake ni kupigania uhuru wa sehemu ya Kashimir inayodhibitiwa na India. Serikali ya India pia imekilaani chama hicho kuhusika na milipuko iliyotokea mwezi Agosti mwaka 2003 mjini Bombay na shambulizi dhidi ya jengo la bunge la India lililotokea mwishoni mwa mwaka 2001.

Vyombo vya India pia vimesema kuwa kutokana na mbinu iliyotumika na nyakati za milipuko, milipuko hiyo inahusika na makundi ya kigaidi duniani. Polisi imethibitisha kuwa baruti iliyotumika katika milipuko ya New Delhi ni ya aina ya RDX, ambayo ni baruti ya kijeshi yenye nguvu kubwa inayopendwa kutumiwa na makundi ya magaidi.
Kuhusu nyakati milipuko, kwanza milipuko ilitokea kabla ya kuwadia kwa sikukuu kubwa ya jadi ya India ya "Taa" kwenye soko kubwa lenye watu wengi. Pili, siku hiyo wawakilishi wa India na Pakistan walianzisha mazungumzo kuhusu kufungua mpaka kwenye sehemu ya Kashimir. Hivyo lengo la magaidi ni kuharibu utulivu wa India na kuzuia nchi hizo mbili kufanya usuluhishi.
Idhaa ya Kiswahili 2005-10-31
|