Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-01 16:23:26    
China itaendeleza uzalishaji wa bidhaa maarufu

cri

Pamoja na maendeleo ya uchumi na biashara ya nje ya China, bidhaa zinazozalishwa nchini China zinachukua nafasi kubwa zaidi katika bidhaa zinazozalishwa duniani. Walakini kuhusu bidhaa za maarufu za China, ni wateja wa nchi za nje kufahamu aina chache tu. Hali hii inatazamiwa kubadilika katika miaka michache ijayo. Hivi sasa China imeharakisha hatua za uzalishaji wa bidhaa maarufu na kutarajia kuwa aina za bidhaa maarufu zinazozalishwa nchini China zitaongezeka zaidi katika soko la dunia.

Tangu kufanyika mageuzi sifa za China katika uchumi wa dunia zinaongezeka kwa mfululizo, lakini kutokana na kuwa kiwango cha jumla ya teknolojia ya viwanda ya China bado ni cha chini na kukosa teknolojia muhimu zenye haki-miliki za China yenyewe, bidhaa za viwanda vingi ni zenye faida ndogo; Faida vinayopata baadhi ya viwanda vya China ni ndogo za kazi za usindikaji, ambapo faida kubwa zimechukuliwa na viwanda maarufu vya nchi za nje. Mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa ubora wa bidhaa ya China Bw. Sun Po alisema kuwa, China ikitaka kufanikisha lengo la marekebisho ya muundo wa uchumi, kubadilisha mtindo wa ongezeko la uchumi na kupata maendeleo ya kasi na mwafaka ya uchumi, haina budi kuzalisha aina nyingi za bidhaa maarufu. Alisema,

"Tukitaka kushindana na kampuni za nchi za nje zinazozalisha bidhaa maarufu duniani, tunapaswa kuharakisha hatua za uvumbuzi wa teknolojia na kuharakisha uzalishaji wa bidhaa bora maarufu, ili tufikie kiwango chao kwa haraka. Kwa hiyo suala la bidhaa maarufu linahusiana na marekebisho ya muundo na mtindo wa ongezeko la uchumi kwa hivi sasa, na tena linahusika na maendeleo ya muda mrefu ya uchumi, ujenzi wa mambo ya kisasa na mustakabali wa taifa, na ni suala moja muhimu sana la kimkakati."

Kutokana na mkakati uliowekwa na serikali ya China wa kuendeleza uzalishaji wa bidhaa maarufu, China itahimiza viwanda kufanya ushirikiano na viwanda vya mikoa mingine na viwanda vya sekta nyingine nchini ili kuzalisha bidhaa bora zenye nguvu kubwa ya ushindani duniani. Aidha, tokea mwaka 2000 serikali ya China ilishawishi miundo ya wakala kuanzisha shughuli za tathmini kuhusu bidhaa maarufu za China. Katika miaka 5 iliyopita aina zaidi ya 160 za bidhaa zimewekwa kwenye orodha ya tathmini, na bidhaa aina zaidi ya 900 zimepata sifa ya bidhaa maarufu ya China. Viwanda vinavyozalisha bidhaa hizo bora viko katika mikoa karibu yote ya China.

Mkakati wa kuzalisha bidhaa maarufu unaotekelezwa hivi sasa nchini China, umepata ufanisi katika kuhimiza marekebisho ya muundo wa uchumi na mpango bora wa raslimali, kuhimiza raslimali zikusanyike katika viwanda bora na viwanda vinavyozalisha bidhaa maarufu na kuleta ubora na ufanisi wa ongezeko la uchumi. Matokeo ya uchunguzi mpya yaliyotangazwa na idara ya takwimu ya China yanaonesha kuwa bidhaa maarufu za China zinadumisha hadhi bora katika maeneo mengi, na zaidi ya 60% ya wakazi wa mijini wanapenda kununua bidhaa maarufu za China.

Mkakati wa kuzalisha bidhaa maarufu pia umehimiza marekebisho ya muundo wa uchumi na mpango mwafaka wa raslimali. Hivi sasa sehemu mbalimbali za China zinaharakisha kuimarisha viwanda na kuharakisha uzalishaji wa bidhaa za aina mpya zikizingatia uzalishaji wa bidhaa maarufu na viwanda vinavyozalisha bidhaa maarufu.

Mji wa Qingdao ulioko katika pwani ya mashariki ya China ni moja ya mikoa iliyoanza mapema zaidi kutekeleza mkakati wa kuzalisha bidhaa maarufu. Hadi hivi sasa Qingdao imekuwa na viwanda 22 na aina 44 za bidhaa ambazo zimepata sifa ya bidhaa bora za China. Naibu meya wa Qingdao Bw. Wu Jingjian anaona kuwa bidhaa maarufu hizo zimekuwa nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo ya uchumi wa mji. Alisema,

"Ninaona kuwa maendeleo ya kiwango cha bidhaa maarufu, viwanda maarufu na sekta maarufu ya uzalishaji-mali yamekuwa kigezo muhimu cha mji kuwa na uhamasa mkubwa au la katika mazingira ya uchumi wa soko huria. Wanaviwanda wa Qingdao pia wanatumia vilivyo nafasi ya ufunguaji wa masoko, kufanya kazi kwa makini na kuzalisha bidhaa bora, sasa wameleta maendeleo makubwa ya viwanda. Bidhaa maarufu na viwanda vikubwa vimekuwa nguvu kubwa inayoharakisha maendeleo ya uchumi wa mji wa Qingdao."

Katika harakati za uzalishaji wa bidhaa maarufu, viwanda vya Qingdao vinajitahidi kufanya uvumbuzi wa teknolojia na usimamizi na kujenga mfumo wa utafiti na uvumbuzi wenye ufanisi. Hivi sasa mji wa Qingdao umejenga vituo 10 vya uvumbuzi wa teknolojia vya ngazi ya taifa, ambavyo licha ya kuvumbua bidhaa za teknolojia ya kiwango cha juu kwa ajili ya viwanda vya mji huo, bali pia vimekabidhiwa jukumu kuhusu miradi ya teknolojia ya ngazi ya taifa. Kampuni ya Haier ambayo ilianzishwa mwaka 1984 na kuongoza sekta ya uzalishaji wa vyombo vya umeme vya majumbani kwa hivi sasa, katika miaka zaidi ya 20 iliyopita imekuwa kampuni kubwa ya kimataifa yenye sifa kubwa nchini na katika nchi za nje. Mwaka 2004, Thamani ya bidhaa za kampuni ya Haier ilifikia Yuan za Renminbi bilioni zaidi ya 60. Hivi karibuni katika matokeo ya uchunguzi yaliyotangazwa na gazeti la "Financial Times" la Uingereza kuhusu "aina kumi za bidhaa za China zilizofikia ngazi ya kimataifa" kampuni ya Haier inachukua nafasi ya kwanza. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Haier Bibi Yang Mianmian alipozungumzia hali ya kampuni hiyo kuzalisha bidhaa bora maarufu alisema,

" Kuwa na chapa maarufu ni kuwa na kundi la bidhaa maarufu zinazofahamika kwa watu, tunataka kufanya chapa ya Haier kuwa chapa yenye hataza zetu wenyewe. Tunatakiwa kushikilia mambo mawili: La kwanza ni hakimiliki yetu wenyewe, na lingine ni uvumbuzi wa masoko."

Mkurugenzi wa kampuni ya pia ya Qingdao ambayo bidhaa zake zinauzwa sana katika sehemu nyingi duniani, Bw. Jin Zhiguo alisema kuwa viwanda vya China vinatakiwa kuwa na bidhaa bora zinazopendwa na wateja wa nchi nyingi duniani.

Alisema kuwa bia za Qingdao ni bia za chapa maarufu duniani kutokana na kupendwa na watu wengi wa nchini na wa nchi za nje na kuthibitishwa na mashirika maalumu ya kimataifa. Namna ya kufanya bidhaa hizo zenye chapa maarufu ya China kuwa chapa moja maarufu duniani, inatuhitaji kuwapa furaha wateja wa bia za Qingdao na kuwafanya wateja licha ya kupata furaha, pia tunatakiwa kuwafanya wateja waone kuwa hawakupoteza pesa zao, ila wamenunua bidhaa za maana.

Habari zinasema kuwa pamoja na maendeleo ya uchumi na biashara ya China kwa nje, hatua za maendeleo ya bidhaa bora maarufu zinaharakishwa zaidi. Mwaka huu China itafanya shughuli za kupiga kura kuchagua bidhaa bora maarufu zenye nguvu ya ushindani duniani. Kiongozi wa idara ya usimamizi wa ubora na karantini ya China Bw. Sun Bo alisema kuwa, madhumuni ya kufanya uchaguzi wa bidhaa bora zenye nguvu ya ushindani duniani ni kutumia nafasi hiyo kukuza uzalishaji wa bidhaa hizo, kuhimiza marekebisho ya muundo wa uchumi wa taifa na kubadilisha mtindo wa ongezeko la uchumi ili kuimarisha viwanda bora na kuhimiza bidhaa za viwanda hivyo kuingia kwenye soko la dunia na kuwa bidhaa maarufu duniani.

Idhaa ya Kiswahili 2005-11-01