Syria tarehe 1 iliahidi tena kushirikiana kikamilifu na tume ya uchunguzi ya kimataifa ili kuchunguza ukweli wa mambo kuhusu tukio la kuuawa kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Bw Rafik al Hariri baada ya baraza la usalama kupitisha azimio namba 1636 kuitaka Syria ifanye ushirikiano kikamilifu katika mchakato wa Umoja wa Mataifa kuchunguza tukio la kuuawa kwa Bw Hariri. Lakini Syria inapinga kithabiti nchi za magharibi ikiwemo Marekani kuiwekea shinikizo mara kwa mara kwa kisingizio cha kuchunguza tukio hilo.
Gazeti la Tishrin la Syria tarehe 1 lilichapisha makala ikisema kuwa Syria itashirikiana ipasavyo na tume ya uchunguzi ya kimataifa na kutekeleza ahadi yake. Waziri wa mambo ya uhamiaji wa Syria pia alieleza kuwa Syria inataka kuwatafuta watuhumiwa wa tukio la mauaji hayo kwa kushirikiana na tume hiyo, ili kupata ukweli wa mambo wa tukio hilo. Lakini wizara ya mambo ya nje ya Syria siku hiyo ilieleza siku hiyo kuwa ripoti ya uchunguzi wa mwanzo kuhusu tukio la kuuawa kwa Hariri iliyowasilishwa na mkuu wa kamati hiyo Bw. Detlev Mehlis haiambatani na ukweli wa mambo, na nchi za magharibi ikiwemo Marekani kuhimiza baraza la usalama lipitishe azimio kutokana na ripoti hiyo kutaleta athari ya uzorotaji kubwa kwa Syria.
Siku hiyo, vijana mia kadhaa wa Syria waliandamana katika barabara mjini Damascus kuzilaani nchi za magharibi ikiwemo Marekani kwa kuilaani Syria bila sababu.
Wachambuzi wanaainisha kuwa baada ya kupitishwa kwa azimio namba 1636, Syria inakabiliana na hali mbaya zaidi katika kupambana kisiasa na nchi za magharibi kuhusu tukio hilo.
Kwanza, mkuu wa kamati ya uchunguzi ya kimataifa Bw. Detlev Mehlis tarehe 31 alirudi mjini Lebanon kuendelea na kazi ya uchunguzi. Kutokana na madaraka aliyopewa na baraza la usalama, Mehlis ataweza kuwahoji watuhumiwa wa tukio hilo wakati wowote na mahali popote, pia kuna uwezekano wa kumhoji rais Bashir Al-Assad. Kwa hiyo katika kipindi hiki cha uchunguzi, kama tume hiyo inaona kuwa kama Syria haifanyi ushirikiano kamili na kamati hiyo, Syria itakabiliwa na taabu kubwas zaidi.
Pili, kipindi cha madaraka ya tume ya uchunguzi ya kimataifa kimeahirishwa hadi tarehe 15 mwezi Desemba, lakini muda uliosalia wa kuchunguza tukio la Hariri hautakuwa mrefu. Kwa kuwa azimio namba 1636 limelipa baraza la usalama madaraka ya kuchukua hatua zaidi, kama nchi za magharibi bado zitaona kuwa Syria haikufanya ushirikiano kamili katika kuchunguza tukio hilo, bila shaka zitalihimiza baraza la usalama lichukue hatua zaidi na kuiwekea Syria vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia. Wachambuzi wanaona kuwa ingawa Syria inapinga kithabiti nchi za magharibi kuilaani Syria, lakini bado itaendelea kutekeleza maazimio husika ya baraza la usalama na kushirikiana ipasavyo na kamati ya uchunguzi ya kimataifa.
Kutokana na hayo, Syria iko tayari katika mawazo kushirikiana kikamilifu na kamati hiyo. Lakini kwa kuwa uchunguzi huo unahusikana na mamlaka na heshima ya taifa, rais Bashar wa Syria siku zote alikataa kuhojiwa na tume hiyo kabla ya hapo. Kwa hiyo, kama tume hiyo inataka kumhoji rais huyo au la, na kama rais huyo mwenyewe atakubali kuhojiwa na tume hiyo au la, hilo litakuwa suala gumu kati ya tume hiyo na Syria. Lakini Syria haijali inakabiliana na suala gumu namna gani, itashirikiana na tume hiyo kupata ukweli wa mambo kuhusu tukio la kuuawa kwa Bw Rafik al Hariri haraka iwezekanavyo na kuachana na hali hiyo yenye shida.
Idhaa ya Kiswahili 2005-11-02
|