Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-02 19:45:52    
Mapishi ya vipande vya nyama ya kuku vyenye ladha ya pilipili na pilipili manga

cri

Mahitaji:

Nyama ya paja la kuku gramu 500, nusu ya pilipili mboga, nusu ya pilipili hoho, karanga zilizokaangwa gramu50, mchuzi wa pilipili hoho vijiko viwili, kiasi kidogo cha vipande vya vitunguu maji, vitunguu saumu, tangawizi na pilipili manga na mchuzi vijiko viwili, chumvi kijiko kimoja, sukari vijiko viwili, mafuta ya ufuta kijiko kimoja, wanga kijiko kimoja, na maji bakuli moja.

Njia:

1. kata nyama ya kuku iwe vipande vipande, viweke kwenye bakuli

moja, tia mchuzi wa soya, chumvi, sukari, mafuta ya ufuta na wanga, kisha koroga koroga. Piga karanga zilizokaangwa kwa kisu mpaka ziwe vipande vidogo vidogo. Kata pilipili mboga na pilipili hoho ziwe vipande.

2. Washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vitunguu maji na pilipili manga na kisha koroga koroga, vipakue na tia vipande vya nyama ya kuku, vikaange na vipakue.

pasha moto tena, tia mafuta kidogo na tia vipande vya pilipili mboga na pilipili hoho, vitunguu saumu, tangawizi halafu korogakoroga kwa haraka, tia mchuzi wa pilipili hoho, mimina maji na ukorogekoroge mpaka maji yachemke, tia vipande vya nyama ya kuku korogakoroga halafu vipakue. Mimina vipande vya karanga na vitunguu maji. Kitoweo hiki sasa kiko tayari kuliwa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-11-02