Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-02 20:23:56    
Mpango wa kimataifa wa kuwatibu watoto wenye ugonjwa wa ukimwi waanzishwa

cri
Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa na Shrika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa tarehe 25 mwezi Oktoba zilianzisha mpango wa kimataifa wa kuwatibu watoto wenye ugonjwa wa ukimwi, na kuzitaka pande mbalimbali zilifuatilie suala hilo.

Katibu wa Mfumo wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa Bw. David Bull tarehe 24 alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Xinhua alisema kuwa, mpango huo wa kimataifa unaoitwa "Kuwalinda Watoto, Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi" una lengo la kukusanya nguvu zote ili kutoa misaada ya lazima kwa watoto wanaoteseka na ugonjwa huo. Alisema, katika suala la ugonjwa wa ukimwi, watoto hawajapata ufuatiliaji wa kutosha, ugonjwa huo umewaua watoto wengi, kuwafanya wawe yatima na kubeba mizigo ya familia mapema wakiwa na umri mdogo.

Ripoti iliyotolewa tarehe 25 na Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa imesema kuwa, hivi sasa, mtoto mmoja anakufa kila baada ya dakika moja kutokana na magonjwa yanayohusiana na ukimwi, na mtoto mmoja na vijana wanne wenye umri kati ya 15 na 24 wanaambukiwa virusi vya ukimwi.

Bw. Bull alifahamisha kuwa, mpango huo wa "Kuwalinda Watoto, Kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi" unapanga kuboresha kwa kiasi kikubwa hali ya kinga na tiba kwa watoto dhidi ya ugonjwa wa ukimwi hadi mwaka 2010, na umeweka ratiba ifuatayo: kwanza, kuwakinga watoto wachanga wasiambukizwe virusi vya ukimwi kutoka kwa mama wajawazito, na kutoa matibabu hayo kwa asilimia 80 ya kinamama wenye ugonjwa wa ukimwi au walioambukizwa virusi vya ukimwi kutoka asilimi 10 au chini zaidi ya hivi sasa; pili, kuyafanya matibabu yawafikie asilimia 80 ya watoto wenye ugonjwa wa ukimwi au walioambukizwa virusi vya ukimwi kutoka asilimia 5 au chini zaidi ya hivi sasa; tatu, kupunguza idadi ya vijana wenye ugonjwa wa ukimwi au vijana walioambukizwa virusi vya ukimwi hadi asilimiai 25; nne, kutoa misaada kwa asilimia 80 ya watoto yatima ambao wazazi wao wamekufa kutokana na ugonjwa wa ukimwi.

Bw. Bull alikadiria kuwa mpango huo utahitaji dola za kimarekani bilioni 30 ili kutimiza malengo yake yote, na fedha hizo zitachangiwa na nchi zilizoendelea. Bw. Bull alisema kuwa:"Tunatumai kuwa nchi zilizoendelea zitainua viwangio vya vya misaada, na kuanzisha mfuko maalum wa fedha kwa ajili ya kinga na tiba dhidi ya ugonjwa ukimwi kwa watoto."

Idhaa ya Kiswahili 2005-11-02