Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-02 20:25:59    
Maziwa ya mama yana vitu vinavyoweza kuzuia virusi vya ukimwi visiingie mwilini

cri
Majaribio yaliyofanywa na wanasayansi wa Uholanzi tarehe 23 mwezi Novemba yameonesha kuwa, vitu vyenye sukari vilivyomo ndani ya maziwa ya mama vinaweza kuzuia virusi vya ukimwi visiingie kwenye chembechembe za mwilini. Kama matokeo ya majaribio hayo yatathibitishwa zaidi, yatatoa njia mpya ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.

Virusi vya ukimwi HIV vinaishambulia aina moja ya chembechembe za mwilini, ambazo zinafanya kazi muhimu katika kuwasaidia binadamu kujikinga dhidi ya virusi, kama chembechembe za aina hiyo zikiharibiwa na virusi vya ukimwi, binadamu wako hatari. Vitu vyenye sukari vilivyomo ndani ya maziwa ya mama vinaweza kuzuia virusi vya ukimwi visiingie kwenye chembechembe za aina hiyo, hii inamaanisha kuwa njia ya maambukizi ya virusi vya ukimwi imekatwa.

Wanasayansi wanaona kuwa watoto wachanga wanaweza kupata kiasi kikubwa cha vitu hivyo kwa kunyonya maziwa ya mama, na kupata uwezo wa kujikinga dhidi ya ugonjwa wa ukimwi.

Lakini watafiti wamesema kuwa, matokeo hayo hayamaanishi kuwa akina mama walioambukizwa virusi vya ukimwi wanaweza kuwanyonyesha watoto, kwani watoto wanaonyonya maziwa ya mama walioambukizwa virusi vya ukimwi, nao wataambukizwa virusi vya ukimwi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa, kila mwaka watoto wachanga laki 2 wanaambukizwa virusi vya ukimwi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-11-02