Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-11-03 20:00:48    
Mapambano ya kisiasa yaongezeka kati ya vyama viwili kwenye baraza la juu la bunge la Marekani

cri

Kutokana na madai makali ya wabunge wa chama cha Demokrasia, baraza la juu la bunge la Marekani linalosimamiwa na chama cha Republican lilifanya mkutano wa faragha tarehe mosi kujadili upelelezi wa makosa uliotolewa kabla ya vita vya Iraq na jambo kuhusu kufichuliwa kwa jasusi mmoja wa shirika la upelelezi la Marekani.

Kutokana na kanuni za kawaida za kazi ya baraza la juu la bunge la Marekani, kila mbunge kwenye baraza hilo ana haki ya kutaka kuitisha mkutano wa faragha. Lakini mkutano huo ni mkutano wa kwanza ulioitishwa na baraza la juu kwa kulazimisha na chama kimoja bila kushauriana na chama kingine miaka 25 iliyopita. Vyombo vya habari vya Marekani vilichambua kuwa jambo hilo linaonesha kuwa malumbano ya kisiasa kwenye baraza la juu la bunge la Marekani kati ya vyama viwili vya nchi hiyo yanapamba moto siku hadi siku.

Aliyeongoza kulitaka baraza la juu liitishe mkutano wa faragha ni Bw. Harry Reid, kiongozi wa chama cha Demokrasia kwenye baraza la juu. Alikikosoa chama cha Republican kutoa upelelezi wa makosa kabla ya vita vya Iraq na kutofanya chochote kuhusu kesi ya kufichuliwa kwa jasusi wa Shirika la upelelezi la Marekani. Alisema kuwa serikali ilidhibiti upelelezi na kuifanya Marekani kutumbukiza kwenye matope ya vita, na bunge la Marekani linalosimamiwa na chama cha Republican halikuchukua chochote kuhusu jambo hilo. Baadaye, kutokana na ombi la Bw Harry Reid, wanachama wa Republican ambao ni wabunge wa baraza la juu walilazimika kukubali kuitisha mkutano huo uliofanyika kwa saa mbili.

Kiongozi wa chama cha Republican kwenye baraza la juu Bw. Bill Frist alighadhabishwa sana na jambo hilo. Alisema kuwa wabunge wa chama Demokrasia wameliteka nyara baraza la juu, kitendo hicho ni kuwapuuza viongozi wa baraza la juu na kumwaibisha. Amelaani kitendo hicho cha wabunge wa chama cha Demokrasia kuwa ni kitendo cha kuwafukuza wananchi wa Marekani.

Katika kipindi cha hivi karibuni, wabunge wa chama cha Demokrasia wamekatishwa tamaa na vitendo mbalimbali vya serikali ya Bush. Idadi ya vifo vya askari wa jeshi la Marekani nchini Iraq imezidi 2000, mkurugenzi wa ofisi ya makamu wa rais Bw. Lewis Libby alijiuzulu kutokana na kuhusika na kutoa ushahidi wa uwongo kwenye kesi ya kufichuliwa kwa jasusi wa shrikila la upelelezi la Marekani, uchunguzi uliofanywa na tume ya upelelezi ya baraza la juu haujathibitishwa na rais Bush alimteua mwanasheria wa kundi la wahafidhina kuwa jaji wa mahakama kuu ya shirikisho la Marekani, yote hayo yamekuwa visingizio vya chama cha Demokrasia vya kuishutumu serikali na wanachama wa Republican.

Wachambuzi waliainisha kuwa hivi karibuni rais Bush wa Marekani amekosolewa kwa mambo mbalimbali na kukumbwa na janga katika mambo ya kisiasa na mambo yanayotakiwa kujadiliwa kwenye mkutano wa faragha na baraza la juu yanamlenga Bush.

Mwenyekiti wa tume ya upelelezi ya baraza la juu, mwanachama wa chama cha Republican Bw. Pat Roberts alieleza tena kuwa tume yake imepata maendeleo katika uchunguzi wa kipindi cha pili kuhusu upelelezi wa makosa uliotolewa kabla ya vita vya Iraq. Lakini wanachama wa chama cha Republican wanafanya ujanja wa kutumia mkutano huo wa faragha. Jambo linalopaswa kuzingatiwa ni kuwa Ikulu ya Marekani bado haijatoa maelezo kuhusu mkutano huo. Rais wa zamani Bw. Jimmy Carter alieleza kuunga mkono kitendo cha chama cha Demokrasia. Kwa hiyo vyombo vya habari vya Marekani vinaona kuwa msukosuko huo wa kisiasa hautatulia hivi karibuni.